Wanafunzi 7 wafariki baada kuangukiwa na paa la darasa Kenya

Makumi ya wanafunzi waliondoshwa kwenye eneo la tukio lakini wengi wanaaminiwa kuwa bado wamekwama kwenye vuifusi vya jengo

Chanzo cha picha, TWITTER / @ROBERTALAI

Maelezo ya picha, Makumi ya wanafunzi waliondoshwa kwenye eneo la tukio lakini wengi wanaaminiwa kuwa bado wamekwama kwenye vuifusi vya jengo
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Wanafunzi saba wamethibishwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya darasa la shule yao kuporomoka mapema Jumatatu asubuhi viungani mwa jiji la Nairobi nchini Kenya.

Jengo la mbao la shule ya msingi ya Precious Talent liliporomoka muda mfupi kabla ya masomo ya siku kuanza. Wanafunzi 50 wamelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu katika mji mkuu wa Nairobi, kulingana na msemaji wa serikali Cyrus Oguna.

Kituo cha televisheni nchini Kenya NTV kimetuma picha ya ujume wa Bwana Oguna kupitia Twitter akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio ambapo jengo liliporomoka, akiwahakikishia wazazi kwamba serikali italipia garama ya matibabu ya wanafunzi waliojeruhiwa:

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Wakati huo huo wanafunzi kadhaa bado wamekwama ndani ya jengo hilo na maafisa wa shirika la msalaba mwekundu wanaendelea na shughuli za uokozi .

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Mafisa wa zima moto wa Baraza la jiji la Nairobi kwa ushirikiano na Shirika la Msalaba mwekundu wanasaidiana wenyeji kuwaokua watoto waliokwama chini ya jengo hilo.

Kamanda wa polisi George Seda na mbunge wa eneo la Dagoreti, John Kiarie, wamethibitisha kuongezeka kwa idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo.

Wakaazi wa Dagoreti

Chanzo cha picha, Robert Alai

Mkurungezi wa shule hiyo ya kibinafsi, Moses Wainaina Ndirangu, amaeiambia Runinga ya Citizen nchini Kenya kuwa jengo hilo liliathiriwa na ujenzi wa bomba la maji taka karibu unaoendelea karibu na hapo.

Amesema wanafunzi karibu 800 wanasoma katika shule hiyo lakini ni wanafunzi 20 pekee waliokadiriwa baada ya ajali hiyo.

Unaweza pia kusoma:

Idadi kubwa ya watu waliojitokeza kutazama shughuli maafisa wa uokozi pamoja na polisi wanaong'ang'ana kufanya msako kwenye vifuzi vya darasa lililopomoka

Chanzo cha picha, REUTERS

Maelezo ya picha, Idadi kubwa ya watu waliojitokeza kutazama shughuli maafisa wa uokozi pamoja na polisi wanaong'ang'ana kufanya msako kwenye vifuzi vya darasa lililopomoka

Baadhi ya wanafunzi wanasemekana kukiimbilia makaazi ya watu walio karibu na mtaa wa Dagoretti, Magharibi mwa Jiji la Nairobi baada ya jengo la shule kuporomoka.

Afisa wa ngazi ya juu wa wizara ya elimu, Belio Kipsang, amewasili katika eneo la tukio.

Picha kweny mitandao ya habari ya kijamii zinaonyesha mamia ya wkazi wa eneo hilo wakikusanyika kuzingira eneo la tukio huku shughuli za uokozi zikiendelea kuwasaka waathiriwa wa mkasa.

Vitabu , madawati na viti vinaonekana katikakati ya vifusi.

Serikali imeanzisha uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo.

unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Mwathiriwa azungumza kuhusu janga la bwawa Nakuru