Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Wabunge wa Chadema wajiweka karantini kuepuka kusambaa kwa virusi.
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema, kimewataka wafuasi wake bungeni kuacha kuhudhuria vikao vya bunge na kukaa mbali na majengo ya bunge ya Dodoma na Dar es salaam ili kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.
Hatua hii ya upinzani inakuja wakati bunge hilo liliomboleza vifo vya wabunge watatu waliokufa katika kipindi cha chini ya wiki mbili.
Chadema kimewataka wabunge wasitisha vikao vya bunge na kujiweka karantini kwa walau wiki mbili.
Miongoni mwa waunge watatu waliofariki Dkt. Augustine Mahiga, ambaye kifo chake cha ghafla kimetokea leo alfajiri.
Hadi kifo chake kinatokea Bwana Mahiga alikua waziri wa katiba na na masuala ya sheria wa Tanzania na awali alishikilia nyadhfa za kidiplomasia katika Umoja wa Mataifa na Somalia ambapo alikuwa mmoja wa wanadiplomasia walioheshimika barani Afrika.
Ingawa maafisa hawajahusisha vifo vya wabunge waliokufa na virusi vya corona, serikali imekua ikikosolewa kwa kupuuza janga la corona na kwa kutoweka hatua kali za kukabiliana na maambukizi ya Covid-19.
Chadema kimekua kikisisitiza serikali iache kupuuza virusi vya corona na kuchukua hatua kama zilizochukuliwa na nchi nyingine duniani zikiwemo za Afrika kudhibiti maambukizi badala ya kutumia nyungu kujifukiza.
Kiongozi wa Upinzani na mbunge wa Chadema Freeman Mboe amekua akiishauri serikali kuchukua hatua mbali mbali kukabiliana na virusi vya covid-19:
Idadi rasmi ya watu walioambukizwa virusi nchini Tanzania imeripotiwa kufikia watu 480.
Je Chadema wanataka nini hasa?
- Wabunge wote wa Chadema waache Mara moja kuhuduria vikao vya Bunge au kamati za Bunge.
- Wabunge wote wajiweke karantini kwa muda usiopungua wiki mbili
- Wanasisitiza wabunge wao wote walioko Dodoma wasiende majimboni/mikoani bali wabaki Dodoma kwenye katarantini hadi itakapothibitika wani salama na au kupata maelekezo mengine yoyote yaliyo rasmi. Aidha wanawasihi wabunge wengine wote wa vyama vingine kutafakari kama kweli ni salama kuendelea nba Vikao vya Bunge katika mazingira yaliyopo.
- Pia imelitaka Bunge kusitisha shughuli Bunge kwa sikiu 21 kuruhusu Wabunge na watumishi wote wa Bunge kwenda karantini.
- Kupima Wabunge wote, Watumishi wa Bunge na familia zao kubaini ni wangapi tayari wana maambukizi ya virusiili hatua stahiki za kitabibu ziweze kuchukuliwa.
- Kamati mahsusi za Bunge husususani za Huduma za Bunge na kamati ya Uongozi zifanye vikao vyake kwa njia ya mtandao(zoom) ili maamuzi muhimu kuhusu Utawala na mwenendo wa Bunge yaweze kufanyika.
- Chadema inaendela kusisitiza kwa Watanzania wote kuwa mstari wa mbele kila mmoja wao kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
- Inasisitiza kuwa ni uzembe kusubiri kufanyiwa kinga na mwenzi. Anza kwako.