Diamond na Etoo kuanzisha chuo cha mafunzo ya mpira

Diamond

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutokaTanzania Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amesema yupo katika mazungumzo na mchezaji maarufu wa mpira kutoka Cameroon, Samuel Eto'o kutaka kujenga shule ya mpira nchini humo.

Imeripotiwa katika Daily News kuwa mwanamuziki huyo alituimbuiza katika sherehe za tuzo za shirikisho la mpira barani Afrika, (CAF) iliyowaburudisha watu wengi wakiwemo meneja Gianni Infatino na wachezaji wengine.

Katika kurasa yake ya tweeter, Diamond amebainisha kuwa na mazungumzo na Eto'oo kwa muda mrefu sasa ya kutaka kuanzisha klabu ya mchezo wa mpira kwa sababu ukanda wa Afrika mashariki una wachezaji mpira wa baadae wenye uwezo.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Diamond amesema ''Hapo awali, nilidhani kuwa kujihusisha na maswala ya michezo ni kitu kisichokuwa na faida, lakini sasa naona ni jambo la faida sana…Huko mbeleni? Nitakuwa mmiliki wa timu yangu mwenyewe, ambayo tayari inafanya biashara kwenye premiere ligi kwa sababu sitaki kuanza mwanzo kabisa.''

Mwanamuziki huyo hakutoa muda kamili wa mradi huu lakini ni wazi kabisa kuwa anataka kununua moja ya klabu zilizopo sasa au mchezaji maarufu.

Katika mitandao ya kijamii watu wengi wameonesha kufurahishwa sana na jambo hili na kumtakia kila la heri kwenye mradi huo.