Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Utendakazi wa viongozi wapya Sudan wafichuliwa
Katika mfululizo wa makala kutoka Afrika, mwandishi wa habari wa Sudan Zeinab Mohammed Salih anasema serikali iliyochukuwa hatamu ya uongozi baada ya kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir- kung'olewa madarakani imeshindwa kukabiliana na janga la corona.
"Tulifanikiwa kumuondoa Omar al-Bashir. Lakini mbona tumeshindwa kukabiliana na kirusi kidogo cha corona?" anauliza Akram al-Tom, waziri wa afya wa Sudan, licha ya ongezeko la maambukizi ya Covid-19 Magharibi mwa Ulaya na Marekani mwezi Machi.
Sudan kufikia sasa ina idadi ya juu ya watu walioambukizwa corona (zaidi ya 2,000) na vifo (karibu 100) katika eneo la Afrika Mashariki, baadhi ya watu wanaendelea kuuliza maswali.
Lakini Bw. Tom amekuwa akikwepa vyombo vya habari.
Wizara ya Afya imesitisha mazungumzo na wanahabari - ili kuzingatia amri ya watu kutokaribiana - japo haijabainika kwanini haiwezi kufanya hivyo kupitia mifumo mingine ya kidigitali.
Magazeti yaliacha kuchapishwa
Kutokaribiana sio jambo ambalo linazingatiwa na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok na mawaziri wake baada ya kuonekana katika kanda ya video wakiwa uwanja wa ndege mjini Khartoum wakipokea mwili wa waziri wa ulinzi Gamal Omer aliyefariki ghafla Sudan Kusini mwisho wa mwezi Machi.
Pia walipuuza agizo la kutokaribiana wakati wa mazishi nyumbani kwake, licha ya onyo la majirani wao kuhusu hatari ambayo huenda ikasababishwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Bw. Tom huonekana angalau mara moja kwenye televisheni, lakini kuna taarifa ambayo imerekodiwa lakini kuangazia idadi ya watu walioambukizwa Covid-19 na waathiriwa wa ugonjwa huo.
Na habari zimekuwa finyu baada ya wenye magazeti kupunguza uchapishaji kutokana na kupungua kwa mauzo.
Baada ya amri ya kutotoka nje kuwekwa, habari zinapatikana mitandaoni pekee.
Hii inamaanisha raia wengi wa Sudan hawapati taarifa kwasababu huduma ya mtandao haijafika katika maeneomengi nchini humo - kulingana na baadhi ya takwimu zilizopo ni asilimia 26 pekee ya watu walio na uwezo wa kupata huduma hiyo.
Hali hiyo imewaacha watu na maswali ikiwa serikali inayojumuisha majenrali wa kijeshi na raia- inaweza kuaminiwa.
Mapema mwezi huu huduma za mtandao zilikatishwa kwa siku mbili Mashariki mwa jimbo la Kessala baada ya mapigano ya kikabila kusababisha vifo vya watu karibu 10.
Japo hatua hiyo huenda ilikuwa jaribio la kuzuia watu kutumia mitandao ya kijamii kuzua hali ya taharuki, sasa kuna hofu serikali huenda inapanga njama ya kuminya uhuru wa habari kama ulivyokuwa ukifanya utawala ulioondolewa madarakani.
Vikosi vya usalama bado vina uwezo mkubwa katika utawala wa sasa - na umeonesha hatua kidogo sana katika hali ya kuzingatia haki za binadamu na demokrasia.
'Wafanyakazi wahamiaji walitoroka vituo vya karantini'
Baada ya amri ya kutotoka nje ya kitaifa kuanza kutekelezwa April mosi, polisi walidaiwa kuwapiga na kuwakamata madaktari - akiwemo mkuu wa hospitali kuu ya wazazi Sudan - walipokuwa wakielekea kazini.
Hii ilifanyika licha ya madaktari hao kuwa na vibali vya usafiri. Bw. Tom hatimaye alilazimika kuingilia kati na kuamuru waachiliwe huru.
Coronavirus Afrika:
Baadhi ya watu wanaamini virusi vya corona vililetwa Sudan na mamia ya wahamiaji wa nchi hiyo kutoka Misri na Muungano wa Milki za Kiarabu mwezi Machi kwasababu mlipuko wa virusi ulianza katika mataifa hayo.
Serikali iliwaweka katika vituo vya karantini, lakini waliondoka kabla ya muda wao wa kukaa hapo kukamilika, wakilalamikia hali mbaya ya maisha katika vituo hivyo.
Wengine ni wanafunzi waliokuwa wakirejea nyumbani kutoka mji wa Wuhan, China - ambao waligoma kuondoka uwanja wa ndege kupinga hatua ya serikali ya kutaka kuwapeleka katika vituo vya karantini.
Baada ya mvutano wa muda mrefu wa wanafunzi hao katika uwanja wa ndege hatimaye serikali iliwaruhusu waende nyumbani.
Wengi wanachukulia hatua hiyo kama ishara ya utepetevu wa serikali- ya muungano inayojumuisha majenerali wa kijeshi na raia walioungana kumuondoa Bashir kupitia maandamano ya Umma.
Watu wengi, hasa wazee, wamekuwa wakifariki kutokana na magonjwa tofauti katika mji mkuu wa Khartoum, kwasababu huduma katika vituo vya afya - zikiwemo hospitali - zimesitishwa tangu mlipuko wa virusi vya corona uliporipotiwa mwezi Machi .
Baadhi ya madaktari walikataa kufanya kazi, wakilalamikia ukosefu wa vifaa kinga.
Mfumko wa bei wafikia asilimia 100
Wizara ya Afya wiki mbili zilizopita ilitangaza kuwa vituo 30 vya afya vimefunguliwa mjini Khartoum. Lakini, baadhi ya vitua havijafunguliwa
Serikali imetenga hospitali mbili Khartoum - ambazo zina uwezo wa kuwahudumia karibu watu milioni 10 - kuwashughulikia wagonjwa wa Covid-19 pekee.
Kando na janga la kiafya Sudan pia inakabiliwa na -janga la kiuchumi.
Kiwango cha mfumko wa bei kimefikia asilimia 100, hali ambayo imefanya maisha kuwa magumu kwa mamilioni ya watu.
Hali yao imezoroteshwa zaidi na hatua ya kuwekwa kwa amri ya kutotoka nje, kwani hawana namna yoyote ya kujipatia kipato cha siku.
Baadhi yao wanasikitika hakuna kiongozi hata mmoja aliyejitokeza hadharani kuwatia moyo ama hata kuwapati amsaada wa chakula.
Wanasema hali inayowakumba inatokana na uongozo mbaya - jambo ambalo hawakutarajia hasa baada ya kufanikiwa kumng'oa madarakani Omar al-Bashir Aprili 2019.