Je ni nini kilichoshambuliwa Iran?

Chanzo cha picha, EPA
Iran imetibua jaribio la uhalifu wa mtandaoni chini ya juma moja kulingana na waziri wa mawasiliano nchini humo.
Mohammed Javad Azari-Jahromi alisema kwamba shambulio hilo lilikuwa likilenga mifumo ya kielektroniki ya serikali. Waziri huyo hakutoa maelezo.
Madai kama hayo yalitolewa siku ya Jumatano kuhusu shambulio baya zaidi. Mwezi Juni mwaka huu, mfumo wa silaha wa Iran ulishambuliwa, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti.
Ni nini kilichoshambuliwa Iran?
Bwana Jahromi alitoa tangazo hilo kuhusu shambuliuo la pili wiki hii katika mtandao wa Twitter.
Alisema kwamba mfumo wa Dejfa Fortress ulifanikiwa kuzuia shambulio hilo ambalo lilitumia kirusi 'Well-known APT27'- ambacho wataalam wamekihusisha na washambuliaji wanaozungumza lugha ya Kichina.
Bila kutoa maelezo zaidi, waziri huyo alisema kwamba sava na hackers zilishambuliwa . Jumatano iliopita, bwana Jahromi aliambia maafisa wa Iran news Agency kwamba shambulio hilo kubwa la mtandaoni lililenga miundo msingi ya Iran.
Siku moja awali, waziri huyo alifutilia mbali ripoti kwamba mamilioni ya akaunti za benki za Iran zilishambuliwa.
Kwa nini Marekani iliishambulia Iran mwezi Juni?
Kulingana na gazeti la The Washington Post, shambulio hilo la Marekani - kama anavyosema rais Trump alijiondoa katika hatua ya kuishambulia Iran - liliharibu mifumo ya kompyuta za serikali, mifumo inayodhibiti urushaji wa silaha pamoja na mashine zinazorusha makombora.
Marekani ilikuwa ikijibu kuangushwa kwa ndege yake isio na rubani pamoja na mashambulizi ya meli za Marekani ambazo taifa hilo imelaumu Iran, lilisema gazeti la The New York Times.

Chanzo cha picha, EPA
Marekani inatarajiwa kuiwekea vikwazo zaidi Iran ambavyo rais Trump amevitaja kuwa vikubwa zaidi.
Alisema kwamba vikwazo hivi vilihitajika kuizuia Tehran kutotengeneza silaha za kinyuklia akiongezea kwamba shinikizo za kiuchumi zitaendelea hadi pale Tehran itakapobadili mwenendo wake.
Hali ya wasiwasi kati ya Marekani na Iran imeongezeka tangu Marekani mwaka uliopita kujiondoa katika makubaliano ya mpango wa kinyuklia wa Iran wa mwaka 2015 na kurudisha vikwazo hali ambayo imeathiri uchumi wa Iran.
Maafisa wa Marekani pia wameushutumu utawala wa Iran na washirika wake kwa kutekeleza mashambulizi makali ya mtandaoni dhidi ya viwanda vya Marekani na vitengo vya serikali.














