Virusi vya corona: Kuvuruga utaratibu wa chanjo kwa watoto kutasababisha vifo vinavyoweza kuepukika

Iliyochapishwa

Mamilioni ya watoto wanaweza kupoteza maisha kutokana na maradhi yanayoweza kuzulika kwa sababu ya kukatizwa kwa programu za chanjo kutokana na virusi vya corona, wataalam wametahadharisha.

Takribani nchi 68 zimeathirika - baadhi zikisitisha kabisa kampeni za chanjo.

Shirika la Afya duniani limeshauri nchi nyingi kusitisha chanjo ili kusaidia kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Lakini sasa makundi kadhaa ya wataalamu wanaona kuwa kutakuwa na madhara ya muda mrefu kutokana na hali hii.

Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia watoto (Unicef), Taasisi ya chanjo, Sabin na Shirika la Chanjo la Gavi pia yameonesha wasiwasi kuwa maelfu ya watoto watapoteza maisha kwa sababu zinazoweza kuzuilika.

Katika hospitali ambayo kwa kawaida hujaa Mji mkuu wa Niger, Niamey ,chumba cha kusubiri huduma kiko kimya.

Kuna ripoti ya kuwepo kwa wagojwa karibu 1,000 wa virusi vya corona nchini humo.

Lakini Polio, ambayo inaweza kusababisha kupooza au hata kifo, pia inarejea- wagonjwa wanne wapya wa polio wameripotiwa tangu mwezi Februari.

Zeinabou Tahirou amekaa akiwa amevaa kilemba chake na barakoa ya buluu, akiwa amempakata mtoto wake wa kike, Fadila.

''Nilikuwa nina hofu kuja hapa, kwa sababu ya virusi vya corona,'' alisema.

''Lakini wahudumu wa afya waliniambia jinsi chanjo ilivyo muhimu, na pia niachotakiwa kufanya ili kubaki salama-kama vile kunawa mikono mara kwa mara.''

Kuna sababu kadhaa huduma ya chanjo kuvurugwa, ikiwemo:

Wazazi kuhofu kupata maambukizi ya Covid-19 ikiwa watatoka nje ya nyumba zao.

Wahudumu wa afya wakielekeza nguvu yao kuhudumia matatizo mengine kama kupata vifaa vya chanjo hospitalini.

''Surua iko juu, kuhara, kipindupindu,'' Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia watoto (Unicef) Henrietta Fore ameeleza.

''Hivyo hili litakuwa tatizo kweli. Kama dunia tumepambana na maradhi mengi ya watoto.''

Karibu watoto milioni 80 walio chini ya mwaka mmoja wako hatarini

Wastani wa idadi ya wtoto wanaokosa chanjo kwa sababu ya janga la virusi vya corona:

  • Asia Mashariki- watoto milioni 34.8
  • Afrika -watoto milioni 22.9

Milipuko ya sasa ya magonjwa yanayoweza kuzuilika:

  • Nepal na Cambodia - surua
  • Ethiopia - surua ,kipindupindu na homa ya manjano

Chanzo: WHO, Unicef, Sabin na taasisi ya chanjo na shirika la chanjo Gavi.

Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya Johns Hopkins kutopata huduma hii muhimu kwa wanawake na watoto kunaweza kusababisha ongezeko la watoto 6,000 wanaokufa kila siku.

''Tunachokitegemea kwenye maradhi haya ni kwamba yatarejea tena kwa kasi,'' anaeleza Mkuu wa WHO idaya ya chanjo Kate O'Brien.

''Na hii ina maana kuwa tutashuhudia vifo vingi vya watoto .''Lakini hali hii bado inaweza kudhibitiwa, ''ikiwa serikali zitachukua hatua sasa''.

Tahadhari hii imekuja wakati viongozi wa dunia wanakutana kwa ajili ya mkutano wa dunia wa chanjo, hii leo, Uingereza ikiwa mwenyeji wa mkutano huo mwaka huu.

Taarifa zaidi kurusu virusi vya corona: