"Niliishia hospitalini kwa sababu ya kope bandia"

Chanzo cha picha, Getty Images
Akiwa mpenzi mkubwa wa kuongeza kope kwa karibu mwaka mzima, muuguzi wa Brazili Valéria Campos hakuwahi kufikiria kwamba angeweza kupata aina fulani ya mzio wakati wa kufanya upasuaji.
Hata hivyo, miezi minne baada ya kudumu na kope bandia - aliporudi saluni kuweka kope zingine baada ya zile za awali kuonekana kuanguka muda unavyokwenda - aligundua kuwa kuna kitu hakiko sawa.
Muuguzi huyo anaripoti kwamba saa tatu baada ya zoezi hilo, jicho lake likaanza kuwa jekundu, kuvimba, na kupata maumivu. "Mtaalamu huyo alitumia njia zile zile ambazo tayari nilikuwa nimezizoea. Lakini kadiri saa zilivyopita, jicho langu lilivimba na kuumia zaidi na zaidi," anakumbuka Valéria.
Kwa kuwa ilikuwa Jumamosi usiku, ilimbidi asubiri hadi asubuhi ili arudi saluni ili kuziondoa kope zake zake bandia.
Baada ya kuziondoa, alienda kwenye chumba cha dharura cha hospitali ya Belo Horizonte, Brazili, ambako alipewa rufaa ya kupata huduma ya dharura ya macho.

Chanzo cha picha, PERSONAL FILE
"Kwa kweli sikuweza kulala usiku huo, ilikuwa saa 3 asubuhi nilipoamka na sikuweza kufungua macho yangu tena. Kwa mujibu wa daktari, nilikuwa na maambukizi, lakini sikujua kama yalitokana na kope za 'syntetisk' au gundi iliyotumiwa." Aliongeza.
li kupona kabisa kutokana na maambukizi, Valéria alihitaji antibiotics kwa siku saba. Ingawa tatizo hilo halikuathiri uwezo wake wa kuona hata kidogo, anasema kope zake za asili hazikua tena au kuwa na wingi uliokuwa nao kabla ya kuongezwa muda. "Idadi ya kope nilizonazo zimepungua kwa sababu nilikuwa na nywele nyingi za asili," anahitimisha.
Nyuzi ama kope bandia za syntetisk
Katika kuboresha urembo wake, Mwanafunzi wa saikolojia Adne Lucilla Carvalho Santos aliamua kuweka kope bandia za nyuzi za syntetisk kwa mara ya kwanza mnamo Julai.
'Jambo ambalo sikutarajia ni kwamba ningepatwa na mzio'.
Dakika chache baada ya kumaliza kuweka, mwanafunzi wa chuo kikuu anakumbuka kwamba alianza kuhisi usumbufu machoni pake. Dalili za kwanza za maambukizi ni uwekundu na na macho kama kuchomachoma.

Chanzo cha picha, Pesronal file
Kope bandia na hatari zake
Zoezi la kuongeza ama kuweka kope bandia ni zaidi ya kubandika nyuzi za synthetic au hariri kwa kila kope ya asili, na kuifanya kuonekana ndefu na inayopendeza.
Kwa aina hii ya utaratibu gundi maalum hutumiwa. "Ikiwezekana, fanya uchunguzi wa dutu au gundi itakayotumika kuuunganisha (kope bandia na asili)", anaelezea daktari Ediléia Bagatin, mratibu wa Idara ya Dermatological Cosmiatry ya Brazilian Society of Dermatolojia.
"Kipimo hiki kwa ujumla kinatumika kwa eneo la ndani ya mkono na si kwa jicho. Ikiwa baada ya siku tatu hakuna athari ya mzio, mtu anaweza kufanya hivyo kwa usalama zaidi," anaongeza.

Chanzo cha picha, personal file
Ingawa inaonekana kuwa haina madhara, matumizi ya muda mrefu ya kuweka kope bandia, ukosefu wa usafishaji sahihi na utunzaji wake unaweza kusababisha shida mbali mbali, kuanzia upotezaji wa asili wa nywele zinazolinda macho, kuacha (macho) wazi na bila kinga, hadi kusababisha magonjwa makubwa zaidi kama vile vidonda .
"Kope zina kazi ya kulinda macho dhidi ya mwanga, vumbi na vitu vingine. Matatizo ya kawaida yanayohusiana na upanuzi wa kope ni blepharitis, ikifuatiwa na kiwambo cha mzio, vidonda vya konea, kupoteza au kunyonyoka kwa kope za asili," anaeleza Claudia Del Claro, daktari wa macho ambaye ni mwanachama wa bodi ya Jumuiya ya Brazili ya Ophthalmology.














