Virusi vya corona: Rais Yoweri Museveni awaonesha Waganda jinsi ya kufanya mazoezi ya nyumbani kudhibiti maambukizi

Rais Yoweri Museveni akifanya mazoezi nyumbani kwake

Chanzo cha picha, Yoweri K museveni /Twitter

Maelezo ya picha, Rais Yoweri Museveni akifanya mazoezi nyumbani kwake
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Uganda imepiga marufuku kufanya mazoezi ya mwili ya umma kama njia ya ziada ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Rais Yoweri Museveni amesema kuwa Waganda wanapaswa kufanyia mazoezi ya mwili majumbani mwao na akatuma video kwenye mitandao ya kijamii kuwaonyesha jinsi mazoezi hayo yanavyoweza kufanyika.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Katika video, rais ambaye alikua miguu peku alianza kupiga pushapu katika sebule yake kupasha misuli.

Halafu akapiga pushapu 21 moja baada ya nyingine, huku afisa wake wa habari akihesabu. Alifanya 30 jumla:

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Maagizo hayo yanakuja baada ya video na picha za watu wanaofanya mazoezi yaya kukimbia na makundi ya watu wengine wakifanya mazoezi ya viungo -aerobics katika mji mkuu Kapala kushirikishwa katika mitandao ya kijamii.

Hii si mara ya kwanza kwa rais Museveni kuonyesha uwezo wake wa kiafya.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 75- aliliambia taifa mwaka jana kuwa amepoteza kilo 30 za mwili wakekwasababu alikua ameanza kuangalia afya yake na kufanya mazoezi ya mwili.

Hanuari Bwana Museveni alitembea umbali wa kilomita 200 (maili 125) kupitia Luweero triangle, ambako alikua na ngome yake ya kijeshi wakati wa vita vilivyomuweka madarakani.

Rais Museveni pia amepiga marufuku matembezi yoyote ya pikipiki za teksi al maarufu "boda boda".

Virusi vya corona

Taarifa zaidi juu ya virusi vya corona:

Amri ya kukaa nyumbani inaendelea kutekelezwa kote nchini Uganda

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Amri ya kukaa nyumbani inaendelea kutekelezwa kote nchini Uganda

Pikipiki zilikua zimeruhusiwa kubeba mizigo, ingawa baadhi ya waendeshaji wake wamekua bado wanawabeba wasafiri .

Wizara ya Afya Jumatano ilitangazakuwa ilithibitisha kisa kimoja zaidi cha maambukizi ya virusi vya corona, na hivyo kulifanya taifa hilo kuwa na jumla ya visa 53 vya maambukizi.

Zaidi ya watu 3,500 wamekwisha fanyiwa vipimo hadi sasa, kwamujibu wa wizara hiyo.

Amri ya kukaa nyumbani kwa muda wa wiki mbili inaendelea kutekezwa nchini Uganda.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?