Mashambulizi ya New Jersey: Wauaji 'walilenga duka la jumla la Wayahudi'

Duka la jumla la Kosher liliengwa na watu waliojihami kwa bunduki mjini Jersey, Disemba 11 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Duka la jumla la Kosher liliengwa na watu waliojihami kwa bunduki mjini Jersey
Iliyochapishwa

Duka la jumla mjini New Jersey lililengwa katika mashambulizi ya bunduki yaliosababisha vifo vya zaidi ya watu sita wakiwemo washukiwa wawili, maafisa wanasema.

Chanzo cha mashambulizi hayo haijabainishwa, lakini meya wa jiji la Jersey ameandika katika Twitter yake kuwa"chuki dhidi ya wayahudi" haina nafasi katika mji huo.

Washukiwa wanaamiwa kuwaua majesusi katika maeneo tofauti mjini humo na kisha wakatoroka kwa kutumia gari la kukodi kufika katika duka hilo la jumla.

Video za usalama zinawaonesha wakipiga risasi nje ya duka hilo la jumla kabla ya kuingia.

Wachunguzi wanaamini kuwa miili mitatu iliyopatikana ndani ya duka la jumla la kosher ni ya watu watatu waliouawa na washambuliaji hao , ambao pia walipatikana wameuawa ndani ya jingo hilo kufuatia makabiliano ya saa nne dhidi ya polisi siku ya Jumanne.

Mhasiriwa mwingine alijerurihiwa, lakini alifanikiwa kutoroka but managed to escape, maafisa bwalisema siku ya Jumatano.Afisa mmoja wa polisi na takriban watu watano wamefariki katika msururu wa makabiliano makali ya risasi katika mji wa Jersey katika jimbo la New Jersey.

Shule kadhaa na biashara zilifungwa kwa muda. Sababu ya kisa hicho haijajulikana. Mamalka inasema haiamini kwamba lilikuwa shambulio la kigaidi.

Mamlaka ilimtambua afisa wa polisi aliyefariki kuwa Joseph Seal mwenye umri wa miaka 39 ambaye alikuwa katika mpango wa kuwapokonya watu silaha haramu katika jimbo la New Jersey.

Akizungumza na ripota , afisa mkuu wa polisi wa mji wa Jersy Mike Kelly alisema kwamba bwana Seal alikuwa akiongoza maafisa wa polisi katika kuondoa bunduki haramu mitaani.

Maafisa wa polisi wawasili katika eneo la tukio mjini Jersey

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Makumi ya maafisa waliojihami walipelekwa katika eneo hilo huku washukiwa hao wakijificha ndani ya duka moja la jumla

Bwana Kelly alisema kwamba ufyatulianaji wa risasi ulizuka kwa mara ya kwanza katika makaburi ya umma mwendo wa saa sita saa za Marekani.

Inaaminika kwamba bwana Seals aliuawa alipokuwa akiwakaribia washukiwa. Wawili hao walitoroka katika eneo hilo na kujificha katika duka moja la jumla ambapo waliendelea kuwafyatulia risasi maafisa wa polisi.

Makumi ya maafisa wa polisi , ikiwemo wale wa kitengo cha Swat na maafisa wengine walipelekwa katika eneo hilo na kusababisha mauaji ya watu watano katika duka hilo- huku wawili kati yao wakidaiwa kuwa washukiwa hao.

Maafisa wa polisi wanachunguza eneo la ufyatulianaji wa risasi

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Polisi wanasema kwamba watu watatu katika duka hilo huenda waliuawa na washukiwa hao

Maafisa wa polisi wanasema kwamba washukiwa hao walikuwa wamejihami na bunduki zenye uwezo mkubwa na walifyatua mamia ya risasi wakati wa kisa hicho.

Bwana Kelly alisema kwamba inaaminika watu watatu katika duka hilo waliuawa na washukiwa hao, na kusisitiza kwamba uchunguzi kamili utafanyika huku majibu yakichukua muda.

Mtu mmoja ambaye alinusurika anaendelea na matibabu , na gari lililotumiwa na washukiwa hao linachunguzwa na wataalamu wa kutegua mabomu.

Waathiriwa ni kina nani?

Waathiriwa watatu waliouawa ndani ya duka hilo mashambulio ya risasi yalipozuka, lakini mmoja walifanikiwa kutorokabaada ya kujeruhiwa.

Walitambuliwa kama na maafisa wa New Jersey kama Mindy Ferencz, 32; Miguel Douglas, 49 na Moshe Deutch, 24.

"Mindel Ferencz, Mungu ailaze pema roho, alikuwa mwanzilishi wa duka hili,"alisema Rabbi David Niederman, ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitisha kifo cha mama huyo wa watoto watano.

"Alikuwa mama mwenye upendu mkuu kwakila mtu,"aliongeza. "Inasikitisha kuwa maisha yake yaikatizwa ghafla."

Moshe Deutch

Chanzo cha picha, Facebook/ Chai Lifeline

Maelezo ya picha, Moshe Deutch, 24

Mama yake Ferencz aliliambia jarida la New York Times kuwa mume wake , ambaye anamilikiduka hilo la jumla alikuwa amechukuwa mapumziko, ya kwenda kufanya kazi katika sinagogi la wayahudi lililo karibu dakika chache kabla ya makabiliano nya risasi kuanza.