Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Aliishi mitaani na sasa analipwa mamilioni ya pesa, aliwezaje?
Imekuwa ni miaka miwili ya matukio kwa Gavin Eastham ambaye amekuwa akilala katika kijisanduku cha simu ya umma mtaani kwa ukosefu wa ajira ambaye sasa anapokea mamilioni ya pesa kwa kuendesha biashara ya mafunzo ya masumbwi.
Mwezi Februari mwaka jana, alijipata akikimbilia kwenye kona za mitaa katika usiku wake wa kwanza wa maisha ya mitaani.
Ndoa ya Eastham mwenye umri wa miaka 36 ilikuwa imevunjika na alikuwa na jeraha la mgongo, na kwa hivyo hakuwa na uwezo wa kufanya kazi.
"Kwasababu sikuwa na asili ya Wales kaskazini , ilimaanisha kuwa sikuwa na anwani. Sikuwa na mahali popote pa kwenda ,"anasema.
Mke wake wa zamani alifikiri kuwa alikuwa na mahala pa kuishi , lakini haikuwa hivyo.
Mwanzo aliamua kwenda katika maktaba ya eneo hilo, walau kujikinga na baridi, lakini alihisi kuwa muda unakwenda na anapaswa kubadili mambo.
"Nilifikiria kuwa ningeendelea kuwa mtu asiye na makazi, watu wangeniona hivyo, na kama ningekuwa mtu asiye na makazi watu wangenidhrau ," alikiambia kipindi cha BBC cha biashara cha Wake Up to Money.
Baada ya kuishi siku chache pale ndani , mhudumu wa maktaba akaanza kunishuku. Nilimwambia nina mipango ya kuanzisha biashara yangu.
"Nilihisi kwamba ninahitaji kufanya mabadiliko chanya, ninahitaji kufanya kitu fulani ," alsiema.
Pia aliitumia maktaba kujifunza kitu cha muhimu : "Nilikuwa ninafanya utafiti juu ya kuishi maisha ya kutokuwa na makazi ya kuishi . Mimi ni mtu wa mjin kwa hiyo nilifanya utafiti kidogo kwa kusoma blogi na mitandao kuhusu ni jinsi gani mtu anaweza kuishi maisha ya mitaani ."
Wakati usiku alikuwa akifikiria juu ya kupata malazi, mchana alikuwa anasoma vitabu juu ya mikakati ya biashara.
"Hii ni kama uendawazimu, lakini kitu ambacho nimekuwa nikikifanya vizuri kilikuwa ni ufundishaji wa ndondi. Nikajiuliza ni vipi ninaweza kugeuza kitu hiki kuwa fursa ya kuyanusuru maisha yangu ya baadae?"
Alianza kufanya utafiti na akabuni jina na ngembo, akaandika mtaala na akanunua jina kwa pauni £1.58.
"nilifikiria- kama nitakuwa na jina nitaweza kuendelea."
"Hii ndoto ambayo nilifikiria nitaitimiza wakati mmoja ilitia nguvu niliyoihitaji kuishi ."
Baada ya kuishi wiki tatu mitaani, aliweza kupata makazi ya muda halafu , mwezi Mei mwaka jana, akazindua shule ya kufundisha mchezo wa masumbwi (ndondi) aliyoiita Cobra Life katika eneo la Flintshire, Wales.
Na sasa anasema anaendesha "biashara inayostawi, inaymuingizia mamilioni ya pesa."
Huku akiwa na mipango ya kuiendeleza, anapanga kumuajiri mkufunzi wa kudumu: "Hii itanipa fursa ya kuondoka ulingoni na kupanga mikakati ya kuipanua zaidi ," alisema.
Anasema mafunzo ya ndondi yanampa motisha ya kuendelea: " Ujuzi huu muhimu umekuwa ndani yangu tangu nilipokuwa mtotokwa hiyo hata kama nilikuwa na wakati mgumu nilijua nina uvumilivu na nikazingatia maono yangu juu ya malengo ambayo yalikuwa yameandikwa kwenye karatasi!"