Virusi vya corona: Je kuna hatari gani ya maambukizi unapoogelea baharini na katika mabwawa?

Iliyochapishwa

Huku msimu wa baridi ukiingia maeneo mengi katika jumuiya ya Afrika Mashariki yanaendelea kuwa na hali nzuri licha ya watu wachache kuzuru mabwawa ya kuogelea na baharini huku wengi wakiwa na hofu iwapo virusi hivyo vinaweza kusambazwa katika maji au la.

Kwa kuwa hakuna tafiti za moja kwa moja kuhusu uhai wa virusi hivyo katika maji, shirika la Afya duniani WHO limepata mapendekezo yake kupitia ushahidi mwingine wa tafiti za kisayansi kuhusu virusi vya corona.

Shirika hilo linakumbuka kwamba virusi aina ya Influenza vinatarajiwa kufa dakika tano tu baada ya kukutana na maji ya kunywa yenye klorini ya miligramu 0.3 kwa lita.

Japokuwa uwezekano wa virusi vya corona katika maji yasiyo na klorini upo juu, havijapatikana katika maji ya kunywa , Shirika la Pan American Health PAHO limesema.

Lakini je virusi hivyo vinaweza kusababisha maambukizi katika maji ya baharini na mabwawa ya kuogelea?

Baraza kuu la utafiti wa kisayansi nchini Uhispania CSIC lilitoa ripoti wiki iliopita likichanganua kuhusu uwezekano wa maambukizi.

Mabwawa ya kuogelea

Dawa ya klorini inayotumika kuua vidudu katika mabwawa ya kuogelea husababisha mauaji ya virusi vya corona.

Matumizi yake yamelazimishwa katika mataifa mengi na mashirika ya afya kwa miaka mingi.

Kutaka majibu tofauti kuhusu suala hilo kulingana na Joan Grimalt , mtafiti katika taaisi ya mazingira na utafiti wa maji nchini Uhispania aliyekuwa akizungumza na BBC .

Maambukizi katika maji sio rahisi kufanyika , na sio rahisi zaidi kufanyika katika maji ya chumvi ama maji ya mabwawa ya kuogelea, anaongezea.

Asilimia ya Klorini ambayo kidimbwi cha kuogelea kinafaa kuwa nayo ni miligramu 0.5 kwa lita.

Japokuwa mabwawa ya kuogelea yana kati ya miligramu 1 na mbili kwa lita , kiwango ambacho kulingana na mamlaka ya sekta hiyo ni salama kwa afya.

Kituo cha kudhibiti magonjwa duniani (CDC) kinakubaliana kwamba utunzi mzuri wa mabwawa ya kuogelea, mirija ya moto , spas, ama maeneo ya kuchezea huvunja makali ya virusi.

Hatahivyo baraza kuu la utafiti wa kisayansi Uhispania linapendekeza uoshaji wa mikono na uso kwa kutumia sabuni kabla ya kuiingia katika kidimbwi cha kuogelea, na kusisitiza kwamba ni watu wengi katika mabwawa ya kuogelea au bahari ambao wanaweza kuwaweka wenzao hatarini.

Baharini

"Maji ya bahari yana chumvi na ni kipengee hiki ambacho kimethibitishwa katika utafiti kinaweza kuua virusi vya corona.

Lakini hilo ni suala la kawaida, anasisitiza. Hutokea na virusi vingi.

Virusi hivyo husambaa ndani ya maji na chumvi hiyo hupunguza uwezo wake wa kuambukiza

Mchanga wa baharini

Kuna sababu tatu ambazo hufanya maambukizi ya virusi vya corona katika mchanga kutofanikiwa: jua, chumvi iliopo katika michanga hiyo na sakafu ya mchanga. Miale ya jua huua virusi hivyo katika mchanga.

Pia lazima itiliwe maanani kwamba mchanga huo una chumvi nyingi ya baharini.

Cha mno ni kwamba mchanga hauna sakafu laini. ''Kile kilichogundulika ni kwamba virusi hivyo haviwezi kuishi katika sakafu isiyo laini'', alisema Grimalt.

Maji ya mto , ziwa ama mitiririko

Iwapo tunataka kwenda kuoga katika mito, ziwani na maji yasiyotembea matumizi yake yanahitaji ushauri.

Katika mazingira kama hayo tahadhari inapaswa kuchukuliwa.

Mazingira hayo ya maji hayafai kutumika katika kujiburudisha ikilinganishwa na maji mengine mbadala.

Utafiti uliofanywa katika virusi vingine vya corona unasema kwamba , virusi huwa na uwezo wa kufanya maambukzi katika maji safi , kulingana na ripoti hiyo ya CSIC.

Lakini ukweli ni kwamba , virusi hivyo haviwezi kusababisha maambukizi ndani ya maji lakini iwapo unataka kuhakikisha kuwa uko salama ni vyema kuogelea katika maeneo ambayo una uhakika hayana maambukizi na hayo ni maeneo kama vile baharini na mabwawa ya kuogelea, anasema Grimalt.