Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Bruce Lee' achaguliwa kuwa diwani Afrika Kusini
Baada ya Vasco da Gama kuwa spika wa baraza la mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini,sasa Bruce Lee amechukua wadhfa katika baraza la mji wa Tshwane nchini humo.
Kwa wale waliokosa somo la historia ,Vasco da Gama alikuwa baharia maarufu ambaye amerikodiwa kuwa mtu wa kwanza kusafiri majini kutoka Ulaya hadi India kupitia Cape of Good Hope.
Na muda mfupi baadaye,orodha ya majina ya madiwani yaliotolewa huko Tshwane nchini humo humo yalionyesha 'Bruce Lee' akiwa katika wadhfa wa maendeleo ya kiuchumi katika baraza hilo.
Bruce Lee ni mcheza filamu kutoka nchini Marekani.