Fahamu lenzi za kisasa zinazoweza kutoa data mbele ya macho ya mtumiaji

Mojo lens

Chanzo cha picha, MOjo

Maelezo ya picha, Makampuni yanatengeneza lenzi za kisasa zinazoweza kutoa data mbele ya macho ya mtumiaji.
Iliyochapishwa

Lensi za kisasa zinazotumia teknolojia ya juu zinatoa matumaini ya kuleta data moja kwa moja kwenye eneo lako unaloona.

Fikiria kuwa lazima utoe hotuba, lakini badala ya kutazama chini kwenye maandishi yako, maneno yanasogea mbele ya macho yako, popote pale macho yako yatakapoelekea.

Hiyo ni moja tu ya mambo mengi ambayo wahudumu wa bidhaa ya smart wanaangazia na kuahidi kuwa lenzi za namna hii zenye umahiri wa hali ya juu katika mawasiliano zitapatikana katika siku zijazo.

''Fikiria... wewe ni mwanamuziki na maneno yako, au sauti za muziki mbele ya macho yako. Au wewe ni mwanariadha na una kifaa chako cha kidijitali mbele yako na unaweza kuona umbali wako na taarifa nyingine unazohitaji,'' anasema Steve Sinclair kutoka kampuni ya Mojo, ambayo inatengeneza lenzi za kisasa zitakazowezesha mawasiliano.

Kampuni yake inakaribia kuanza majaribio ya kina ya lenzi za kisasa kwa wanadamu, ambayo yatampa mvaaji onyesho la juu ambalo linaonekana kuelekea mbele ya macho yao.

Illustration of how Mojo data might look

Chanzo cha picha, MOjo

Maelezo ya picha, Lenzi za kisasa zinaweza kukupa taarifa muhimu

Lenzi ya 'scleral' (lenzi kubwa zaidi inayoenea hadi kwenye weupe wa jicho) hurekebisha uwezo wa kuona wa mtumiaji, lakini pia inajumuisha onyesho ndogo la LED, vitambuzi mahiri na betri thabiti.

''Tumeunda kile tunachokiita kielelezo-kamili ambacho kinafanya kazi na kinaweza kuvaliwa - hivi karibuni tutafanya majaribio ya ndani,'' anasema Bw Sinclair.

"Sasa inakuja sehemu ya kuvutia, ambapo tunaanza kufanya uboreshaji wa utendaji, na kuivaa kwa muda mrefu ili kudhibitisha kuwa tunaweza kuivaa siku nzima."

Presentational grey line

Lenzi zingine za kisasa zinatengenezwa ili kukusanya data ya afya.

Lenzi zinaweza ''kujumuisha uwezo wa kujichunguza na kufuatilia shinikizo la ndani ya macho, au glukosi,'' anasema Rebecca Rojas, mwalimu wa sayansi ya macho katika Chuo Kikuu cha Columbia.

Viwango vya sukari kwa mfano, vinahitaji kufuatiliwa kwa karibu na watu wenye ugonjwa wa sukari.

''Wanaweza pia kutoa chaguzi za utoaji wa dawa, ambayo ni ya manufaa katika uchunguzi na mipango ya matibabu. Inafurahisha kuona teknolojia ilipofika, na uwezo unaotoa kuboresha maisha ya wagonjwa.''

Utafiti unaendelea ili kuunda lenzi zinazoweza kutambua na kutibu hali ya matibabu kuanzia hali ya macho, kisukari, au hata saratani kwa kufuatilia vialama fulani kama vile viwango vya mwanga, molekuli zinazohusiana na saratani au kiasi cha glukosi kwenye machozi.

Timu katika Chuo Kikuu cha Surrey, kwa mfano, imeunda lenzi za kisasa zenye kuwezesha mawasiliano ambayo ina kitambua picha kwa ajili ya kupokea taarifa za macho, kihisi joto cha kutambua uwezekano wa ugonjwa wa konea na kitambuzi cha glukosi kinachofuatilia viwango vya glukosi kwenye kiowevu cha machozi.

University of Surrey lens with detector

Chanzo cha picha, University of Surrey

Maelezo ya picha, Lenzi iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Surrey inaweza kufuatilia afya ya mvaaji

''Tunaifanya kuwa tambarare, yenye safu nyembamba sana ya matundu, na tunaweza kuweka safu ya kihisia moja kwa moja kwenye lenzi ili iguse jicho moja kwa moja na ina mawasialiano na chanzo cha machozi,'' anasema Yunlong Zhao, mhadhiri wa uhifadhi wa nishati na bioelectronics katika Chuo Kikuu cha Surrey.

''Utajisikia kama ni vizuri zaidi kuvaa kwa sababu ni rahisi zaidi, na kwa sababu kuna kuwasiliana moja kwa moja na chanzo cha machozi na kuweza kutoa matokeo sahihi zaidi ya kuhisia,'' anasema Dk Zhao.

Licha ya msisimko, teknolojia ya lenzi hii bado inapaswa kushinda changamoto kadhaa.

Changamoto moja itakuwa kuhakikisha lenzi zina moto kwa kutumia betri na bila shaka zitalazimika kuwa ndogo sana, kwa hivyo zitatoa nguvu ya kutosha kufanya chochote muhimu?

Kampuni ya Mojo bado inajaribu bidhaa yake, lakini inataka wateja waweze kuvaa lenzi zake siku nzima, bila kuzichaji tena.

''Matarajio [ni] kwamba hutumii taarifa kutoka kwa lenzi kila mara lakini kwa muda mfupi siku nzima. ''Uhai halisi wa betri utategemea jinsi na mara ngapi inatumiwa, kama vile simu ya mkononi au saa yako ya dijitali hii leo,'' msemaji wa kampuni anaeleza.

A woman wears Google Glass at book presentation

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Google Glass - iliyozinduliwa mwaka wa 2014 - haikufanikiwa

Wasiwasi mwingine juu ya faragha umekuwepo tangu Google ilipozindua miwani yake mahiri mnamo mwaka 2014, ambayo ilionekana kote kuwa haikufaulu kutimiza lengo lililokusudiwa.

''Kifaa chochote chenye busara chenye kamera inayotazama mbele inayomruhusu mtumiaji kupiga picha, au kurekodi video, huhatarisha faragha kwa sababu ya watazamaji,'' anasema Daniel Leufer, Mchambuzi mkuu wa sera katika kikundi cha kampeni ya haki za kidijitali, Fikia Sasa.

''Kwa miwani ya kisasa, kuna angalau wigo fulani wa kutoa ishara kwa watazamaji wakati wanarekodi - kwa mfano, taa nyekundu za onyo - lakini kwa lenzi hizi za kisasa ni ngumu zaidi kuona jinsi ya kuunganisha kipengele kama hicho.''

Kando na wasiwasi wa faragha, waundaji pia watakuwa na wasiwasi juu ya usalama wa data kwa watu wanaovaa lenzi.

Lenzi za kisasa zinaweza tu kutimiza utendakazi wao ikiwa zitafuatilia mienendo ya macho ya mtumiaji, na data hii pamoja na nyingine inaweza kufichua mengi.

''Itakuwaje ikiwa vifaa hivi vitakusanya na kushiriki data kuhusu kile ninachotazama, muda gani ninachokitazama, iwe mapigo ya moyo wangu yanaongezeka ninapomtazama mtu fulani, au ni kiasi gani ninatokwa na jasho ninapoulizwa swali fulani?&,'' anasema Bw Leufer.

''Aina hii ya data ya karibu inaweza kutumika kufanya makisio yenye matatizo kuhusu kila kitu kutoka kwa mwelekeo wetu wa kijinsia hadi kama tunasema ukweli kwa kuhojiwa,'' anaongeza.

''Wasiwasi wangu ni kwamba vifaa kama vile glasi za AR (uhalisia uliodhabitiwa), au lenzi a kisasa za mawasiliano, vitaonekana kama hifadhi inayoweza kuwa data ya karibu.''

Kwa upande wake, kampuni ya Mojo inasema data zote zinalindwa na kuwekwa faragha.

Mojo expanded lens view

Chanzo cha picha, MOJO

Maelezo ya picha, Lenzi ya kisasa ya Mojo hujumuisha skrini ndogo

Zaidi ya hayo kuna wasiwasi kuhusu bidhaa ambayo itajulikana kwa mtu yeyote anayevaa lenzi ya kawaida.

''Aina yoyote ya lenzi ya kisasa inaweza kuhatarisha afya ya macho, isipotunzwa ipasavyo au kutowekwa ipasavyo machoni.

''Kama vile kifaa kingine chochote cha matibabu, tunahitaji kuhakikisha afya ya wagonjwa ndiyo kipaumbele, na kifaa chochote kinachotumiwa kinapewa kipaumbele, manufaa ambayo yanazidi hatari,'' asema Bi Rojas, kutoka Chuo Kikuu cha Columbia.

''Nina wasiwasi kuhusu kutofuata sheria, au ukosefu wa usafi wa lenzi na kuvaa kupita kiasi.

Haya yanaweza kusababisha matatizo zaidi kama vile kuwasha, kuvimba, maambukizo au hatari kwa afya ya macho.

Rebecca Rojas, instructor of optometric science at Columbia University

Chanzo cha picha, Columbia University

Maelezo ya picha, Kama lenzi zozote zile, lenzi za kisasa zitahitajika kutumiwa kwa uangalifu, anasema Rebecca Rojas

Huku lenzi za Mojo zikitarajiwa kutumika kwa hadi mwaka mmoja kwa wakati mmoja, Bw Sinclair anakiri hili ni jambo la kutia wasiwasi.

Lakini anadokeza kuwa lenzi ya kisasa inamaanisha inaweza kuratibiwa kutambua ikiwa inasafishwa vya kutosha na hata kuwatahadharisha watumiaji inapohitaji kubadilishwa.

Kampuni pia inapanga kufanya kazi na madaktari wa macho kwa maagizo na ufuatiliaji.

''Huwezi tu kuzindua kitu kama lenzi ya kisasa na kutarajia kila mtu ataitumia siku ya kwanza,'' asema Bw Sinclair.

''Itachukua muda, kama bidhaa zote mpya za watumiaji, lakini tunafikiri ni jambo lisiloepukika kwamba bidhaa zetu zote za macho hatimaye zitakuwa za kisasa.''