#HakiKwaUwa, kampeni ya mtandao baada ya mwanafunzi kuuawa kanisani Nigeria

Chanzo cha picha, UWAVERA OMOZUWA/FACEBOOK
Kuna ghadhabu nchini Nigeria baada ya mauaji ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22, Uwavera Omozuwa aliyeuawa kanisani.
Kampeni ya hashtag #JusticeForUwa au # HakiKwaUwa imeenea kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria, huku familia yake ikiomba msaada wa kumtafuta aliemuua.
Uwavera alikua anajisomea katika kanisa "tulivu" karibu na nyumbani Benin City wakati alipouawa, dada yake, Judith, aliiambia BBC idhaa ya Pidgin.
Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa muuguzi alikufa hospitalini siku ya Jumamosi, siku tatu baada kushambuliwa.
Judith Omozuwa alisema kuwa dada yake alibakwa.
Familia yake ilisema kuwa ilipokea simu kutoka kwa mwanamke kutoka kanisa la Redeemed Christian Church of God siku ya Jumatano jioni.
Uwavera alipelekwa hospitalini baada ya mlinzi kumpata, sketi yake ikiwa imechanika na blauzi yake ikiwa imejaa damu, Judith Omozuwa alisema.
'Kushindwa kukabiliana na unyanyasaji wa jinsia '
Hatahivyo, msemaji wa polisi katika jimbo la southern Edo, ambalo mji mkuu wake ni Benin City, ameiambia BBC Idhaa ya Pidgin kwamba wanashughulikia tukio hilo kama mauaji, si kesi ya ubakaji.
Mwanafunzi huyo aliuawa kufuatia mapigano katika kanisa, msemaji aliongeza, bila kutoa maelezo zaidi.
Uwavera alikua ndio tu amedahiliwa katika Chuo Kikuu cha Benin kusoma microbiolojia.
Mara kwa mara alikwenda kukaa na "kusoma" katika kanisa karibu na nyumbani kwao kwasababu kulikuwa na utulivu, dada yake aliongeza kusema.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa katika vyombo vya habari nchini humo zinasema kuwa kikundi cha wanaume kiliingia kanisani na kumbaka na baadae kumgonga na kifaa cha kuzima moto (fire extinguisher).
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Jumanne, Wanigeria wengi walikasirika baada ya polisi kudai kumpiga risasi msichana mwenye umri wa miaka 16, Tina Ezekwe katika mji wa kibiashara - Lagos.
Afisa huyo alikamatwa, polisi ilisema.
Katika Twitter, Wanigeria wengi walielezea hojfu yao juu ya kushindwa kwa serikali kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia, na kuhoji iwapo wazazi wanawalea wavulana ipasavyo.












