Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona Afrika: 'Hakuna muda wa kunasua uchumi wa Afrika' dhidi ya corona
Virusi vya corona "havitasababisha maelfu ya vifo pekee" barani Afrika, bali pia huenda vikaathiri pakubwa "uchumi na ustawi wa kijamii", kwa mujibu wa kiongozi mkuu wa Afrika katika Shirika la Afya Duniani, Matshido Moeti.
Kauli yake inatukumbusha kuwa mlipuko wa ugonjwa huu si dharura ya kiafya pekee.
Mwaka mmoja uliopita, ripoti ya Afrika kutoka Benki ya Dunia, iliyoangalizia ukuaji wa uchumi wa mataifa ya jangwa la sahara kwa mwaka 2019 na 2020 kwa kiasi cha 2.8%.
Kushuka huko kwa uchumi, kumeshusha malengo ya taarifa nyingi ambazo zilitegemewa kuongeza uchumi, na sasa bara hili litaanguka kiuchumi kwa kiwango ambacho haijakipitia kwa miaka 25, kwa uchumi kushuka kwa kiwango cha kati ya 2.1% na 5.1%, kutokana na athari zinazotokana na kusambaa kwa mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19.
Benki ya dunia inasema athari zinazotokana na ugonjwa wa Covid-19 katika bara hilo zimegawanyika katika sehemu tatu:
- Biashara zimeathirika na kushindwa kusafirishwa kwa bidhaa
- Fedha za ufadhili kupungua na hata fedha kutoka nchi za kigeni kupungua
- Matatizo ya kila siku katika uchumi yanayosababishwa na makatazo mbalimbali na watu kufungiwa
Bei za bidhaa zimeathiri uchumi
Bei ya mafuta , ingawa imekuwa nafuu kidogo lakini gharama yake iko mbali na kile ambacho serikali ya Nigeria inakihitaji ili kuweza kupanga bajeti yao vizuri au kuifanya Angola kukabiliana na anguko la uchumi ambalo nchi hiyo inakumbana nayo kwa sasa.
Mwaka mmoja uliopita bei ya madini ya shaba ilikuwa chini ya dola tatu, lakini sasa imeshuka mpaka $2.20.
Bei ya shaba imeshuka karibu karne sasa, lakini mwezi sasa tangu mlipuko wa virusi vya corona ulivyoweza kuathiri zaidi soko hilo la shaba. Na hali mbaya zaidi kwa wasafirishaji wa bidhaa hiyo Zambia.
Mpaka hivi karibuni sekta ya madini nchini Afrika Kusini na Zimbabwe, haikuweza kuendelea kufanya shughuli zake.
Lakini duniani kote kuna hofu bei ya madini kushuka, ni muda tu haujafika.
Mwaka 2018, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa na taasisi za maendeleo za kimataifa, Unctad, FDI kuwa bara hilo lilikuwa na maendeleo mazuri.
Lakini sasa Unctad inasema kuwa corona imesababisha uwekezaji kushuka kwa 15%.
Wanaotegemea jamaa zao ughaibuni wajipata mashakani
Mwaka 2019, ulikuwa mwaka wenye mafanikio makubwa katika utumaji wa fedha.
Benki ya dunia imeweka makadirio ya watu waliopo ughaibuni kutuma dola bilioni 49 kwenda nyumbani kwao, kiasi ambacho ni dola mbili zaidi ya mwaka 2018.
Ilidhaniwa kuwa mwaka 2020 ungekuwa na mafanikio makubwa zaidi.
Lakini hali hiyo haitawezekana ikiwa bara la Ulaya, Marekani na China kuwa imefungwa , watu wamepoteza ajira na malipo kufanyika imekuwa ngumu.
Hatua hizo za kuzuia maambukizi ya corona zinaonekana kuwa ngumu kufuatwa, lakini zimeonekana kutumika katika maeneo mbalimbali duniani na mafanikio kuonekana kidogo.
Ingawa hatua hizo zinakuja na angalizo.
Idadi kubwa ya watu wanakabiliwa na wakati hadi wanaonelea ni bora kufa na ugonjwa wa corona kuliko kufa kwa njaa, labda kama serikali inaweza kuingilia kati kwa kuweka jitihada ambazo zina ahueni kwao.
Katika nchi kama vile Gambia, Zimbabwe na Liberia, robo ya pato jumla la kitaifa inatokana na kodi ya fedha au bidhaa zinazotumwa na raia wao wanaoishi nje ya nchi ya nchi.
Bajeti za watu binafsi zitaathirika ikiwa huduma hiyo itasitishwa
Inakadiriwa watalii karibu milioni 67 walizuru mataifa ya Afrika mwaka 2018, na fedha walizotumia zilisaidia kubuni nafasi za kazi karibu milioni 20, na kuchangia karibu 8% ya pato jumla la uchumi wa bara hilo.
Ugonjwa wa Covid-19 imelemaza kabisa usafiri wa angani hali iliyofanya mahoteli yakisaliabila wageni huku maeneo ambayo ni vivutio vya watalii yakifungwa.
Mlipuko wa virusi vya corona umekumba bara Afrika wakati ambao idadi ya watalii hususan kutoka China ilikuwa imeongezeka.
Wataalamu wa masuala ya kiuchumi wanahofia sekta hiyo itaathiriwa vibaya kutokana na janga la corona.
Ripoti ya Muungano wa Afrika inasema bara hilo huenda ikapoteza karibu dola bilioni 50 katika sekta ya utalii pamoja na nafasi za ajira milioni mbili .
Athari ya marufuku ya kutotoka nje
Lakini athari za kiuchumi zimeanza kuwapata watu wengi baranini Afrika hususana kutokana na amri ya kutotolka nje iliyowekwa na mataifa yao.
Moja ya athari ambayo virusi hivi vitasababisha ni ongezeko la madeni katika malipo ya huduma mbalimbali.
Kushuka kwa bei za bidhaa, fedha kushuka thamani na changamoto ya serikali za Afrika kutumia fedha nyingi zaidi ya bajeti yao kutasababisha madeni kuongezeka zaidi na zaidi na athari kuwa kubwa zaidi ya matokeo ya sekta ya huduma ya afya.
Jibu rahisi ni kwa watoa mikopo kuweka unafuu katika mikopo.
Wiki hii kumekuwa na haueni ya moja ya nne.
IMF imetangaza kutoa nafuu ya mikopo kwa nchi 25 zikiwemo 19 za Afrika.
Malipo ya riba kulipwa kwa kipindi cha miezi sita kumeweza kuleta majibu chanya hivi karibuni kwa nchi kama ya Ethiopia lakini hiyo ni sehemu ndogo tu ya tatizo.
Haijaelezwa bado kuhusu mikopo ya muda mrefu ya ujenzi katika nchi maskini barani Afrika kama kutakuwa na unafuu wowote.
Pia unaweza kusoma:
Suala la madeni ni changamoto kubwa
Karibu robo ya karne iliyopita, wakati ambao IMF na World Bank zilipoanzishwa, kulikuwa na mzigo mzito wa madeni kwa mataifa maskini ya Afrika, mataifa ya Afrika yalikuwa yanadaiwa fedha na nchi tajiri na taasisi za fedha.
Lakini siku hizi , viongozi wa sekta binafsi wamechukua jukumu kubwa kuleta maendeleo katika mataifa mbalimbali ya barani Afrika kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Kwa sasa ni je, viongozi wa sekta binafsi au msaada wa ulaya wako tayari kukabiliana na janga hilo.
Ni suala gumu na mfumo wake ni mgumu lakini ngoja tuone hali itaendaje, alisema Masood Ahmed, rais wa kituo cha maendeleo ya dunia kilichopo Marekani(Global Development).
Mkopo mkubwa si suluhisho
Shirika la fedha la IMF na benki ya dunia wameweka kiasi cha dola bilioni 64 kwa ajili ya msaada wa kukabiliana na virusi vya corona.
Ethiopia imesema kuwa fedha hizo hazitoshi labda wangepata dola bilioni 150 kwa ajili ya bara la Afrika peke yake.
Wakati mataifa matajiri wana riba ndogo kuwawezesha kuendeleza programu zitakazowawezesha kukabiliana na athari za kiuchumi zilizotokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona., jambo ambalo halipo kwa mataifa mengi ya Afrika.
Benki kuu za Afrika zimekuwa zikipata punguzo la riba lakini watu wengi wana madeni lakini ni watu wachache wenye mikopo huku ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea, hivyo hakuna usawa katika hatua hiyo.
Afrika Kusini imesema itatenga dola milioni 66, kusaidia wakulima wadogo ili mazao yatakayozalishwa yaqweze kuwasaidia.
Nchini nyingine Afrika ni Nigeria, ambayo imetoa msaada wa kifedha kwa wahitaji lakini hakuna ushahidi wa kutosha katika hilo.
Lakini kama serikali zitajaribu kukopa fedha zaidi , madeni yataongezeka zaidi.Tim Jones, kutoka kampuni ya Jubilee Debt Campaign, alisema kuwa kukopa fedha zaidi sio jibu.
Mpaka sasa waafrika wanaonekana kujaribu kukabiliana na maambukizi yaliyotokea katika baadhi ya maeneo ya nchi za Ulaya na Marekani.
Ubunifu wa hali ya juu unahitajika
Mataifa mengi ya Afrika na changamoto za kiuchumi hata kabla ya hali hii.
Lakini athari za kiuchumi kutokana na virusi vya Corona tayari zimeanza kuonekana katika bara hili, watu wameanza kupoteza ajira zao na shughuli zimekuwa haziendelei kwa sasa ambazo zingeweza kusaidia mataifa ya Afrika kukabiliana na hali ya umaskini.
Baadhi ya wafuatiliaji wa mambo wameeleza kuwa maisha ya watu wengi yanaweza kufa katika kupambana na ugonjwa huo kuliko vifo ambavyo vinaweza kutokea kutokana na ugonjwa wenyewe wa Covid-19.
Sasa si wakati wa kupima hatua zinazochukuliwa kwa upande mmoja, tunapaswa kuachana na hali hiyo na watunga sera inabidi kufikiria nje ya boksi ili kuja na mbinu itakayosaidia kukabiliana na tatizo, alisema kiongozi wa shirika la fedha duniani, IMF idara ya mataifa ya Afrika.