Coronavirus: Athari za kiuchumi za mashirika ya ndege Afrika

Iliyochapishwa

Mashirika ya ndege Afrika yamepoteza $ 40m tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona nchini China mnamo Februari, kulingana na Shirika la kimataifa la usafiri wa anga IATA.

Shirika la ndege kubwa barani Afrika Ethiopia Airlines limekataa kufuta safari za ndege kwenda China licha ya kuongezeka kwa shinikizo kutokana na kuzuka kwa coronavirus.

Kwa kulinganisha, Shirika la ndege la Afrika Kusini, South African Air ways, Royal Air Maroc, Air Tanzania, Air Mauritius, EgyptAir, RwandAir na Kenya Airways zote zimesimamisha safari za kwenda na kutoka China.

Lakini mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege Ethiopia Tewolde Gebremariam alisema Jumatano kwamba kuahirisha safari za ndege kwenda China si suluhisho la kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona. Shirika la habari la Xinhua limeripoti.

Aliongeza kuwa si haki kuitenga China kwasababu ya virusi.

"Kuruka moja kwa moja kwa China haimaanishi kuwa virusi vya corona , kwa sababu abiria kutoka China wanaweza kusafiri kwenda nchi za kiafrika kupitia njia nyingine nyingi.'' Alieleza mkuu huyo.

Bwana Tewolde alisema Shirika la Ethiopia limeathiriwa na virusi kama mashirika mengine, akionesha kupungua kwa 20% ya mahitaji.

Athari za kiuchumi

Makamu wa rais wa IATA, Rafael Kuuchi, aliiambia BBC kuwa upotevu wa mapato katika soko la usafiri wa anga kwa kiasi kikubwa kumetokana na kuahirisha safari za ndege kuelekea China.

Anasema madhara ya kiuchumi yanakuwa mabaya zaidi kwa mashirika ya ndege ya Afrika, ambapo mwaka jana yalipata hasara ya pauni milioni 78.

Mpaka sasa Misri, Tunisia, Morocco,Algeria, Nigeria na Senegal.

Shirika la afya duniani (WHO) limeonya kuwa nchi zilizo na mfumo mbaya wa afya huenda zikashindwa kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona hasa Afrika.

Visa vya maambukizi ya virusi vya corona vimeendelea kuenea duniani, ina maana kuwa mashirika ya ndege muda mfupi ujao yatawawia vigumu kujiendesha na kusababisha kuwapunguza kazi mamia ya wafanyakazi wake.