Siku ya choo duniani: Mjadala wa kutumia maji kujiosha au kujifuta baada ya kwenda haja

Iliyochapishwa

"Kama waarabu lazima tuhakikishe tuna vitu vitatu kila tunapojiandaa kusafiri: Pasi zetu za usafiri, bunda la pesa, na keni dogo la maji,"alitania mchekeshaji wa Misri Bassem Youssef wakati akitumbuiza mara ya kwanza katika tamasha la Uingereza mwezi Juni.

Aliendelea mbele na kuonesha paipu ya maji inayofahamika kama shattaf (au"bomba la kuosha makalio").

"Sielewi: nyinyi ni watu wa nchi zilizoendelea sana duniani. Lakini linapokuja suala la kujisafisha makalio, mko nyuma."

Watu wengi huenda wakakubaliana na Youssef.

Suala la watu katika mataifa ya magharibi hujipangusa makalio baada ya kujisaidia maliwatoni badala ya kutumia maji limezua gumzo duniani.

Maji husafisha vizuri zaidi kuliko kutumia karatasi.

Wale ambao wamezoea kutumia maji je, huwa wanajiuliza kama ni jambo jema kujisafisha kwa kutumia karatasi pekee?

Mataifa mengi duniani watu wameanza kusitisha kutumia maji chooni.

"Usafi wa ubeberu"

Na sio ukweli kwa mataifa yasiokuwa ya magharibi duniani: Wafaransa pia waliupatia ulimwengu mtindo wao wa ujenzi 'bidet'.

Japo kifaa hicho kimepoteza umaarufu Ufaransa, bado kinatumika Italia na Argentina, kwa mfano.

Youssef anaamini kuwa kifaa hicho cha kujisafishia "bum gun" hupatikana zaidi nchini Finland.

Ingawa bado mataifa mengi yanaunga mkono matumizi ya kujifuta na makaratasi - ikiwa ni pamoja na Uingereza na Marekani.

Na ikilinganishwa na maeneo mengine duniani, "mataifa haya mawili yamekuwa na ushawishi mkubwa katika utaratibu wa usafi chooni", anasema mwanahistoria na msanifu wa majengo, Barbara Penner katika kitabu chake kinachofahamika kama ''Bathroom''.

Mataifa ya Kiafrika yanayoegemea ujenzi wa bafu za kimarekani yalipata umaarufu miaka ya 1920, na yalijulikana na "usafi wa ubeberu".

Hata hivyo matumizi ya maji yanaungwa mkono na watu katika mataifa mengi ya Kiislamu, kwa sababu elimu ya dini inashauri utumiaji wa maji kudumisha usafi.

Mtu mmoja ambaye amevutiwa na mjadala wa kutumia maji au karatasi chooni ni Zul Othman, mshirikishi wa mradi wa serikali nchini Australia, ambaye amefanya utafiti kuhusu utamaduni na mitazamo ya kihistoria kuhusu vifaa vya choo.

Utafiti wa Othman unaonesha kuwa waislamu wa asili ya Australia wanajenga bafu na vyoo mtindo wa magharibi ambapo wanatumia karatasi na baadae kujiosha, kwa kutumia jagi ya maji au kuweka mfereji karibu na vyoo vyao.

Lakini suala la usafi halihusishwi na waumini wa dini ya kiislamu pekee.

Astha Garg, mwanasayansi wa masuala ya data kutoka Mumbai ambaye amekuwa akifanya kazi katika eneo la San Francisco kwa zaidi ya miaka miwili iliopita, anasema kuwa aliangazia uzuri na ubaya wa kutumia maji chooni kwake.

Othman kwa upande wake anazungumzia kushangazwa kwake na hatua ya watu katika mataifa ya magharibi kukazania matumizi ya karatasi chooni.

Anasema wanafunzi wenzake mjini Sheffield, Uingereza, walilazimika kutumia noti ya pauni ishirini kujifutia chooni baada ya kuishiwa na tishu.

Mwanafunzi huyo aligutushwa na jinsi vitu vingi vinavyotumika chooni kwa mwaka wakati inasadikiwa kuwa watumiaji wa karatasi duniani kwa mwaka - hutumia roli 141 kila mmoja kwa mwaka.

Astha Garg pia alishangazwa na takwimu ya matumizi ya tishu chooni.

Aliongeza kuwa gharama ya kifedha na uharibifu wa mazingira

Familia ya Kuo sasa inatumia karatasi ya chooni kwa kiwango kidogo sana.

Tamaduni nyingi karne hii huwa wana namna nzuri ya kujisafisha.

Vyoo vya chini yaani ya kuchuchumaa vimeonekana kupendwa na wengi na kuwa rahisi kusafisha.

Marekani wamegeuza chooni kuwa sehemu ya kifahari , kwa kuwa na choo cha kifahari.

Vyoo vya Marekani, kuna vitabu vingi vya hadithi fupi huwa vimewekwa maliwatoni ambavyo mtu anaweza kusoma akiwa anajisaidia.

Wakati huko nchini China, wazazi wanawakemea watoto wao kutosoma wakiwa chooni.