Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Makasisi wa kikatoliki wafungwa jela kwa kuwanyanyasa watoto viziwi Argentina
Mahakama nchini Argentina imewahukumu makasisi wawili wa Kanisa Katoliki la Roma kifungo cha zaidi ya miaka 40 jela kila mmoja v kwa kuwanyanyasa kingono watoto viziwi katika shule ya kanisa.
Horacio Corbacho na Nicola Corradi, pamoja na muhudumu wa bustani, walipatikana na hatia ya kuwabaka na unyanyasaji katika shule ya kikatoliki iliyopo katika jimbo la Mendoza kuanzia mwaka 2004 hadi 2016.
Waathiriwa kadhaa walikuwa mahakamani kushuhudia kutolewa kwa hukumu Jumatatu.
Kesi hiyo imeishitua Argentina, nchi ambayo anatoka Papa Francis, huku wengi wakilishutumu kanisa kwa kuzorota kuchukua hatua.
Kanisa Katoliki limekabiliwa na shutuma za unyanyasaji wa kingono wa watoto katka maeneo mbali bali duniani katka kipindi cha miongo michache iliyopita.
Mahakama ilibaini nini?
Jumatatu, mahakama katika mji wa Mendoza alimhukumu kasisi wa Kiargentina kifungo cha miaka 45 jela.
Padre huyo mwenye umri wa miaka 59 alipatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono watoto katika shule inayofahamika kama Instituto Antonio Provolo de Mendoza katika mji wa Luján de Cuyo.
Corradi, mwenye umri wa miaka 83-mwenye uraia wa Italia, alihukumiwa kifungo cha miaka 42 jela.
Alikuwa anachunguzwa kwa unyanyasaji alioutekeleza katika shule ya Verona, nchini italia miaka ya 1970, lakini hakuwahi kushitakiwa.
Armando Gómez, muhudumu wa bustani katika shule ya Luján de Cuyo alihukumiwa kifungo cha miaka 18 jela.
Hawawezi kukata rufaa juu ya uamuzi wa mahakama kwa mujibu wa sheria za Argentina kuhusu makosa hayo.
Unaweza pia kusoma:
Umma umepokea vipi hukumu hiyo?
Hakuna mshtakiwa hata mmoja aliyetoa kauli yoyote baada ya hukumu kusomwa.
Baadhi ya mama za waathiriwa waliokuwepo mahakamaniwalionekana wakilia na kukumbatiana.
Wakati huo huo , umati wa watu wengi wao wakiwa ni vijana walishangilia hukumu ilipotangazwa nje ya mahakama.
" Haujui ina umuhimu gani hukumu hii kwetu, na kwa dunia, "mfanyakazi wa kiwandani Ariel Lizárraga, baba wa mmoja wa waathiriwa, alinukuliwa akisema na Washington Post.
"Kanisa limekuwa likijaribu kuficha unyanyasaji huu. Lakini mapadre hawa waliwabaka na kuwanyanyasa watoto wetu. Watoto wetu wasiosikia! Leo, mwiko dhidi ya makasisi wanaoshutumiwa unaishia hapa ," alisema.
Majibu ambayo hayajajibiwa
Hukumu katika kesi hii ni ya hivi karibuni inayotia doa katika namna Kanisa Katoliki la Roma linavyoshughulikia kesi za unyanyasaji wa kingono dhidi kote duniani.
Kesi hiyo imewatisha watu wa Argentina, ambako makumi ya kesi za unyanyasaji katika Kanisa Katoliki umejitokeza katika miaka ya hivi karibuni.
Waathiriwa wa Mendoza waliambiwa jinsi walipokuwa watoto walivyozuiwa kutumia lugha za ishara ili wasiweze kuwasiliana juu ya yale waliyokuwa wakitendewa.
Mahakama ilisikiliza pia jinsi waathiriwa walivyobakwa.
Waargentina wengi wanauliza ni kwanini polisi na mfumo wa sheria ndio waliochukua uamuzi wa kufunga shule na kuwazuwia wanyanyasaji kutowafikia waathiriwa wao - na sio Kanisa Katoliki.
Unaweza pia kutazama: