Jinsi muziki wa hip-hop ulivyochangia niwe Muislamu

Chanzo cha picha, ISMAEL LEA SOUTH
Ingawa watu wengi watakuambia kuhusu muziki unaowavutia, kwa Ismael Lea South muziki ulibadilisha mtindo wake wa maisha.
South alizaliwa Willesden, kaskazini-magharibi mwa London Mei 1973, na alitambulishwa kwa muziki wa hip-hop tangu umri mdogo alipokuwa akisoma katika Shule ya Upili ya South Kilburn.
"Shule yetu ilikuwa na utamaduni mkubwa wa Kiafrika na Afro-Caribbean. Tulikuwa tunasikiliza watu kama Big Daddy Kane, A Tribe Called Quest, Public Enemy, Eric B & Rakim," alikiambia kipindi cha Jumapili cha BBC Radio 4.

Chanzo cha picha, ISMAEL LEE SOUTH
Ingawa anakiri mwanzoni "Kutikisa kichwa kwa mpigp wa muziki", Ismael baadaye alianza kuona zaidi kile ambacho wasanii anaowapenda walikuwa wakisema.
"Huu ulikuwa wakati ambapo wasanii wengi wa rap walikuwa wakitumia misemo ya Kiarabu, na hawakuwa Waislamu, kwa hiyo wangesema mambo kama 'Inshallah' [yakimaanisha Mungu akikubali]."
Pia alianza kulipa kipaumbele wanamuziki waliotilia maanani zaidi muziki wao.
"Kungekuwa na wanamuziki ambao wangerap kuhusu jinsi walivyoanza kutazama maisha kwa undani zaidi na wangerap kuhusu hali ya kiroho," Ismael anaelezea.

Chanzo cha picha, ISMAEL LEE SOUTH
Mfano anaoutoa ni wa hip-hop wa mwaka 1987 wa Eric B & Rakim, ambamo Rakim "alikuwa akisema alikuwa mvulana mtukutu lakini akajifunza hiyo haikuwa njia ya kuishi na sasa anataka kupata kazi.
"Nilikuwa nikifikiria ni nini kilimfanya abadilike kutoka kuwa hivyo na kupata kazi na alikuwa akitaja tungo za Kiislamu, hivyo kunifanya nifikirie," anasema.
Kipindi kikubwa kilichofuata kwa Ishmael kilikuwa pale alipoalikwa na rafiki yake kutembelea Speaker's Corner katikati mwa London ambapo kundi la Cash Crew lilikuwa likitumbuiza wakiwa kwenye ziara.
"Kwa hiyo tulikwenda Hyde Park Corner bila kujua Hyde Park Corner ni nini na nilivutiwa. Niliona Wakristo, Waislamu, Wayahudi, wasoshalisti, wasioamini kwamba Mungu hayuko, wakijadiliana na nikafikiri 'oh eneo hili ni zuri'."

Chanzo cha picha, ISMAEL LEE SOUTH
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Akiwa huko, pia alikutana na mzungumzaji mwingine anayeitwa Muhammad Khaja ambaye angekuwa na athari kubwa kwa mustakabali wake.
"Alikuwa utamaduni sawa na mimi, Afro-Caribbean, alikuwa amevaa mavazi ya Kiislamu ya Kiafrika na, alipokuwa akizungumza na kujadili, hakuna mtu aliyeweza kushindana naye.
“Nilianza kumuuliza kuhusu Uislamu, nikasema ‘kuna mambo fulani sikubaliani kabisa na uidlamu,” anasema.
Miezi sita baadaye, Ismael alipigiwa simu na rafiki yake ambaye alipendekeza watembelee msikiti. Akiwa huko, alikutana tena na Muhammad Khaja.
"Alisema, 'Hujambo, unanikumbuka? Nataka kuzungumza nawe zaidi kuhusu Uislamu', na kisha kutoka hapo nikaanza kujifunza na kujifunza."
Ingawa mwanzoni alikuwa na mashaka juu ya kuwa Mwislamu, "kwani alitaka kujifurahisha akiwa mdogo", hatimaye aliamua kuwa tayari kusilimu.
"Na hivyo ndivyo nilivyosilimu."
Lakini ingawa muziki wa hip-hop ulikuwa imemsaidia kuwa Mwislamu, bado iichukua muda kwa familia yake, ambao walikuwa Wakristo, kukubali maisha haya mapya.
"Nilipoukubali Uislamu niliacha kunywa pombe, niliacha kula nyama ya nguruwe, niliacha kwenda karamu - familia yangu ilifikiri nimepata wazimu," anasema.
"Lakini nilipomwambia mama yangu nataka kutulia na nioe, mama yangu aliposikia alisema, 'oh, sawa'.
"Sababu ya hiyo alishawishika."














