Mchipuko, wasanii na historia ya miaka arobaini ya muziki wa Hip Hop. Nini kimebadilika?
Maelezo ya picha, Che Kothari, ambaye pia ni mpiga picha na mchoraji, azindua picha zake kuonyesha chimbuko la Hip Hop na hali ya muziki huo miaka 40 baadaye. Ni katika maonyesho kuhusu utamaduni wa Hip Hop na waanzilishi wa muziki huo. Huyu hapa ni LL Cool J
Maelezo ya picha, Kothari pamoja na Ryan Paterson wamekuwa wakikusanya picha za wasanii ambao wamekuwa muhimu katika kuchipuka kwa muziki wa Hip Hop. Hii ni picha yake marehemu Christopher Wallace maarufu kama Notorius BIG au Biggie Smalls kama alivyojulikana kwa mashabiki wake.
Maelezo ya picha, Kothari pia aliweza kuwapiga picha wasanii kama vile Ice Cube, Chuck D, Afrika Bambaataa, Erykah Badu na Nas aliye kwenye picha hii.
Maelezo ya picha, Kothari anasema , katika maonyeso haya sio nia yake kuonyesha ambavyo muziki ulichipuka hatua kwa hatua ni wasanii tu maarufu ambao wanasifika kwenye muziki huu ambao wameupa sifa yake. Pia maonyesho yanalenga kusherehekea mkusanyiko wa picha za wasanii hao maarufu wa Hip Hop.
Maelezo ya picha, Kutoka kwa wasanii waliosifika na waliochipukia katika maisha hatari ya mitaani hadi kwa mavazi yao , umaarufu wao na mafanikio yao, maonyesho yanaweza wazi muziki wa Hip Hop ulivyokuwa.
Maelezo ya picha, Katika kipindi cha miaka 40 iliyopita, wanamuziki kama vile, Pubic Eenemy, De la Soul na Jay Z wamewa mashuhuri kweli kweli.Marehemu Tupac Shakur, bado yuko vinywani na akilini mwa wengi tangu kutokea kifo chake.
Maelezo ya picha, Dr Dre, mshindi wa tuzo ya Grammy amewatengezea nyimbo wanamuziki kama vile Eve, Mary J Blige na Snoop Dogg. Pia ameshuhudia kukuwa kwa muziki huo na kujionea wanamuziki wa kizazi kipya wakichipuka akiwemo Aminem na 50 Cent.
Maelezo ya picha, Pharrell Williams hapa alipigwa picha na Steve Carty, anajulikana tu kwa kifupi kama Pharrel. Ni muimbaji na mtengezaji wa mitindo ya kila aina. Amepata tuzo nyingi tu ikiwemo tuzo ya wimbo bora zaidi.
Maelezo ya picha, Miaka arobaini ya Hip Hop.Maonyeso yatakayoendelea hadi tareye 31 Mei mjini Toronto Canada.