Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Idadi ya vifo Kenya yafikia watu wanane
Idadi ya watu waliofariki kutokana na janga la virusi vya corona nchini Kenya imefikia wanane baada ya mtu mmoja zaidi kufariki nchini humo ndani ya saa 24 zilizopita.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari hii leo Jumapili, Waziri wa Afya wa Kenya Bw Mutahi Kagwe maesema kifo hicho kimetokea katika Kaunti ya Siaya, Magharibi mwa Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kazi ya kutambua watu ambao walikutana na marehemu kabla ya kufikwa na umauti inaendelea.
Wakati ho huo waziri Kagwe ameeleza kuwa wagonjwa wapya sita wamethibitishwa nchini humo baada ya watu 766 kufanyiwa vipimo ndani ya saa 24 zilizopita.
"Kati ya wagonjwa hao, wanaume ni watano na mwanamke ni mmoja. Raia wa Kenya ni watano na mmoja ni raia wa kigeni," imeeleza taarifa hiyo na kuongeza: "Wawiwili kati yao hivi karibuni walisafiri kutoka Mashariki ya Kati, mmoja ametokea Mombasa na watatu hawana historia ya kusafiri katika siku za hivi karibuni. Umri wao ni baina ya miaka 25 mpaka 59."
Watano kati ya wagonjwa hao walikuwa kwenye vituo vya karantini ya lazima vilivyowekwa na serikali na mmoja alipatikana kwenye msako wa timu ya uangalizi.
Wagonjwa hao wamepatikana katika Kaunti za Nairobi, Mombasa na Siaya.
Habari njema ni kuwa mtu mmoja amepona virusi hivyo na kufanya idadi ya waliopota Kenya kufikia 25.
Awali hapo jana Jumamosi kulikuwa na wagonjwa waili tu ambao walipatikana Kenya , huku wagonjwa 11 wakitarajiwa kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupona virusi hivyo nchini Rwanda.
Kiwango kilichotangazwa Jumamosi ni cha chini cha maambukizi kutangazwa na Wizara ya afya nchini Kenya tangu kutangazwa kwa mara ya kwanza kwa maambukizi ya virusi hivyo tarehe 13 Machi ambapo mtu mmoja alitangazwa.
Katika tangazo lililotolewa na Katibu mkuu wa wizara ya Afya Mercy Mwangangi Jumamosi wagonjwa wapya ni Mkenya mmoja na mwingine ni raia wa kigeni.
Ijumaa Kenya ilitangaza kuwa watu 10 waliokuwa wakipata matibabu ya virusi hivyo katika vituo vya kujitenga na hospitali ya Mbagathi wamepona na wataruhusiwa kwenda nyumbani, alisema Waziri wa afya Mutahi Kagwe.
Hatua zilizotangazwa na serikali ya Kenya kudhibiti coronavirus
- Kenya ilitangaza marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa moja jioni hadi alfajiri saa kumi na moja
- Marufuku ya kuingia na kutoka katika kauti nne, kaunti ya Nairobi, Kilifi na Kwale
- Raia wa Kenya wameagizwa kuvaa barakoa kila mara wawapo katika maeneo ya umma
- Wageni wote wanaongia nchini kutoka mataifa yaliyoathiriwa watalazimika kujitenga binaffsi kwa gharama zao.
- Wakenya katika mataifa ya kigeni wametakiwa kufuata muongozo wa nchi husika
- Atakayekiuka maagizo ya karantini atakamatwa kama iafisa wa ngazi ya juu wa serikali aliyetiwa mbaroni pwani ya Kenyazitasaidia serikali yake kukabili janga la corona ikiwa ni pamoja na amri ya kutotoka nje kuanzia Ijumaa Machi 27 kuanziasa moja usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.
- Kufungwa kwa baa zote na wenye hoteli kuruhusiwa tu kuuza chakula cha kwenda kula nyumbani.
- Ibada za Kanisa na Swala za pamoja Misikitini zimesitishwa huku mazishi ya kiruhusiwa kuhudhuriwa na familia ya marehemu pekee.
- Sherehe za harusi pia zimepigwa marufuku.
Rwanda yaruhusu waliopona
Huku Kenya ikitangaza kupungua kwa maambukizi siku ya Jumamosi nchini Rwanda walitangaza kuwa wagonjwa 11 waliopona Covid -19 wataruhusiwa kwenda nyumbani.
Akizungumza kupitia televisheni ya taifa hilo Waziri wa Afya Dkt. Daniel Ngamije amesema hii ni awamu ya tatu ya wagonjwa wanaoruhiwa kwenda nyumbani baada ya kupona virusi vya corona na sasa idadi ya watu waliopona virusi hivyo kwa ujumla imefikia 18.
Hii inamaanisha kuwa idadi ya watu wenye virusi vya corona Rwanda imebakia kuwa watu 100 kati ya wagonjwa 118 waliothibitishwa nchini humo hadi tarehe 11 Aprili.
Kwa mujibu wa wizara hiyo mtu hufanyiwa vipimo mara mbili, kipimo cha pili kikifanywa saa 72 baada ya kipimo cha kwanza na iwapo hatapatikana na virusi vya corona basi huwa anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Hatua zilizochukuliwa na Rwanda kudhibiti maambukizi ya corona.
- Tarehe 22 Machi Rwanda ilitangaza amri ya kukukaa nyumbani al maarufu GumaMurugo na baadae kurefusha zaidi marufuku hiyo kwa siku 21
- Rwanda ilitangaza kufunga mipaka yote ya nchi hiyo na watu kuamrishwa kusalia majumbani mwao katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
- Hatua zingine zilizochukuliwa ni pamoja na watumishi wote wa serikali na wa kibinafsi kufanyia kazi nyumbani na safari za kuenda mikoani kusitishwa kwa wiki mbili kukiwa na uwezekano wa muda huo kuongezwa.
- Vilabu vya pombe na, maduka yasio ya chakula pia yamefungwa huku usafiri wa bodabobda ukisitishwa.
- Shirikisho la Soka la Rwanda(FERWAFA), pia limetangaza kwamba michuano yote itafanyika bila kuhudhuriwa na mashabiki katika viwanja vya michezo, huku shirikisho la mpira wa mkono nchini humo likiahirisha michezo yake yote.
- Maeneo ya umma na maeneo yote ya utoaji wa huduma yameagizwa kuweka vitakasa mikono kwa ajili ya umma unaotembelea maeneo hayo.
- Raia wamehimizwa kukaa nyumbani na kuepuka matembezi yasiyo ya maaana na kunawa mikono mara kwa mara kwa muda wa sekunde 20.
- Hakuna abiria atakayeruhusiwa kusimama na kutoa wito kwa watu wa eneo na vikosi vya usalama kusaidia kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa.
- Hatua hiyo ilichukuliwa siku moja baada ya wizara ya afya ya Rwanda siku ya Jumamosi kutangaza kuwa watu wengine sita wameambukizwa virusi vya corona miongoni mwao mtoto mchanga wa miezi 10.