Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
New Zealand: Spika aongoza mjadala akiwa amempakata mtoto wa mmoja wa wabunge
Spika wa bunge nchini New Zealand ameonekana akimpakata mtoto wa mmoja wa mmoja wa wabunge akiongoza mjadala katika bunge hilo la wawakilishi.
Trevor Mallard aliweka picha akiwa amempakata mtoto wa kiume wa mbunge Tāmati Coffey katika mtandao wake wa Twitter yake.
Bw. Coffey, ambaye ni mbunge wa Labour wa eneo la Waiariki, alitangaza kuzaliwa kwa mtoto wake, Tūtānekai Smith-Coffey, mwezi Julai.
Siku ya Jumatano Bw. Coffey alihudhuria vikao vya bunge na mwanawe kwa mara ya kwanza baada ya kurejea kazini kutoka likizo ya uzazi.
Wakati wa kikao hicho Spika Mallard alichukua jukumu la kumpakata mtoto pamoja na jukumu la spika.
Picha hiyo ya Bw. Coffey akiwa amembeba mtoto bungeni iliwekwa na mbunge wa chama cha Green Gareth Hughes kwenye Twitter.
"Inapendeza sana kuwa na mtoto bungeni, hii ni kwa kweli ni nzuri sana @tamaticoffey," Bw. Hughes aliaandika.
Akizungumza na Newshub, Bw. Coffey alisema "Napata usaidizi kutoka kwa wafanyikazi wenzangu wote Bungeni".
Coffey ni mbunge wa hivi punde kumpeleka mtoto wake bungeni, na kufuata mfano wa wanasiasa wengine duniani.
Lib Dem kiongozi wa Jo Swinson, ambaye alihudhuria vikao vya bunge na mtoto wake mwaka 2018, na Seneta wa Australia Larissa Waters, ambaye alimnyonyesha mwanawe bungeni mwaka 2017, ni miongoni mwa wabunge waliogonga vichwa vya habari kwa kuchukua hatua hiyo.
Mwezi September mwaka jana Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern aliandikisha historia kwa kuandamana na mtoto wake wakati akitoa hotuba yake ya kwanza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.