Coronavirus: Kenya yatangaza visa tisa zaidi vya ugonjwa wa corona

Wasafiri wanaowasili Kenya kutoka China

Chanzo cha picha, EPA

Iliyochapishwa

Visa vya hivi karibuni vinaifanya Kenya kuwa na jumla ya idadi ya watu 25 wenye maambukizi ya corona nchini Kenya.

Kati ya visa tisa, saba ni Wakenya huku wawili wakiwa ni wageni.

Waziri huyo amesema wagonjwa wametengwa na wanafuatiliwa kwa karibu. Bwana Kagwe amesema kuwa visa vilivyothibitishwa vya coronavirus vimepatikana katika mji wa Nairobi, na kaunti za Mombasa, Kilifi na Kwale

Amesema kuwa serikali itafanya vipimo vya lazima kwa wasafiri na wale watakaokua wametangamana na wagonjwa.

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe amesema kuwa juhudi za kuwatafuta watu 745 waliotangamana na visa vya hivi karibuni zinaendelea

''Inasikitisha kwamba baadhi ya Wakenya wanapuuza maagizo tuliyoweka kukabiliana na ugonjwa huu'' alisema awali Waziri Kagwe.

Akihutubia vyombo vya habari Juampili Bwana Kagwe alisisitiza umuhimu wa Wakenya kuzingatia hatua zilizowekwa ili kuepusha maafa.

''Huu ugonjwa sio mzaha'' aliongeza kusema. Kenya inasisitiza kuwa wiki mbili zijazo zitakuwa hatari zaidi endapo hali ya maambukizi haitadhibitiwa.

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Hatua za dharura zilizochukuliwa kuanzia usiku wa leo Jumapili, baa zote zitafungwa na wenye hoteli wataruhusiwa kuuza chakula cha kwenda kula nyumbani.

Ibada za Kanisa na Swala za pamoja Misikitini imesitishwa huku mazishi ikiruhusiwa kuhudhuriwa na familia ya marehemu pekee.

Sherehe za harusi pia zimepigwa marufuku.

Hyao ni masharti makali kuwekwa na mamlaka ya Kenya tangu ilipotangaza kisa cha kwanza cha coronavirus nchini March 13.

Masharti mengine ya kuzuia maambukizi Kenya

  • Ndege za kimataifa zitasitishwa kuanzia Jumatano Machi 25 ispokuwa ile ya kubeba mizigo
  • Wageni wote wanaongia nchini kutoka mataifa yaliyoathiriwa watalazimika kujitenga binaffsi kwa gharama zao.
  • Wakenya katika mataifa ya kigeni wametakiwa kufuata muongozo wa nchi husika
  • Atakayekiuka maagizo ya karantini atakamatwa kama iafisa wa ngazi ya juu wa serikali aliyetiwa mbaroni pwani ya Kenya.

Huku hayo yakijiri serikali imetangaza kuwa itamfikisha mahakamani naibu wa gavana wa jimbo la Kilifi pwani ya Kenya kwa kukaidi maagizo ya kujiweka karantini binafsi baada ya kuwasili nchini wiki iliyopita. Kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha serikali cha kuwatenga watu walio na ugonjwa wa corona.

maelezo zaidi
Hatua zilizochukuliwa na mataifa ya Africa kukabiliana na coronavirus