Virusi vya corona: Madaktari wataja mchanganyiko wa dawa unaoweza kutibu Covid-19

Chanzo cha picha, Getty Images
Dkt John Wright kutoka Bradford Royal Infirmary (BRI) anaelezea baadhi ya majaribio yanayoendelea kwa ajili ya kupata tiba ya Covid-19, na mchanganyiko wa aina tatu za dawa ambazo zinaweza kuwa ufunguo wa tiba ya corona.
Katika taasisi ya BRI kwa sasa tunafanya majaribio manane ya matibabu kujaribu kupata dawa ya Covid-19.
Sisi ni sehemu ya juhudi kubwa za kimataifa. Ni kama mwangaza wa sayansi ya dunia uliojikita moja kwa moja katika virusi hivi visivyoonekana.
Mojawapo ya majaribio makubwa zaidi tunayoshiriki ni jaribio la Kupona. Tayari zaidi ya wagonjwa 10,00 wamekusanywa kote nchini na wanatumia mojawapo ya dawa kadhaa zinazofanyiwa utafiti .
Wiki iliyopita katika taasisi ya BRI tulimchukua mmoja wa wagonjwa nchini Uingereza kwa ajili ya jaribio kuona iwapo dawa iliyotengenezwa AstraZeneca ni salama na yenye ufanisi . Hii ni moja ya majaribio madogo madogo ya pamoja yanayoitwa kitaalamu Accord trial - yaliyobuniwa ili kutathimini zaidi dawa ambayo inaweza kuongezwa Majaribio ya kupona-Recovery trial.
Matumaini ni kwamba hii dawa ya Astra Zeneca, ambayo bado haina jina, itasaidia kuondoa hatari ya ukali zaidi wa virusi kwa mfumo wa kinga ambao hutokea miongoni mwa wagonjwa wachache wa corona, na kuuweka mwili katika hali ya mshituko na kuharibu kabisa ufanyaji kazi wa viungo vya ndani vya mwili kama vile mapafu, moyo mishipa ya damu na figo.
Ukali huu wa kupindukia wa virusi umeitwa "cytokine storm" - cytokines zikiwa ni molekyuli ambazo huashiria uwepo wa maambukizi ambayo ni lazima mwili upambane nayo. Dawa katika majaribio mapya huzuia cytokine inayoitwa IL-33 (or interleukin-33).

Chanzo cha picha, Mark Winterbourne
Mark Winterbourne, ambaye alijitolea kufanyiwa utafiti wa dawa ya IL-blocker, aliwasili katika hospitali akiwa na dalili ambazo kwa mara ya kwanza zilidhaniwa kuwa ni za maradhi ya kibofu cha mkojo.
Baada ya kupimwa alipatikana Covid-19 ndipo tulipogundua kuwa hiki ndio kilikuwa ni chanzo cha tatizo . (Covid-19 ni ugonjwa ambao unadalili tofauti-lakini hiki hakikua kisa cha kawaida , alisema Mark anasema mgonjwa anayekuja kujitolea huja kwa njia ya kawaida kwake, wakati nilipokua anafanya kazi ya kujitolea kama mpiga picha ya Mkimbiaji mashuhuri, alikutana na kuwa rafiki na mkimbiaji Sir Mo Farah.
Ninashuku kwamba chanjo ya Covid-19 itapatikana baada ya kwa hiyo utafutaji wa majaribio haya ya tiba ni muhimu.
Madaktari hapa wanaangalia mbele ya muda-sio mbali sana, wanatumaini-wakati yeyote -mwenye dalili za mapema ataweza kwenda katika kituo cha kupima, achukuliwe vipimo na kupata majibu haraka na kuandikiwa mchanganyiko wa dawa zenye ufanisi, kabla dalili hazijawa mbaya.
Mchanganyiko huu unaweza kujumuisha dawa za kupunguza makali ya virusi -antiviral drug, dawa ya kuzuia kuharibu kazi ya mfumo wa kinga ya mwili, na dawa ya kuzuia uvimbe mwilini -anti-inflammatory drug.
Miongoni mwa dawa za kupunguza makali ya virusi ama antivirals zinazofanyiwa uchunguzi, moja inaweza kuzuia virusi vya corona kuganda katika ukuta wa mapafu, na nyingine inaweza kusaidia kuvizuia kuzaliana tena mwilini .
Dawa za kuzuia mfumo wa kinga zinaweza kusaidia kuzuia mfumo wa kinga kupambana kupita kiasi na virusi - the cytokine storm. Kama dawa ya kuzuia IL-33 kutoka kwa Mkataba wa majaribio -Accord trial ina ufanisi, itakua miongoni mwa dawa zitakazokuwa miongoni mwa zile zitakazoshindania kutibu virusi vya corona.
Dawa za kuzuia uvimbe unaotokana na mwili kukabiliana na maambukizi Anti-inflammatory drugs ni pamoja na steroids - kwa mfano Dexamethasone, moja ya dawa za kwanza zilizojumuishwa katika majaribio ya dawa za kupona- au Recovery trial.

Chanzo cha picha, Tom Lawton
Kilichogunduliwa na madaktari wanaotibu Covid-19
Prof John Wright, daktari na mtaalamu wa magonjwa ya majanga, ni mkuu wa taasisi ya utafiti wa tiba ya Bradford- Bradford Institute for Health Research, na mzoefu wa tiba za kipindupindu, HIV na Ebola katika mataifa yaliyoko kusini mwa jangwa la sahara. Anaandika maelezo haya kwa ajili ya BBC na anarekodi kutoka katika Wodi za hospitali kwa ajili ya BBC Radio.
Inaelekea ni jambo ambalo huenda lisiwezekane kwamba dawa moja itatibu Covid-19. Inadhaniwa kuwa mchanganyikowa dawa ambazo zamani zilitumiwa kutibu Kifua kikuu-zenye mchanganyiko wa dawa za kukabiliana na maambukizi - antibiotics - na HIV - na mchanganyiko wa dawa za kupunguza makali ya za antiretrovirals - na ninatarajia kuwa itakuwa ndio njia ya kumaliza ugonjwa huu pia.
Daktari wa taasisi ya BRI wa magonjwa ya mfumo wa kupumua Dinesh Saralaya anaimani kuwa mchanganyiko wa dawa ya tiba utapatikana hivi karibuni.
" Ninadhani tutapata walau dawa mbili au tatu ambazo zitawazuwia wagonjwa hawa kuhitaji kamwe kwenda hospitalini ," anasema.
"Utakwenda kwenye kituo cha kupimwa na halafu upewe madawa baada ya kupatikana na virusi vya corona. Chini ya mikakati ya sasa, unapata virusi vya Covid, kwa hiyo unatengwa, halafu unaugua sana, unapata joto kubwa la mwili, unaanza kushindwa kupumua, halafu ndio unaingia hospitalini. Lakini watu wanahitaji kupewa madawa mapema sana ."
Daktari wetu mwingine anaweza kuwa anachangia katika utafiti mwingine-kama mtoaji wa vimelea wanaoshambulia kinga ya mwili.
Debbie Horner alipata Covid-19 mwanzoni kabisa mwa mlipuko na akapona haraka .Wiki mbili zilizopita, wakati nilipowaita kuwatembelea watu kama yeye kuwataka watoe damu zao ilizichukuliwe sampuli za plazma, alikubali mara

Chanzo cha picha, Debbie Horner
Watafiti walitaka kubaini ikiwa plazma kutoka kwa watu hao zina Covid-19 zingesaidia wagonjwa wengine kupambana na ugonjwa wa corona. Kazi hii pia ni sehemu ya majaribio ya kupona- Recovery trial.
Imegunduliwa sasa kwamba wagonjwa ambao wana uwezekano wa kuwa na viwango vya juu vya plazma ni wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 35 ambao waliugua sana walihitaji matibabu ya hospitali.
Taasisi ya taifa la Uingereza ya matibabu kitengo cha damu - NHS Blood and Transplant (NHSBT) inatafuta watu waliopona Covid-19 ambao ni wanaume , au wenye umri wa zaidi ya miaka 35 wa kujitolea , au ambao waliugua hadi kulazwa hospitalini ili kufanyiwa utafiti huo unaohusishwa na seli nyeupe za damu.
Debbie aliugua kijdojgo Covid-19 kwa hiyo kuna uwezekano kwamba plazma hazina uwezo mkubwa wa kupambana na ugonjwa zikilinganishwa na zile za kusababisha ugonjwa kulingana na maoni ya timu ya utafiti .Matokeo bado hayajatolewa. Kama seli zake nyeupe zitahitajika anafurahi kujitolea kutoa sampuli yake kwa ajili ya utafiti wa dawa.
"Ni tofauti kidogo na kuchukuliwa damu kawaida ," anasema. "Wanachukua sehemu ya damu yako-sehemu ya plazma-na wanakurudishia seli zako zote nyekundu na sehemu nyingine ya damu ambayo haihitajiki kwa hiyo kusema ukweli, ni kama tu unajihisi umeishiwa na maji mwilini kidogo ."
Vikombe vichache vya chai vinatosha kukufanya urejee katika hali ya kawaida,Debbie anasema.

Chanzo cha picha, NHSBT
Mike Murphy, Profesa wa kitengo cha dawa kinachohusika na uongezaji wa damu mwilini katika chuo kikuu cha Oxford, anasema hii ni fursa kubwa ya kuelewa zaidi juu ya thamani ya kuongezewa utando wa seli mwilini kwa ujumla. Seli nyeupe zilikusanywa mwishoni mwa miaka ya 2000 kuangalia iwapo inaweza kuwa njia ya kuwatibu watu wenye Ebola na mafua, anasema.
"Lakini wakati kulipokua na watoaji wa utando wa seli hizi ambao walikua wamepona maambukizi, na kuweza kutoa sampuli zao, maambukizi yalipungua, kwa hiyo kulikua hakuna fursa ya kupima faida ya Plazma. Janga la Covid-19 ni tohfauti bila shaka ."













