Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watoto huwa na vidole kama mijusi tumboni ambayo huondoka kabla kuzaliwa
Utafiti wa madaktari umeonesha kuwa watoto wakiwa tumboni huwa na misuli mikononi inayofanana na mijusi, ambayo hupotea kabla ya kuzaliwa.
Wanabaiolojia wanaeleza katika jarida la kisayansi la development kuwa haya ni moja ya mabadiliko ya kale kuonekana kwa binadamu.
Wanakadiria misuli hiyo kuwa na umri wa miaka milioni 250, mabadiliko hayo ni kama ambavyo hutokea pale reptilia anapobadilika kuwa mamalia.
Haijulikani ni kwanini mwili wa binadamu unatengeneza na kuondoa misuli hiyo kabla ya kuzaliwa. Wanaibailojia wameendelea kusema kuwa hatua hii ya maendeleo huweza ikawa sababu kuu ya kufanya vidole gumba viwe tofauti.
Vidole gumba vina misuli ya ziada ukilinganisha na vidole vingine.
Mara chache sana unaweza kumkuta mtoto ama mtu mzima kuwa na kidole cha ziada na misuli ya mikono, lakini kamwe sio misuli mithili ya mjusiambayo ilionwa na wanabailojia hao pale walipoangalia picha skani za 3D za mimba (kiinitete na fetusi) ya wiki saba hadi kumi na tatu.
Muda mwingine viking'ang'ania sana huweza sababisha ulemavu wa viungo. Wanabailojia wanasma katika matokeo yao, ndani ya watoto kumi na tano wanaoendelea kukua wanaweza kusaidia kutafuta jibu la matatizo ya kuzaliwa nayo.
Mwandishi mkuu wa utafiti huo Dkt Rui Diogo, kutoka Chuo Kikuu cha Howard nchini Marekani amesema ''tuna misuli mingi sana inayoenda kwenye kidole gumba, hususani kwenye mwondoko wa vidole gumba, lakini tumepoteza misuli mingi ambayo inaenda kwenye sehemu nyingine za mwili.
''Katika kukua kwetu hatuvihitaji sana.''
''lakini ni kwanini ipo hapo? Hatuwezi sema ni hatua ya ukuaji, angalia ni tofauti na kuanza tena mwanzo, misuli inaenda kuwa miwili, mitatu, minne, mitano halafu naacha mmoja uende kwenye kidole gumba.
''Labda sio rahisi. Labda inabidi kutengeneza sehemu fulani ya msuli halafu inapotea kwenye sehemu nyingine lakini bado inaendelea kung'ang'ania kwenye kidole gumba.''
Sehemu za mwili zisizo na faida?
Amesema mipangilio ilikuwa ni ya kushangaza kuliko baadhi ya mabadiliko ambayo mwanadamu hupitia, kama vile appendix, kutokwa meno ya mwisho na kifandugu.
''Misuli hii ilipotea miaka milioni mia mbili hamsini iliyopita,'' amesema Dkt Diogo.
''hakuna mamalia mtu mzima, hakuna panya wala mbwa wenye misuli hiyo. Inavutia sana. Ilikuwa ni zamani sna.''
''tulikuwa na uelewa mpana sana kuhusu ukuaji wa samaki, vyura, kuku na panya kuliko spishi wetu wenyewe lakini njia hizi mpya zinatuwezesha kuona ukuaji wa binadam kiundani zaidi.''
Dkt Sergio Almecija, mwana anthrolopojia anayesomea ukuji wa nyani na binadamu, katika jemgo la historia la marekani, amesema matokeo yake yameleta heshima kubwa kwenye ukuaji wa binadamu lakini imezua masawali mengi sana.
'' maana kuu ya uchunguzi huu ni kutuwezesha sisi kuona kwa undani zaidi ni lini haswa katika muendelezo wa kukua kwetu vitu vingine hutokea au hupotea'', aliendelea kueleza.
''Swali la muhimu kwangu kwa sasa ni kitu gani kingine tunakosa kuona? Tutagundua nini pale mwili wa binadamu utapochunguzwa kwa makini sana katika hatua yake ya ukuaji?
'' Ni nini kinasababisha vitu vingine kupotea na kurudi kuonekana tena? Sasa tunaweza kuona jinsi gani inavyokuwa, lakini je ni kwanini?''
Wanabailojia wanamipango ya kuangalia mwili wa binadamu kiundani zaidi. Kwa sasa wameweza kuangalia miguu na kujua misuli ya zida huota na kupotea wakati watoto wakiendelea kukua tumboni.
Nyani na Sokwe bado wana misuli hii na hutumia kupanda na kushika viu vingine kwa kutumia miguu yao.
Dkt Diogo amesema ''baadhi ya vitu yunavyo vipotez a, haimaanishi kama tunakuwa binadamu bora au kuendelea zaidi. Hapana. Tunapoteza vitu ambavyo vinaweza kutengeneza binadamu ambao sio wa kawaida.
''Binadamu hao watakuwa wanabaki na misuli hiyo ya ziada kwa sababu wanakuwa na uwezo wa kusogeza viungo vyote vya mwili vikiwemo miguu na vidole gumba.
''Tumevipoteza kwa sababu hatuvihitaji.''