Coronavirus: 'Kilichonipata katika wodi ya karantini Kenya'

Moja ya wodi ya kuwatenga wagonjwa katika hospitali ya Mbagathi Nairobi
Maelezo ya picha, Moja ya wodi ya kuwatenga wagonjwa katika hospitali ya Mbagathi Nairobi
Iliyochapishwa

Nilifika katika kituo cha afya cha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta saa kumi na mbili unusu jioni saa za Afrika Mashariki.

Nikapanga foleni ili nifanyiwe vipimo vya kiwango cha joto mwilini. Ilikuwa karibu nyuzi joto 37.7 - ambacho ni kiwango cha juu zaidi ya ilivyotarajiwa.

Nilipokuwa nikisubiri kumuona daktari, niliingiwa na hofu huenda nimemuambukiza ugonjwa mtoto wa dada yangu wa miaka miwili na nusu , wazazi wangu na marafiki nchini mwanangu wa miaka Ethiopia.

Kadiri nilivyosubiri ndivyo nilivyozidi kubabaika.

Wafanyikazi wa ndege waliagizwa wasijongee karibu yangu. Wasafiri kutoka kwa ndege nyingine waliniangalia huku wakipita mbali.

Baada ya kuzuiliwa katika uwanja wa ndege kwa zaidi ya saa nne na nusu, ambulensi ilinichukua na kunipeleka katika hospitali ya Mbagathi - kituo ambacho serikali ya Kenya imefungua wodi ya kuwatenga watu wanaoshukiwa kuwa na visa vya coronavirus.

Katika vyumba hivyo, nilisikia watu wakikohoa.

Wat hospitalini

Nilipelekwa katika chumba kilichokuwa na watu wawili. Nilijifunika na kulala nikiwa nimevalia barakoa.

Tulifanyiwa vipimo siku ya Jumanne karibu saa tisa. Baada ya hapo tulianza safari ya kuogofya ya kusubiri matokeo.

Hali ilikuwa mbaya zaidi wakati Wizara ya Afya ya Kenya ilipothibitisha visa vitatu zaidi vya maambukizi. Tulijiuliza itakuaje ikiwa tulitangamana na watu waliothibitishwa kuwa na ugonjwa wa corona hospitalini.

majengo ya Hospitali

Siku ya Jumatano tulifahamishwa kuwa matokeo ya uchunguzi wetu yalionesha kuwa hatuna virusi.

Nilipata afueni. Niliwapigia simu jamaa zangu na kuwaambia wasiwe na hofu kila kitu kiko shwari. Walifurahi sana.

Moja kwa moja tulikusanya virago vyetu kutoka katika jengo hilo lakini tulizuiliwa kutoka. Ilinibidi nisubiri kujaza stakabadhi za kuthibitisha niko salama. Sikuwa na tatizo na hilo ila nilitaka kuwa nje ya jengo hilo hata kama nitasubiri hadi usiku kufikia maasharti yaliyowekwa.

Daktari amenishauri nijitenge binafsi kwa wiki mbili. Siwezi kutoka nyumbani wala kukutana na wageni.

Habari njema

Masharti mengine ya kuzuia maambukizi Kenya

  • Ndege za kimataifa zitasitishwa kuanzia Jumatano Machi 25 ispokuwa ile ya kubeba mizigo
  • Wageni wote wanaongia nchini kutoka mataifa yaliyoathiriwa watalazimika kujitenga binaffsi kwa gharama zao.
  • Wakenya katika mataifa ya kigeni wametakiwa kufuata muongozo wa nchi husika
  • Atakayekiuka maagizo ya karantini atakamatwa kama iafisa wa ngazi ya juu wa serikali aliyetiwa mbaroni pwani ya Kenya.
Hatua zilizochukuliwa na mataifa ya Africa kukabiliana na coronavirus