Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Taiwan: China haikaribii kufanya mashambulizi , lakini Marekani inaitazama kwa karibu, Jenerali Milley
Shambulio lolote la China dhidi ya Taiwan halijakaribia, jenerali mkuu wa Marekani anasema, lakini akaongozea kwamba taifa lake linaiangalii kwa ukaribu mkubwa China
China ni wazi inakuza uwezo wa kushambulia wakati fulani, lakini kuamua kufanya hivyo itakuwa chaguo la kisiasa, Jenerali Mark Milley aliiambia BBC.
Uchina inasema Taiwan ni mkoa uliojitenga ambao lazima uunganishwe tena na bara, kwa nguvu ikiwa ni lazima.
Imeishutumu Marekani kwa kuunga mkono uhuru wa Taiwan, na kuapa "kuvunja kwa uthabiti" jaribio lolote kama hilo.
Kumekuwa na ongezeko kubwa hivi karibuni la mzozo kati ya China na Marekani - mshirika mwenye nguvu zaidi wa Taiwan.
China imekuwa ikituma ndege nyingi za kivita katika eneo la ulinzi wa anga la Taiwan, huku Marekani ikituma meli za wanamaji kupitia maji ya Taiwan.
Mwezi Mei, Rais wa Marekani Joe Biden alisema China ilikuwa "ikifanya hatari " kwa kurusha ndege zake za kivita karibu na Taiwan. Aliapa kukilinda kisiwa hicho kijeshi iwapo kitashambuliwa.
Beijing ilijibu kwa kuishutumu Marekani kwa "kukiuka ahadi yake kwa Taiwan" na "kuingilia" masuala ya China, na kuongeza kuwa nchi hiyo "haitasita kupigana" ili kuzuia Taiwan kutangaza uhuru rasmi.
'Tunaitazama [China] kwa karibu sana'
Alipoulizwa iwapo alifikiri China ingeshambulia Taiwan, Jenerali Milley, mwenyekiti wa wakuu wa pamoja wa wafanyakazi wa Marekani, aliambia BBC:
"Inaweza, inapaswa, ingekuwa, hayo ni maneno muhimu hapo.
"Katika suala la uwezo, nadhani China inaendeleza uwezo wake. Rais Xi [Jinping] ametaja hilo kwenye majukwaa ya hadhara, alilitaja kwenye hotuba, kwamba ametoa changamoto kwa PLA [Jeshi la Ukombozi la Watu wa China] kukuza uwezo wa kushambulia. Taiwan wakati fulani.
"Na ikiwa wangefanya au la, ni chaguo la kisiasa, ni chaguo la sera, ambalo litatokana na jinsi Wachina wanavyoona faida ya hatari ya gharama wakati huo."
"Hakuna dalili au maonyo ya kitu chochote kinachokaribia kwa wakati huu. Lakini tena, tunaitazama kwa karibu sana," Jenerali Milley aliongeza.
Marekani haina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Taiwan, lakini inaiuzia silaha kama sehemu ya Sheria yake ya Mahusiano ya Taiwan, ambayo inasema kwamba Marekani lazima ipatie kisiwa hicho njia ya kujilinda.
Wakati huo huo, inadumisha uhusiano rasmi na China na pia kidiplomasia inakubali msimamo wa China kwamba kuna serikali moja tu ya China.
China inaliona shambulio hilo kuwa la gharama kubwa
Uchambuzi wa Tessa Wong, mwandishi wa BBC, Singapore
Hofu moja kuu ni kwamba vita vitaanzishwa iwapo China itaivamia Taiwan. Beijing imesema siku za nyuma inaweza kurudisha kisiwa hicho kwa nguvu ikiwa ni lazima.
Lakini wachambuzi wengi wanasema hii haiwezekani - kwa sasa.
Kumekuwa na mjadala juu ya kama China ina uwezo wa kijeshi kufanikiwa katika uvamizi, na Taiwan imekuwa ikiimarisha ulinzi wake wa anga na baharini.
Lakini wengi wanakubali kwamba Beijing inatambua kuwa hatua kama hiyo itakuwa ya gharama kubwa na mbaya - sio tu kwa Uchina, bali pia kwa ulimwengu.
Msimamo thabiti wa China umekuwa kwamba inatafuta "kuungana tena kwa amani" na Taiwan - na kwamba ingechukua hatua tu ikiwa inakabiliwa na uchochezi.
Kichochezi kimoja kinaweza kuwa Taiwan kutangaza uhuru rasmi. Lakini hili ni jambo ambalo Rais wake Tsai Ing-wen ameepuka , licha ya kusisitiza kuwa tayari ni nchi huru.
WaTaiwani wengi wanaunga mkono msimamo huu, ambao unajulikana kama "kudumisha hali ilivyo", ingawa idadi ndogo inazidi kusema wanataka kuelekea uhuru.
Vile vile, Marekani itasita kujiingiza katika mgogoro wa gharama kubwa ya kijeshi bara Asia, na imetoa ishara mara kwa mara kwamba haitaki vita.
China na Taiwan: Misingi
- Kwa nini China na Taiwan zina uhusiano mbaya? China na Taiwan ziligawanyika wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1940, lakini Beijing inasisitiza kuwa kisiwa hicho kitarudishwa wakati fulani, kwa nguvu ikiwa ni lazima.
- Taiwan inatawaliwa vipi? Kisiwa hicho kina katiba yake, viongozi waliochaguliwa kidemokrasia, na takriban wanajeshi 300,000 wanaofanya kazi katika vikosi vyake vya jeshi.
- Nani anaitambua Taiwan? Ni nchi chache tu zinazoitambua Taiwan. Wengi wanaitambua serikali ya China iliyoko Beijing badala yake. Marekani haina uhusiano rasmi na Taiwan lakini ina sheria inayoitaka kukipa kisiwa hicho mbinu za kujilinda.