Watu waanza kujitolea kushiriki majaribio ya chanjo mpya corona

Iliyochapishwa

Watu waliojitolea kutumiwa kwa ajili ya majaribio ya chanjo mpya wameanza kupewa kinga ya chanjo mpya ya virusi vya corona nchini Uingereza.

Takriban watu 300 watadungwa chanjo hiyo katika kipindi cha wiki kadhaa zijazo, kama sehemu ya majaribio yanayoongozwa na Profesa Robin Shattock na wenzake, katika Chuo cha Imperial mjini London.

Vipimo walivyofanyiwa wanyama vilionesha kuwa chanjo hiyo ni salama na inachochea ufanisi wa kinga ya mwili katika kukabiliana na virusi hivyo.

Wataalamu katika Chuo Kikuu cha Oxford tayari wameanza majaribio ya chanjo kwa binadamu.

Majaribio haya ya chanjo ni miongoni mwa majaribio mengi yanayofanyika kote duniani- mipango 120 ya kutafuta chanjo ya corona ikiripotiwa kuendelea duniani..

Kathy, mwenye umri wa miaka 39, anayefanya kazi katika masuala ya fedha, ni mmoja wa watu wa kwanza waliojitolea kushiriki majaribio ya chanjo yanayofanyika katika taasisi ya Imperial.

Anasema kuwa alijitolea kwasababu alitaka kushiriki katika mapambano dhidi ya virusi vya corona.

"Ninadhani ilikuja sio kutokana na kufahamu hasa ni nini ninachoweza kufanya katika kusaidia, na hiki kikaonekana kwangu kwamba ni kitu ninachoweza kukifanya kusaidia.

"Na kuelewa kwamba huenda mambo yasirejee katika hali ya kawaida hadi tutakapokua na chanjo, kwa hiyo nilitaka kuwa sehemu ya mchakato huo pia."

Baada ya awamu hii, jaribio lingine limepangwa kufanyika mwezi Oktoba, likiwahusisha watu 6,000.

Wataalamu katika taasisi ya Imperial wana matumaini kuwa chanjo hiyo inaweza kusambazwa nchini Uingereza na mataifa mengine kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2021.

Wakati huo huo Mwanamfalme wa Uingereza William -Duke of Cambridge alikuna na watu waliojitolea kufanyiwa majaribio ya chanjo hiyo yanayofanyika katika Chuo kikuu cha Oxford katika Hospitali ya Churchill.

Mwanamfalme William aliwaambia wanaojitolea kuwa : "Ni jambo la kusisimua sana na ni mradi ambao umekubalika , na kwa kuwa nyote mmekubali kushiriki ndio maana unavutia."

Utendaji mpya

Chanjo nyingi hudhoofisha au kubadili muundo wa kirusi au sehemu yake, lakini chanjo ya Imperial imetengenezwa kwa utaalamu mpya, wakitumia aina ya mfano wa jeni, inayoitwa, RNA, ambayo inafanana na virusi.

Dungwa kwa njia ya sindano ndani ya misuli, RNA -hutengeneza nakala zake na kuchochea seli za mwili zenyewe kutengeneza nakala zake za protini zinazochipuka ambazo kwa kawaida huchipuka nje ya virusi kama vile unavyoviona nje ya kirusi cha corona.

Hii inapaswa kuufunza mfumo wa kinga ya mwili kutambua na kupambana na virusi vya corona bila kusababisha ugonjwa wa Covid-19.

UCHAMBUZI

Kwasababu ni kiwango kidogo tu cha aina ya jeni kinachotumika katika chanjo ya Imperial, ni kiasi kidogo chanjo hiyo itawafikia watu wengi. Timu ya wataalamu katika Imperial inasema kuwa lita moja tu ya chanjo hiyo itatosha kutengeneza dozi milioni mbili. wakati zitakapohitajika kutengenezwa nyingi , zinaweza kufanyika Uingereza .

Majaribio yote ya tiba huanza kwa umakini na taratibu ili kupunguza hatari za usalama . Wakati chanjo ya Oxford ilipoanza mwezi Aprili, ni watu wawili tu waliopewa kinga siku ya kwanza. Katika kipindi cha wiki moja, katika muda wa wiki moja watu 100 wamekua wakidungwa dawa hiyo kila siku.

Upekee wa chanjo ya Imperial unamaanisha kwamba ni mtu mmoja pekee atakua anapewa kinga kwa siku ya kwanza, akifuatiwa na watatu kila baada ya saa 48. Baada ya wiki moja au zaidi idadi ya watu itakua imeongezeka.

Tofauti na chanjo ya Oxford, inayotumia dozi moja, wanaojitolea kwa ajili ya kufanyiwa chanjo ya Imperial watapewa dozi mbili, wiki nne tofauti

Profesa Shattock na timu yake wanasema hapakua na hofu yoyote katika dawa yao- ni upya tu wa utengenezaji wake ndio unaowafanya waendelee kuwa na tahadhari.

Kuna chanjo zaidi ya 120 za virusi vya corona ambazo ziko katika utafiti wa awali kote duniani. Nyingi kati ya chanjo zitaishia katika maabara. Nyingine 13 kwa sasa ziko katika majaribio ya kimatibabu tano nchini Uchina, tatu Marekani, mbili Uingereza, moja Australia, Ujerumani na Urusi.

Timu zote za chanjo ziko makini kusisitiza kwamba haziko katika mbio za kushindana miongoni mwao, bali dhidi ya virusi. Majaribio kadhaa ya chanjo yatahitajika kufanikiwa ili kuiwezesha dunia kuwa na dozi za kutosha kuilinda dunia.

Profesa Shattock amesema: "Tumeweza kutengeneza chanjo kuanzia sasa na tunaweza kufanya majaribio ya chanjo hii kwa binadamu kwa miezi michache tu.

" Kama mtindo wetu utafanikiwa na kuweza kutoa chanjo yenye ufanisi dhidi ya ugonjwa, inaweza kuwa ni mageuzi makubwa juu ya namna tunavyoshughulikia milipuko ya magonjwa katika siku zijazo."

Mkuu wa uchunguzi wa utafiti, Dokta Katrina Pollock, aliongeza kuwa: "Nisingekua nafanya kazi ya jaribio hili nisingehisi kuwa mwenye matumaini kwamba tutashuhudia kinga ya mwili ya washiriki ikikabiliana na virusi.

"Data za awali za kimatibabu zinaonesha matumaini ya mafanikio katika chanjo. Tunapata jibu la kingamwili ambayo kinga ya mwili inataka kujilinda dhidi ya maambukizi. Lakini bado tuna kazi kubwa ya kutathimini chanjo hii ."

Utafiti huo umedhaminiwa na serikali ya Uingereza kwa pauni milioni 41, pamoja na pauni milioni 5 za misaada mingine.