Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Idadi ya wagonjwa wa corona Kenya yaongezeka hadi kufikia 2767
Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 2,767 baada ya wagonjwa wengine 167 kupatikana na virusi hivyo kutoka sampuli 2,833 zilizofanyiwa vipimo.
Akitoa taarifa za kila siku kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba wagonjwa hao wapya wanaume 125 na wanawake 42.
Bwana Kagwe amesema hatahivyo wagonjwa wengine 46 wamepona, hatua inayoongeza idadi ya wagonjwa waliopona kufikia 752.
Amesema kwamba mgonjwa mwingine mmoja amefariki kwa ugonjwa huo na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 84.
Aliongezea kwamba msimamo wa serikali kuhusu kufunguliwa kwa baa na maduka ya kuuza pombe utasalia ilivyo.
''Ufunguzi wa baa na uuzaji wa pombe utaendelea kuzuiwa, wale watakaokiuka sheria hiyo leseni zao zitafutiliwa mbali'', alisema.
Wagonjwa hao wanashirikisha Wakenya 159, raia 4 wa Eritrea na raia wa Sudani Kusini.
Wagonjwa 54 wanatoka katika kaunti ya Nairobi, 47 kutoka kaunti ya Mombasa, 28 kutoka Busia, 14 kutoka Kiambu , 11 kutoka Uasin Gishu, 4 kutoka Kisumu, 4 wengine kutoka Machakos na mgonjwa mmoja mmoja kutoka Homa Bay, Makueni, Migori, Siaya na Turkana.
Serikali imesema itaingilia kati moja kwa moja hali ya katika kaunti ya Busia kwasababu ya ongezeko la madereva wa malori wanaokutwa na maambukizi ya virusi vya corona, alieleza Waziri Kagwe akiongeza kuwa miongoni mwa waliopatwa na maambukizi ni mtoto wa miezi 11.