Mzozo wa Cameroon : 'Ninasoma shule ya siri'

Iliyochapishwa

Mvulana mwenye umri wa miaka kumi na mmoja Mackjourney huenda kusoma katika shule ya siri nchini Cameroon.

Wakati hivi karibuni familia yake ilivyotoroka uasi wa wanaotaka kujitenga katika majimbo yanayozungumza kiingereza , walifikiri kuwa wamepata mahala ambapo anaweza kuwa anasoma kwa usalama.

Lakini hilo limegeuka kuwa ni kinyume kwani shule anayohudhuria mjini Douala, ambao ni mji mkuu wa Cameroon, iko katika hatari ya kufungwa kwasababu inaonekana na a maafisa ni shule haramu.

Shule kama hizo zisizokubalika kisheria zimeanzishwa kwa haraka mjini Douala, ambako wengi wa wakaazi ni wazungumzaji wa lugha ya Kifaransa.

'Mshambulio ya risasi'

Nyingi kati ya shule katika majimbo yanayozungumza lugha ya Kiingereza kaskazini- Magharibi ukiwemo mji wake mkuu Bamenda, na Kusini-Magharibi zimefungwa kwa miaka mitatu iliyopita, na kuwafanya watoto zaidi ya 600,000 kukosa shule.

''Niliondoka Bamenda kwasababu kulikua na vita . Walikua wanawauwa watu na kuwapiga watu risasi," Mackjourney aliiambia BBC.

Shule ambazo bado zimefungwa ziko katika hatari ya kushambuliwa na wapiganaji wanaotaka kujitenga.

"Tulikua tunakaa darasani na kusikia risasi zinaanguka kwenye paa la darasa kama mvua . Ilikua inatisha," alisema.

Baadhi ya wafanyabiashara mjini Duara wamejitolea kuwapa elimu- kwa gharama.

Mackjourney hutembea mwendo wa kilomita 2 (zaidi ya maili moja) kila asubuhi akipitia njia nyembamba katika eneo la vichaka kwenda katika shule yake , iliyotengenezwa kwa mbao bila madirisha.

Kutoka ndani ya darasa wanaweza kuona majani marefu pande zote.

Eneo hilo limechaguliwa ili iwe vigumu kugundulika na mamlaka.

Kuna shule ya pili ya kibinafsi aliyokuwa ambayo alisomea mjini Douala - ya kwanza ilifungwa na serikali kwa kuwa haikuidhinishwa.

Maafisa wanasema kuwa shule ni lazima iwe na uwanja wa kuchezea, maktaba na madarasa ili isajiliwe rasmi.

Zaidi ya shule 250 zimefungwa.

Lakini wamiliki wa shule hizi, wako tayari kuvunja sheria kwani kuna pesa ambazo wanapata kutoka kwa wazazi wanaohangaika kuwapatia watoto wao elimu.

Huku karo ya shule ikiwa ni $200 (£150), kiwango ambacho ni mara nne ya malipo ya mwezi ya chini kwa mwaka , wanaweza kuingizia pesa hizo kupitia ghasia zilizosababishwa na mzozo."Kulipia gharama ya usajili halikua jambo rahisi kwetu ," alisema mama yake Mackjourney.

Sawa na wazazi wengine, anasema kwa wale waliokimbia mzozo hawana chaguo jingine kwani hali inaendelea kuwa ngumu zaidi kupata nafasi katika shulezi zinazokubaliwa na serikali.

Maafisa wamefunga zaidi ya shule 260 tangu mwanzo wa mwaka wa masomo mwezi Septemba na wakosoaji wanasema haikutoa suluhu mbadala.

Afisa kutoka idara ya elimu kutoka kitongoji cha Wouri mjini Douala , Sylvestre Fils Moukalla, alisema kuwa serikali ilichukua hatua za kuwapokea wanafunzi wanaotoroka mzozo

"Waziri wa Elimu ya sekondari aliuma muungano wa Wazazi na Waalimu (PTA ) mamlaka ya moja kwa moja ya kujenga madarasa zaidi katika shule mbali mbali.

"Miungano hii ya PTA huchangisha raslimali nyingi kujenga madarasa na matokeo yake tatizo la wingi wa wanafunzi kupita kiasi madarasani limetatuliwa.Kwa mfano katika Wouri watoto wote wamepata madarasa," alisema.

Lakini hali halisi ni kwamba mengi ya madarasa yaliyopo yamejaa kupita kiasi.

Masomo ya nyumbani

Baadhi ya wazazi pia wanapenda ukweli kwamba shule za kibinafsi huwafundisha watoto wao kwa kiingereza - na sio Kifaransa.

Huu sio mzizi wa mzozo katika majimbo yanayozungumza kiingereza, ambayo ni numbani kwa 20% ya Wakameroon ambao ni takriban milioni 25.

Matatizo yalianza mwaka 2016 kufuatia uamuzi wa serikali wa kuongeza matumizi ya Kifaransa katika shule na mahakama hususan ni katika majimbo yanayozungumza Kiingereza.

Sula muhimu katika mapambano ya wanaotaka kujitenga limekuwa ni kususiwa kwa shule, kuwateka wanafunzi na waalimu wanaokiuka amri.

Mwezi Februari, watu 176 wengi wao wakiwa ni wanafunzi , walitekwa na kuachiliwa siku mbili baadae.

Badhi ya wale ambao walitorokea maeneo yanayozzungumza Kifaransa, akiwemo Claude Ngwa, wameamua kusomea nyumbani.

Unaweza pia kusoma:

Ni Kwanini Cameroon bado imegawanyika kwa misingi ya ukoloni:

  • Ilitawaliwa na Ujerumani mwaka 1884
  • Majeshi ya Uingereza na Ufaransa yaliwalazimisha Wajerumani kuondoka mwaka 1916
  • Cameroon iligawanyika mara tatu miaka iliyofuatia- 80% ikaenda kwa Ufaransa na 20% ikaenda Uingereza
  • Cameroon iliyoyoendeshwa na Ufaransa ikawa huru mwaka 1960
  • Kufuatia kura ya maoni , Eeneo la Uingereza Kusini likajiunga na Cameroon na Wakameroon wa Kaskazini wakajiunga na Nigeria inayozungumza kiingereza.