Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Karibia vifo 60,000 vyarekodiwa Marekani pekee
Marekani imethibitisha watu walioambukizwa virusi vya corona kufikia zaidi ya milioni moja, idadi hiyo ikiwa ni sawa na karibu theluthi moja ya idadi yote duniani.
Hadi kufikiwa sasa, watu 3,098,391 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona kote duniani huku idadi ya vifo ikiwa ni 216,160, kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Wakati hilo linatokea, makamu rais wa nchi hiyo Mike Pence ameonekana akitembelea kliniki ya Mayo huko Minnesota bila kuvaa barakoa licha ya kwamba kuna kanuni ya kila mmoja kuvaa barakoa.
Katika ujumbe uliofutwa katika mtandao wa Twitter, kliniki hiyo imesema kwamba makamu rais alifahamishwa mapema kuhusu sera yake inayolazimisha kila mmoja kuvaa barakoa.
Bwana Pence anaongoza jopokazi linashughulikia janga la corona katika Ikulu ya rais.
Wakati huohuo, Rais Donald Trump ameagiza viwanda vya kutengenza nyama viendelee na shughuli zao ili kulinda upatikanaji wa chakula wakati janga la virusi vya corona linaendelea.
Rais alizungumzia sheria ya wakati wa Vita vya Korea kuanzia miaka ya 1950 ilipoagiza kwamba mitambo iendelee kutoa huduma.
Inakadiriwa kwamba wafanyakazi 3,300 wa viwanda vya kutengeneza nyama Marekani wamebaini ka kuambukizwa virusi vya corona na 20 wamekufa.
Umoja wa Mataifa mwezi jana ulionya kwamba kuhusu tishio la ukosefu wa chakula kote duniani.
Viwanda vya nyama 22 nchini Marekani vimefungwa katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona.
Takriban watu 70 wamekufa kwa virusi hivyo katika makazi ya wazee huko Massachusetts.
wakaazi wengine 82 na wafanyakazi 81 wamepatikana na virusi hivyo kulingana na chama cha vyombo vya habari.
Aidha bunge la wawakili Marekani halitarejelelea vikao vyake wiki ijayo baada ya baadhi ya wabunge kupaza sauti kwamba ni mapema mno kufanya hivyo.
Jumatatu wabunge walikuwa wameomba kurejelelea vikao vyao lakini kiongozi wa walio wengi wa Steny Hoyer kutoka chama cha Democratic, Jumanne alisema mpango huo umefutiliwa mbali baada ya mashauriano.
"Tumekubaliana kwamba hatutarejea wiki ijayo lakini tutarudi hivi karibuni," Bwana Hoyer alisema.
Hata hivyo wabunge wa Republican waliowengi katika bunge la Senati bado wanaendelea na mpango wao wa kurejelela vikao vyao Mei 4.
Washington DC bado inatekeleza kanuni ya kusalia mndani hadi mei 15. maafisa wanasema kiwango cha maambukizi bado kiko juu.
Eneo la Washington DC ambalo linajumuisha vinga vya Maryland na Virginia limerekodi watu zaidi ya 38,000 huku wengine zaidi ya 1,600 wakiaga dunia.
Raia wa Marekani wanaokufa kwa virusi imepita wale waliokufa katika Vita ya Vietnam
Huku zaidi ya vifo 59,000 kwa sababu ya Covid-19 vikirekodiwa kwa Marekani pekee idadi hiyo imepita wale waliokufa katika Vita ya Vietnam.
Watu wengi zaidi kwasasa wamepoteza maisha yao katika kipindi cha miezi michache ikilinganishwa na raia 58,220 wa Marekani waliokufa karibu miongo miwili iliyopita huko Vietnam - na kuangazia athari ya Covid-19 kwa nchi hiyo.
Mmoja wa washauri kutoka Ikulu ya White House, Dkt Anthony Fauci, ameonya kwamba mlipuko uko mbali na kufikia ukomo wake. Alisema kwamba nchi hiyo huenda ikashuhudiwa kipindi kibaya cha msimu wa ukutizi ikiwa watafiti watashindwa kupata tiba muafaka.
Dkt Fauci alisema ni jambo lisiloweza kuepukika kwamba virusi hivyo vitarejea - na huenda vikaendelea kuwepo hadi msimu huu.
Trump anasema Marekani itaanza kupima watu milioni 5 kwa siku.
Mbili ya sababu Marekani ina idadi kubwa ya wanaoambukizwa virusi namna hiyo ni idadi ya juu ya watu (karibia milioni 330), ikiendana na idadi kubwa ya wanaopimwa.
Marekani imepima watu takribani milioni 5.7 miezi miwili iliyopita kulingana na Shirika la ifuatiliaji wa ugonjwa wa Covid.
Idai hiyo inaonekana kuwa juu lakini kulingana na takwimu ya Shirika la Kisayansi linalochapisha taarifa za Dunia mtandao, Marekani ilikuwa imepima watu 16.3 kwa kila 1,000 idadi hiyo ikiwa ni ya chini ikilinganishwa na Italia iliyopima watu 30.6 kwa kila 1,000.
Rasi Trump amependekeza kwamba hivi karibuni Marekani itafanya vipimo hadi milioni 5 kwa siku, akiongeza kwamba"hivi karibuni tutafika".
Hata hivyo kauli yake inaonekana kuwa na matarajio makubwa kwasababu ripoti zasema hadi kufikia sasa marekani inapima karibia watu 200,000 kwa siku.