Vita vya Ukraine: BBC iko mstari wa mbele huku Ukraine ikishambulia mahandaki ya Urusi

Iliyochapishwa

Wiki mbili tangu kuanza kwa mashambulizi hayo, Ukraine inapiga hatua ndogo lakini thabiti katika maeneo matatu ya mashambulizi katika mstari wa mbele wa kilomita 1,000 (maili 620).

Wanajeshi wanaanzisha mashambulizi ya uchunguzi, huku vikosi vingi vya Ukraine vikiwa vimehifadhiwa, vikisubiri fursa kubwa ya kutekeleza shambulio dhidi ya ulinzi wa Urusi ili kuanzisha shambulio kuu na kujaribu kuikomboa tena ardhi yake kusini mwa nchi hiyo.

Vita vimekuwa vigumu huku pande zote mbili zikipata hasara kubwa , na majeshi yanayopingana yakidai kuwa yameshinda. Hatua za kijeshi kusini mwa Donetsk zimekwama, lakini mashambulikzi yanaendelea.

BBC ilijiunga na kikosi cha 68 cha Jaeger Brigade wakati vikosi vyake vya mapambano vikijaribu kupanua udhibiti wao mashariki mwa kijiji kilichokombolewa hivi karibuni cha Blahodatne.

Machoni mwao kulikuwa na mahandaki yanayolinda vikosi vya Urusi kwenye vilima vilivyo karibu.

Wanajeshi wa taaluma ya kutumia ndege zisizo na rubani wanachukua kamera, nyaya na lori dogo la kubebea risasi, makreti ya mabomu ya moshi na silaha za kutoboa.

Kando na hao, kuna dalili ndogo ya maisha huko Blahodatne. Chini ya njia, mabaki ya magari mawili ya MRAP yaliyotengenezwa Marekani yenye silaha nyingi yamekwama, moja likiwa limeteketea. Kuna zaidi ya magari haya yanayostahimili migodi ambayo yamezimwa katika Eneo hilo na hata zaidi.

"Mba;li la hilo, Warusi wanaendelea kuwashambulia," tunaonywa. Urusi imeharibu magari mengi yaliyotolewa na nchi za Magharibi, licha ya kuwa Vladimir Putin alikiri kuwa amepoteza makumi ya vifaru tangu kuanza kwa mashambulizi ya kukabiliana na Ukraine Juni 5 .

Wanajeshi wanashambulia kutoka mpande tatu: Bakhmut, ambapo wanasonga mbele kaskazini na kusini mwa jiji, ambalo linabakia chini ya udhibiti wa Urusi; kusini mwa Zaporizhzhia; na kusini mwa Donetsk, ambapo vijiji kadhaa vimekombolewa.

Blahodatne ni mmoja wapo. Shambiulio jingine latekelezwa wanajeshi wanajificha kwenye mabaki ya nyumba iliyoharibiwa.

Njia yenye sakafu chafu imewashwa kwa taa za mafuta, ikitoa mwanga laini wa manjano chini ya urefu wake hadi kwenye jiko la mawe na chuma chenye vyungu vitatu vilivyo imara juu. Taulo ipo juu ya Kamba. Mlango mbaya wa mbao unafunguka na, katika kitambaa cha kichwa, Nina Fedorivna anajitokeza.

Amekuwa akiishi hapa chini kwa mwaka uliopita. Wanajeshi wa Urusi walikuja mara moja tu, anasema.

Yeye kamwe, kwa sekunde, hakufikiria kuondoka kijijini hapo.

Mashambulizi ya mizinga imezidi , tunaondoka kupitia njia iliyo mwisho wa nyumba yake. Maiti tatu za wanajeshi wa Urusi zimelala kwenye shimo, karibu na shamba la mboga la Nina Fedorivna. Lori lenye alama ya Z, ambalo lilitumiwa na vikosi vya Urusi, limekaa karibu likiwa na matundu ya risasi .. Mapigano hapa yalikuwa karibu sana.

Katika kijiji kizima maua ya waridi yamechanua - lakini harufu ya maiti ni kali hadi kooni.

Hakuna muda wa kuchelewesha - wanajeshi wana hewa ya umakini . Ni wazi wanajiandaa kwa ajili ya kitu fulani.

Wanaelekea mashariki, na kuacha Blahodatne nyuma. Msafara wa magari mawili umetengana vyema iwapo Urusi itashambulia. Mashamba yanayozunguka yamejaa mabomu ya ardhini, huku alama za utepe mwekundu-na-mweupe zikiwekwa ardhini.

Tunapokaribia gari lingine la kivita la Marekani lililotelekezwa, kuna mlipuko, ukikosa mabaki. Inawezekana ni kutoka kwa ndege isiyo na rubani ya Urusi.

Nilikuwa katika eneo hili mnamo mwezi Machi. Wakati huo wanajeshi walio mstari wa mbele -ilikuwa vigumu kusonga mita chache kwa miezi. Urusi ilikuwa ikitumia silaha nyingi zaidi kuliko vikosi vya Ukraine, ambavyo vilijificha kwenye mahandaki vikingoja mashambulizi kuisha. Wakati huo, kamanda mmoja aliniambia walikuwa wakihifadhi makombora yao kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi hayo. Katika ziara hii, bunduki za Ukraine hazikufyatuliwa kwa siku mbili nilizokuwa na brigedi.

Magari yanaenda kwa kasi hadi kwenye mtandao wa mitaro iliyofichwa kwenye miti. Huko, kamanda wa kitengo, Sajenti Mwandamizi Andrii Onistrat, 49, anawapeleka wanajeshi wake kupitia misheni yao inayofuata - shambulio la Ukraine linapangwa kwa siku inayofuata kwenye mitaro ya Urusi, umbali wa kilomita 3 (maili 1.8) chini ya vilima vya kusini. .

Katika jaribio lao la kupanua eneo la mbele, sehemu za Brigedi ya 68 zitashambulia kutoka mashambani mashariki mwa Blahodatne na Makarivka, kwenye uwanja wa mabomu yaliotegwa ardhini na moja kwa moja atika mashambulizi ya Urusi.

Sgt Onistrat anaelekea katika kundi la wanajeshi wa itifaki na shabaha za mawasiliano. Sehemu hiyo inapoteza hadi drones tano kwa siku. Akiwa anatabasamu, anawatazama wanajeshi wake wenye uso zenye huzuni na kutoa amri moja ya mwisho: "Tabasamu - kwa nini mumekasirika ? Tunashinda vita."

Saa ishirini na nne baadaye, wengi wa wanajeshi hao hao wako kwenye shimo lililojaa maji. Shambulio hilo linaendelea.

Kutoka kwa kamera zao za uchunguzi naweza kuona magari mawili ya kivita yakipita polepole kwenye ardhi iliotegwa mabomu ya ardhini. Ndege isiyo na rubani baada ya ndege isiyo zinatumwa juu ya maeneo ya Urusi kudondosha mabomu ya moshi, na kutengeneza skrini ya moshi kwenye mitaro inayokaliwa na Warusi ili kuruhusu magari kusonga mbele na kuwadanganya maadui kupambana na silaha za vifaru. Ninapotazama, makombora ya Ukraine yanagonga miti iliopo katika mstari wa mbele wa vita.

Yuri, mwanajeshi mchanga, anakimbia ndani na nje ya shimo, akibadilisha betri za ndege zisizo na rubani na kuzipeleka angani, huku sauti zikipiga kelele na kuelekeza mahali kwenye redio. Mbu na nzi wa farasi wanakula wanaume, lakini bado "Frisbee", kutoka magharibi mwa Ukraine, amevua shati lake kwa sababu ya joto.

Adui wao hajizuii. Ninaposimama nje, shambulio la Urusi linanguka karibu na kurusha kwenye mtaro. Mtazamaji aliyesimama katika vivuli vya kuzunguka na bila silaha za mwili ni Zheka.

Kombora lingine la Kirusi linatua karibu na kuanguka . Ninatazama juu na Zheka hajatetemeka. Anapiga kelele kwa Kiingereza – anatoa matusi yanayoelekezwa kwa Warusi - na anatoa vidole viwili vya kati hewani. Milio ya roketi za Grad zinanyesha kwenye maeneo ya wanajeshi wa Ukraine.

Kwa upana zaidi, kukabiliana kunafanywa kuwa kugumu zaidi kwa sababu ya ukosefu wa nguvu za anga za Ukraine. Nchi za Magharibi zimeahidi ndege za kivita za F-16, lakini hazitawasili hadi baadaye mwaka huu

Nje kwenye handaki, mwanajeshi mwingine, Yaroslav, anaelezea: "Helikopta za Urusi, hushambulia eneo hilo kila siku". Amekatizwa huku mashambulizi mengine yakitua karibu. "Nenda kwenye makazi, ," anasema.

Wakati, tarehe 3 Juni, Rais Volodymyr Zelensky alipotangaza kwamba Ukraine ilikuwa tayari kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi, alitaja ubora wa anga wa Urusi na kuonya maisha ya watu wengi wa Ukraine yangepotea. Na ndivyo imekuwa kwa Brigedia ya 68.

Sgt Onistrat anasema hili linamlemea sana. "Ukali wa siku unategemea tu jambo moja - idadi ya watu tunaowapoteza. Wiki iliyopita imekuwa ngumu sana. Tumepoteza idadi kubwa ya wanajeshi."

Kichwani amevaa kofia ya mpira, saizi ndogo sana. Ninamtajia anaanza kulia. "Ilikuwa ya mwanangu," anasema.

Ostap Onistrat, 21, aliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani karibu na mahali tunapozungumza, siku chache kabla ya kuanza kwa mashambulizi hayo. Amekuwa jeshini kwa mwaka mmoja.

Baba yake bado yuko kwenye lindi la huzuni. "Ndege isiyo na rubani ya kamikaze iliruka hadi kwao na kwa kweli ikampiga moja kwa moja. Haikuwezekana kumtambua. Alizikwa kwenye jeneza lililofungwa," Sgt Onistrat anasema.

Anaendeleaje, nauliza. “Nilijitolea, unajua tupo kwa ajili ya kushinda, si kukaa kitako, si kutoroka, nafikiri kila mtu hapa lazima afanye kazi yake kwa weledi, hakuna kitu cha kishujaa, lazima nimalize tu kazi hii."

Ninapouliza kama anatafuta kulipiza kisasi, ananijibu kwa uthabiti: “Kulipiza kisasi ni dhambi.

"Kazi yangu ni kumaliza kazi hii. Nataka kushiriki katika gwaride la ushindi. Nataka tushinde, na ninataka kupoteza watu wachache."

Tunaondoka katika mstari wa mbele, mashambulizi bado yakiendelea . Baadaye, nilipokea ujumbe ukiniambia wamechukua maeneo yaliokaliwa na Urusi.

Tukirudi kwenye kambi ya amri, gari la Sgt Onistrat linalotusindikiza linachepuka na kusimama ghafla. Yeye, pamoja na wengine, haraka wanatoka kwenye gari. Nashangaa kama sisi pia tunahitaji kujificha.

Kisha naona kile ambacho kiliwavutia - miti ya zabibu.

Kama watoto, wanacheka bila kujali kwa muda huku wakinyakua tunda jekundu jeusi kutoka kwenye matawi yenye kivuli, huku mizinga na milio ya risasi ikiendelea kushambulia maeneo ya Warusi kwenye mlima.