Watu 9 wauwawa katika mashambulio ya mabomu nchini Indonesia

Chanzo cha picha, EPA
Iliyochapishwa
Idadi ya watu waliouwawa katika shambulio la kigaidi nchini Indonesia, imepanda kutoka watu wawili na kufikia watu 9.
Watu wengine 13 wamejeruhiwa, katika mashambulio ya kigaidi yaliyolenga makanisa kadhaa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Surabaya.
Miongoni mwa waliouwawa ni pamoja na mhanga wa kujitoa kufa.
Idara ya polisi kupitia kwa msemaji wake Frans Barung Mangera, imesema kuwa mashambulio matatu tofauti yalitokea kwenye makanisa- Kusini mwa Java.
Idara ya usalama imeongeza kusema kuwa, milipuko yote mitatu ilitokea dakika kumi baada ya nyingine.

Mashambulio hayo yanaminika kutekelezwa na Kundi la Islamic State linalojiita Jemaah Ansharut Daulah (JAD).








