Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Virusi 4 ambavyo bado havijapata chanjo hadi sasa na jinsi tulivyojifunza kuishi navyo
Mamilioni ya watu kote duniani wana matumaini kwamba ugonjwa wa Covid-19 hatimae utadhibitiwa kutokana na chanjo itakayopatikana.
Hata hivyo wataalamu wameonya kwamba hata kuharakisha kutafuta chanjo kunaweza kuwa kunapoteza muda zaidi au kibaya zaidi hata chanjo hiyo inaweza isipatikane.
"Kuna uwezekano ukawa ni ugonjwa wa virusi unaosambaa hasa miongoni mwa jamii na virusi hivi huenda visiishe," amesema mkurugenzi wa masuala ya afya ya dharura wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Michael Ryan.
Ingawa uwezekano wa kuishi na virusi hivi kunaweza kuwa na madhara makubwa kwa wengi wakati ambapo idadi ya waliothibitishwa kupata maambukizi imezidi milioni 5.4 na idadi ya waliokufa kote duniani ikifikia 350,000 hilo halitakuwa jambo la kustaajabisha.
Pia vilikuwa na athari mbaya kwa maisha ya watu ya kila siku kwasababu viliwalazimisha kubadili baadhi ya mienendo ya kufanya ngono kwasababu hiyo ilikuwa ndio njia moja kuu ya maambukizi.
Ukweli wa kwamba waathirika wengi wa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi, walikuwa ni wapenzi wa jinsia moja na ugonjwa huo ukawa ni wenye kusababisha fedheha kubwa katika jamii kiasi kwamba baadhi ya vyombo vya habari walitambua 'Ukimwi kama saratani ya wapenzi wa jinsia moja.'
Miongo karibia minne sasa na bado chanjo dhidi ya HIV haijapatikana ukiwa umeambukiza watu takribani milioni 40 kote duniani, na ukweli ni kwamba virusi hivi bado vipo sana na vitaendelea kuishi na mwanadamu kwa kipindi kirefu kijacho.
Hata hivyo, maendeleo ambayo yamepatikana katika njia za kuzuia maambukizi na tiba yake yamepunguza idadi ya vifo lakini upande mwengine HIV sasa imekuwa ni tatizo sugu la kiafya ambalo halizui wale walioathirika kuishi maisha ya kawaida.
1. Virusi vya ukimwi
Zaidi ya miaka 30 imepita tangu wanasayansi waliopofanikiwa kutenga virusi ya HIV, ambavyo vinasababisha ugonjwa wa (UKIMWI).
Kuanza kujulikana kwa virusi vya HIV kulisababisha madhara makubwa kwasababu maambukizi yake yalikuwa ni sawa na kifo.
Virusi hivi vimekuwa sababu ya vifo kwa zaidi ya watu milioni 32 kulingana na idadi ya WHO.
Miongo karibia minee sasa na bado chanjo dhidi ya HIV haijapatikana ukiwa umeambukiza watu takribani milioni 40 kote duniani, na ukweli ni kwamba virusi hivi bado vipo san ana vitaendelea kuishi na mwanadamu kwa kipindi kirefu kijacho.
Hata hivyo, maendeleo ambayo yamepatikana katika njia za kuzuia maambukizi na tiba yake kumepunguza idadi ya vifo lakini upande mwengine HIV sasa imekuwa ni tatizo sugu ya kiafya ambalo halizui wale walioathirika kuishi maisha ya kawaida.
Hivi karibuni, kumekuwa na visa ambapo waathirika wawili wa virusi vya ukimwi walipona kupitia matibabu ya seli.
Hata hivyo, wataalamu wameonya kwamba tiba hiyo ni hatari mno na haiwezi kutumika kutibu wote walioathirika na ugonjwa huo.
2. Homa ya Avian
Tangu miaka ya 1990, homba mbili zimebainiwa ambazo ziliathiri binadamu na watu wengi wakaaga dunia.
Virusi hivyo ambavyo vinasambazwa kwa ndege na baadae vikasambaa hadi kwa mwandamu kupitia kutangamana nao au kwa kitu ambacho kimeambukizwa na kinyesi cha mnyama ambaye ni mgonjwa.
Mwaka 1997, mwathirika wa kwanza wa H5N1 alibainika huko Hong Kong, na kupelekea kuchinjwa kwa kuku wote waliokuwa hai eneo hilo.
Tangu wakati huo, walioambukizwa homa hiyo wamekuwa wakiripotiwa katika zaidi ya mataifa hamsini barani Afrika, Asia na Ulaya huku kukitokea asilimia 60 ya vifo.
Homa ya A H7N9 mara ya kwanza kugunduliwa ilikuwa ni Mei 2013 nchini China, ambapo hadi kufikia sasa milipuko kadhaa imeripotiwa.
Kulingana na WHO, kati ya 2013 na 2017 maambukizi 1,565 kwa binadamu yalithibitishwa ambapo asilimia 39 walikufa.
Ingawa homa zote hizo zimesababisha kiwango cha juu cha vifo, kulingana na WHO, ni nadra sana kwa virusi hivyo kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine.
Na baada ya hilo kuthibitishwa ilikuwa rahisi kusitisha usambaaji wake.
3. Ugonjwa wa SARS
Mara ya kwanza kugunduliwa ni mwaka 2003, ambapo ugonjwa wa SARS-CoV ni aina ya virusi vya corona ambao unaaminika kusambazwa kwa binadamu kupitia mnyama, anayeshukiwa kuwa popo.
Maambukizi ya kwanza yalisajiliwa 2002 katika mji wa Guangzhou nchini China.
Virusi hivi vilikuwa ndi sababu ya janga kubwa la ugonjwa wa matatizo ya kupumua wa (SARS) ambao 2003 uliathirini nchi 26 huku zaidi ya watu 8,000 wakiathirika.
Tangu wakati huo, idadi ndo tu ya maambukizi ndio ambayo imethibitishwa.
Tofauti na homa ya avian, virusi hivi vinaweza tu kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengne na wengi waliwa wamepata maambukizi katika vituo vya afya kwasababu tahadhari stahiki haikuwa imechukuliwa ili kuzuia usambaaji wake.
Kulingana na WHO, hatua hizo zilipochukuliwa, janga hilo lilimalizika Julai 2003.
Hadi kufia wakati huo, zaidi ya watu 8,400 wamethibitishwa kupata maambukizi pamoja na vifo 916 ikiwa ni karibia asilimia 11%.
4. Ugonjwa wa MERS
MERS-CoV ni ugonjwa aina ya virusi vya corona. Mara ya kwanza kugundulika ilikuwa ni 2012 na ndio chanzo cha ugonjwa wa Middle East respiratory syndrome (MERS).
Ni ugonjwa wa virusi ambao umesababisha idadi kubwa ya vifo mingoni mwa 2,494 idadi ya walithibitishwa kupata maambukizi kote duniani hadi kufikia Novemba 2019, vifo vikiwa ni 858.
Ugonjwa huo wa virusi mara ya kwanza ulibainika Saudi Arabia lakini wakati huo pia ulibainika nchi 27 ikiwemo 12 kutoka Mashariki ya Kati.
Kulingana na WHO, wengi waliobainika kupata maambukizi ya ugonjwa huo nje ya nchi za Mashariki ya Kati walikuwa wamepata maambukizi hayo wakiwa kwenye nchi hizo.
Ugonjwa huo wa virusi unasambazwa kutoka kwa Wanyama hadi kwa wa tuna hususan, huku mnyama ngamia akiaminika kuwa chanzo cha maambukizi hayo.
Maambukizi ya binadamu hadi kwa binadamu ni nadra sana kutokea labda kuwe na utangamano wa karibu sana na mnyama huyo bila kuchukuliwa kwa hatua stahiki za kujilinda.
Kwa ugonjwa wa MERS, kama ilivyo kwa ugonjwa wa SARS, baada ya kudhibiti maambukizi ya juhudi za kutafuta chanjo zilisitishwa.