Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanafunzi akamatwa baada ya kuonesha picha mtandaoni ikionesha shida ya maji chuoni
Mwanafunzi wa Chuo kikuu nchini Tanzania amekamatwa baada ya kuweka picha mtandaoni ikionesha wanafunzi wengine wakiwa wamepanga mstari kwa ajili ya kukinga maji , Shirika la kutetea haki za binaadamu limeeleza.
Mugaya Tungu aliwapiga picha wanafunzi wenzie wakiwa kwenye mstari wakiwa na ndoo zao za plastiki, kisha akaiweka mtandaoni picha ambayo ilisambaa mitandaoni. Alikamatwa muda mfupi chumbani kwake. Shirika la kutetea haki za binaadamu limeeleza.
Tungu hajashtakiwa bado na polisi hawajasema chochote kuhusu kesi hiyo, lakini inaamini atashtakiwa chini ya sheria ya makosa ya kimtandao.
Tukio hilo limeamsha hisia mbalimbali mitandaoni watu wakionesha kushtushwa kwa kile wanachokiona kuwa ukiukaji wa haki za binaadamu.