Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vifo vya corona: Kwanini Uingereza imerekodi vifo vingi vya corona Ulaya?
Uingereza kwa sasa ina idadi kubwa ya vifo vya walioathirika na virusi vya corona barani Ulaya, hiyo ni kulingana na takwimu rasmi za serikali.
Siku ya Jumatano, vifo zaidi 649 vya kutokana na corona vilirekodiwa na kufikisha jumla ya vifo vilivyotokea Uingereza kuwa 30,076.
Mpaka Jumanne ya wiki hii Italia ndiyo taifa ambalo lilikuwa na idadi kubwa ya vifo barani Ulaya. Mpaka sasa taifa hilo limesharekodi vifo 29,684 kwa jumla.
Wakati huo huo zaidi ya watu 72,000 wameaga dunia nchini Marekani.
Lakini idadi hiyo inaonesha tu simulizi kidogo ya kile kinachotokea, wataalamu wa afya wamesema.
Tunaweza kuwa na uhakika kwamba idadi vifo iliyorekodiwa huenda ni ya chini ikilinganishwa na idadi kamili ya walioathirika na virusi vya corona, amesema Profesa Sir David Spiegelhalter, kutoka chuo kikuu cha Cambridge, Uingereza.
"Tunaweza kusema kwamba hakuna kati ya nchi hizi inayoendelea vizuri lakini hili sio janga la Ulaya tu kwa hiyo haitakuwa jambo lenye tija kama tutaizungumzia hiyo tu," amesema.
Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:
Ulinganisho wa jinsi mataifa mbalimbali yanavyo kabiliana na virusi vya corona
Kuna changamoto kote duniani ukilinganisha kiwango cha vifo kutoka mataifa mbalimbali.
Katibu wa masuala ya jamii Robert Jenrick amesema katika mkutano na wanabari: "Ni vigumu kufanya ulinganisho wa kimataifa kwa uhakika.
"Tunataka kujifunza mambo kadhaa kadiri tunavyoweza hasa ukizingatia kwamba kwamba dunia nzima inakabiliana na janga hili."
"Mataifa mengine yanapima hatua zilizochukuliwa kwa namna mbalimbali. Na inafanya ulinganisho wa kimataifa kuwa vigumu," ameongeza Profesa Yvonne Doyle, mkurugenzi wa kimatibabu katika wizara ya afya Uingereza.
Idadi ya watu Uingereza ni karibia milioni 66 huku Italia ikiwa karibia milioni 60.
Uingereza itahitajika kusajili angalau asilimia 10 zaidi ya vifo ikilinganishwa na Italia.
Namna tofauti ya nchi mbalimbali zinazohesabu idadi ya vifo pia kunahitajika kutiliwa maanani.
"Kila nchi inahesabu idadi ya vifo kwa namna tofauti," amesema mshauri mkuu wa tiba katika serikali ya Uingereza Chris Whitty, "Kulinganisha nchi moja na nyengine haisaidii".
Kwa mtazamo wa juu juu, Italia na Uingereza kwa sasa hivi ni kama ziko sawa - zinajumuisha waliopimwa na waliothibitishwa kupata maambukizi kila siku.
Lakini pia tunaweza kuchukulia kwamba idadi ya vifo inayorekodiwa hospitali ni sahihi, idadi ya vifo katika vituo vya kutunza wazee au majumbani haziwezi kuchukuliwa kuwa sahihi kwa asilimia mia moja.
Idadi ya watu inamchango wake katika ulinganisho huu.
Kwa mfano, tunajua kwamba athari za virusi vya corona inajitokeza zaidi kwa watu wazee ikilinganishwa na vijana.
Kuna uwezekano mkubwa wazee wakawa na matatizo mengine ya kiafya ambayo yanafanya iwapo watapata virusi vya corona basi watakuwa katika hatari zaidi.
Italia ina idadi kubwa ya watu wazee huku idadi ndogo kabisa ikiwa ya watoto (ambao hatari ya wao kuathirika vibaya na janga la corona iko chini) kwahiyo, ikiwa mambo mengine yote yangekuwa sawa, ungetarajiwa kutokea kwa idadi kubwa ya vifo nchini Italua kuliko Uingereza.
Je kifo kutokana na virusi vya corona ni nini?
Nchini Uingereza, idadi ya kila siku inayotolewa inategemea wale waliothibitishwa kuambukizwa, ingawa ofisi ya tarkwimu za taifa pia inachapisha takwimu yoyote yenye ambapo ugonjwa wa Covid -19 unahisishwa na vifo, bila kuzingatia kwamba alipimwa au la.
Ubelgiji imekosolewa kama nchi iliyoathirika vibaya na virusi vya corona linapokuja suala la walioakufa.
Maafisa wa Ubelgiji wanasema hali yao katika kukabiliana na janga la corona haikuwa vizuri ikilinganishwa wengine: idadi ya vifo hospitalini na kwenye makaazi ya kutunza wazee vinavyoshukiwa kwamba bado havijathibitishwa kama ugonjwa wa Covid-19.
"Watu wamekuwa wakifanya ulinganisho usio sahihi", amesema Profesa Steven Van Gucht, daktari wa magonjwa ya yanayosababishwa na virusi kutoka Ubelgiji ambaye pia ni msemaji wa serikali.
Ni vigumu sana kupata takwimu za uhakika kutoka nchi zenye kudhibiti mfumo wake wa kisiasa.
Kupata idadi ya waliokufa kwa milioni moja ya idadi ya watu, tutasema idadi ya China ni ya chini mno, hata baada ya kuongezeka kwa asilimia 50 ya vifo katika mji wa Wuhan.
Wataalamu wa afya wanapendekeza kwamba kuwa makini na idadi ya wanaokufa ambayo ni ya juu ikilinganishwa na wakati kama huo miaka iliyopita.
Lakini kupata takwimu kama hizi inachukua muda na huenda ikawa miezi kama sio miaka - kabla ya kujua athari kamili za janga la corona ulimwenguni.
Kipi kilichoenda mrama Uingereza?
Nchi zilizofanikiwa kupima idadi kubwa mapema kuchukua hatua ya kufuatilia wengine walioawasiliana na mwathirika inaonekana ndizo zilizofanikiwa kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.
Lakini Ujerumani na Korea Kusini zimekuwa na kiwnago cha chini cha vifo ikilinganishwa na nchi zilizoathirika zaidi.
Idadi ya wanaopimwa kwa siku ikilinganishwa na idadi yote ya watu huenda ikawa tarakimu muhimu kutabiri kiwango cha chini cha vifo.
Lakini sio kwamba takwimu zote za wanaopimwa zinafanana - baadhi ya nchi zinarekodi idadi ya watu wanaopimwa, huku zengine zikirekodi idadi jumla ya wote waliopimwa.
Muda muafaka wa kupima, na ikiwa walipimwa hospitali au katika jamii zao pia kunahitaji kurekodiwa.
Ujerumani na Korea Kusini zilipima idadi kubwa ya watu mapema na kujifunza mengi kuhusu vile virusi hivyo vinavyosambaa.
Lakini Italia ambayo pia imepima idadi kubwa ya watu, pia nayo imerekodi kiwango kikubwa cha waliokufa.
Italia iongeza uwezo wake wa kupima watu baada ya kuwa janga hilo limewaathiri kwa kiasi kikubwa. Uingereza nayo inafanya vivyo hivyo.
Mbunge wa chama cha upinzani Dkt. Rosena Allin-Khan, ambaye amekosoa mkakati wa serikali wa kupima watu akisema umesababisha vifo vingi.