Stanley Ngara: Mfalme wa kondomu wa Kenya anayekabiliana na maambukizi ya Ukimwi

Chanzo cha picha, EPA
Stanley Ngara, anayefahamika kwa jina maarufu kama mfalme wa kondomu wa Kenya, amekuwa akisambaza mipira ya kondomu katika jiji la Nairobi, kwa lengo la kuhamasisha watu umuhimu wa kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi(VVU).
Leo ulimwengu unapoadhimisha siku ya Ukimwi dunini, shirika la habari la EPA linaripoti kuhusu mfalme huyu wa aina yake.

Chanzo cha picha, EPA
"Mipira ya kondomu imehusishwa na uasherati kwa sababu watu hufikiria kuwa mtu akiwa ameathirika na ugonjwa huo basi yeye ni kahaba au anashiriki ngono na zaidi ya mtu mmoja," aliliambia shirika la habari la Bloomberg agency.
Mfalme huyo anajaribu kukabiliana na dhana hiyo potofu inayosababisha unyanyapaa.

Chanzo cha picha, EPA
Akishirikiana na washika dau wengine Bw,Ngara huzungumzia maambukizi ya VVU na Ukimwi, suala ambalo anasema bado halizungumziwi hadharani.

Chanzo cha picha, EPA
"Kenya inahitaji wafalme na malkia wengi zaidi wa mipira ya kondomu," mwanaharakati huyo wa mika 47-aliiambia shirika la habari la EPA.

Chanzo cha picha, EPA
Umoja wa mataifa unasema kuwa karibu watu milioni 1.6 nchini Kenya wanaishi na virusi vya ukimwi tangu mwaka 2018 huku wengine 25,000 walifariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi.
Japo hatua kubwa imepigwa kukabiliana na ugonjwa huo katika miaka ya hivi karibuni, suala la unyanyapaa dhidi ya ugonjwa huo zinalemaza juhudi za kudhuibiti maambukizi, mkuu wa UNAids Winnie Byanyimaa aliiambia BBC.

Chanzo cha picha, EPA
"Tunahofia huenda tukapoteza mapambano dhidi ya unyanyapaa, kwa sababu vijana ambao wamepatikana na virusi vya ukimwi-hawajitokezi kutafuta matibabu kwa kuhofia kuhukumiwa… kwasababu UKIMWI bado inachukuliwa kama dhambi, alisema.













