Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanasayansi waazimia kuwatambua wanyanyasaji kupitia mikono yao
Wanasayansi wanatumai kutafuta njia ya kuwatambua wananyasaji wa kingono kwa kutumia picha za mikono yao.
Mara nyingi nyuma ya mikono ndio huonekana tu katika picha za wanyanyasaji na picha zinazoshirikishwa kwenye mtandao.
Utafiti mpya unalenga kuvumbua ikiwa kweli kila mkono wa mtu ni wa kipekee kwa kutizama tofauti baina ya mkono wa kila mtu.
Watafiti wanatarajia kufanya hili kwa kuzifundisha kompyuta kutambua maumbile asilia katika picha zisizofahamika zilizotumwa na umma.
Hii itasaidia kutengeneza mtambo wa kompyuta ambao utawasaidia polisi kuwahusisha washukiwa na uhalifu kwa kutumia picha tu za mikono yao , wanasayansi wanatumai.
'Hatua ya mabadiliko katika sayansi'
Wanasayansi kutoka vyuo vikuu vya Lancaster na Dundee sasa wanawaita zaidi ya wanasayansi 5,000 kushiriki katika utafiti wao, ili kuwa na taarifa za kutosha kuthibitisha bila ikiwa mikono yetu ni ya kipekee.
Mchunguzi wa maumbile ya mwili Profesa Dame Sue Black alisema : "Mikono yetu inaonyesha tofauti mbali mbali za moja kwa moja kutokana na maendeleo yetu, geni, umri, mazingira tunamoishi na hata ajali.
"Tunafahamu kuwa vitu kama muundo wa mishipa, ngozi, na makovu huwa ni tofuti kati ya mikono yetu ya kushoto na kulia, na huwa hata tofauti baina ya mapacha wanaofanana.
"Tunaangalia namna tutakavyowasilisha hatua ya mabadiliko katika sayansi ili tuweze kuyatathmini, na kuelewa vitu vinavyofanya mikono yetu tofauti ."
App ya wavuti kwa kila mtu mwenye umri wa miaka 18 na zaidi wanatolewa wito kuchangia picha zao kwenye mradi huo wa utafiti kupitia simu za smartphon katika h-unique.lancaster.ac.uk
Picha hazishirikishwi na mashirika ya nje na zitaharibiwa mwisho wa mradi wa utafiti wa miaka mitano, uliodhaminiwa kwa pauni milioni 2.1 kutoka kwa baraza la Ulaya la utafiti
Dkt Bryan Williams, mhadhiri wa utambuzi wa alama za mwili na utambuzi wa binadamu katika chuo kikuu cha Lancaster amesema: "Vifaa vitatengeneza na kutegemewa na vilevile kutumiwa kuchukua maamuzi katika mahakama za uhalifu.
"Pia vinaweza kusaidia maafisa wa usalam kutathmini haraka na bila kutambuliwa saa za picha na maelfu ya picha za uhalifu ."