Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fainali ya Kombe la FA: Man City imeweka kiwango cha juu, Je Man United itawafikia? - Alan Shearer
Manchester City wamepandisha viwango kwa sasa na vitalazimu klabu ya Manchester United - na wengine – kufikia viwango hivyo.
Kwa sasa, pengo kati ya City na kikosi cha Erik ten Hag ni kubwa sana. Walifanya vyema kwa kupachika bao 1-0 kwenye fainali ya Kombe la FA Jumamosi na kisha kurejea mchezoni na kusawazisha, lakini timu bora bila shaka ilishinda mwishowe.
City walikuwa na uwezo wa kumiliki mpira zaidi, nafasi nzuri zaidi na wachezaji bora. Walistahili kabisa ushindi wao wa 2-1 ugani Wembley na tofauti yao ya ushindi ingeweza na ingefaa kuwa kubwa zaidi ya hiyo.
Ndiyo, United waliwarushia kila kitu katika dakika chache za mwisho lakini, kwa sehemu kubwa ya mchezo, hawakuruhusiwa kufanya lolote kwa sababu ya jinsi City wanavyocheza.
Kikosi cha Pep Guardiola kitakupita hadi uchanganyikiwe pindi kinapomiliki mpira, ili ukirudishiwa mpira unakuwa umechoka. Lakini basi, kwa sekunde tano au sita za kwanza, wanashinikiza kwa nguvu hali ya kwamba kwamba ni vigumu sana kwa timu kuitumia furasa hiyo.
Hilo lilitokea Jumamosi na ilimaanisha kwamba hakuna washambuliaji wakubwa wa United kama Marcus Rashford, Casemiro, Christian Eriksen, Jadon Sancho na Bruno Fernandes aliyecheza vyema.
Badala yake, United ilitawaliwa - lakini sio kana kwamba wangeweza kufanya tofauti na wachezaji waliopata. Walipokuwa wakifuatilia mchezo, hawakuwa na kina au ubora wa kubadilisha mchezo, kwa bidii kama walivyojaribu.
Alejandro Garnacho aliongeza cheche kidogo alipoingia zikiwa zimesalia nusu saa lakini chaguo la Ten Hag lilionekana kuwa pungufu, hasa ikilinganishwa na wachezaji wa akiba wa City.
Wakati United walihitaji bao mwishoni, walikuwa na Wout Weghorst pekee wa kumtegemea katika benchi.
United wanahitaji kutumia pesa nyingi kushindana tena
Iwe ulikuwa ustadi wa hali ya juu kuifungua ngome ya City au uwezo wa kuiangamiza, United hawakuwa na uchawi waliohitaji kufanya hivyo.
Ilikuwa siku ya kutamausha kwao lakini kushindwa huku kusiondoe chochote kutokana na kile wamefanikiwa msimu huu - kushinda Kombe la Carabao na kumaliza nafasi ya tatu ili kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa bila shaka ni mafanikio.
Wamepiga hatua kubwa baada ya kupoteza mechi zao mbili za mwanzo za ligi msimu huu lakini pia ni dhahiri ni kazi kubwa iliyosalia kuifanya ili kufikia kiwango cha City.
Fainali ya Kombe la FA: Man Utd waliachilia mabao rahisi - Ten Hag
United ilimaliza kwa pointi 14 nyuma ya mabingwa hao wa ligi ya Uingereza . Kwa upande wa matokeo, walifanikiwa kuwasukuma City karibu kabisa na mchezo mmoja wa hapa na pale lakini hawajafikia kiwango cha kuwania ubingwa wa Ligi Kuu.
Wanahitaji kutumia pesa nyingi - ikiwa wanataka kuwa wagombea wakubwa tena. Nadhani labda wanahitaji kuleta washambuliaji wakubwa watatu au wanne ili hilo lifanyike.
Wanahitaji kutumia fedha vizuri pia, hatua ambayo haijawahi kutokea katika misimu ya hivi karibuni. Ten Hag alisema baada ya fainali ya Kombe hilo kuwa ana mpango wa kuboresha timu yake lakini anahitaji baadhi ya wachezaji wanaoendana na aina yake ya uchezaji.
Kuwasajili haitakuwa rahisi. Ni wazi inategemea ni kiasi gani United wamelazimika kutumia na hiyo inaathiriwa na kile kinachotokea na hali ya umiliki huko Old Trafford, ambayo inachanganya sana kwa sasa.
United wanahitaji nini?
Marcus Rashford anaelezea jinsi subra ndio 'ustadi mkubwa' kama mshambuliaji
Kwa hakika United wanahitaji mshambuliaji wa kati wa kiwango cha juu, ili tu kumpa presha Marcus Rashford, ambaye amekuwa na msimu mzuri, akiwa na mabao 30 katika michuano yote, lakini anahitaji usaidizi.
Bruno Fernandes ndiye mfungaji bora aliyefuata zaidi, akiwa na mabao 14, lakini ndiye mchezaji wao pekee aliyefikisha idadi hiyo mara mbili mnamo 2022-23. Weghorst, ambaye aliwasili Januari, alicheka na wavu mara mbili pekee.
Ni rahisi kusema wanapaswa kuvunja benki na kumleta Harry Kane kutatua tatizo hilo lakini hatujui kama huo ni uhamisho unaowezekana au la.
Lakini ikiwa Tottenham wako tayari kumuuza na Kane anataka kwenda huko, basi ndio, bila shaka atakuwa mmoja ambaye United inapaswa kumwangalia.
Pamoja na watu kama Declan Rice wa West Ham.
Hizo zinapaswa kuwa kiwango cha usajili ambao United inajaribu kuwaleta, ili kuwapeleka kwenye kiwango cha juu zaidi.
Ten Hag ana mengi ya kufikiria ingawa, kupitia upande wake.
Sijui kama kipa mpya ni kipaumbele lakini tuliona David de Gea akifanya kosa lingine kubwa huko Wembley - alipaswa kuokoa shambulio la bao la ushindi la Ilkay Gundogan.
Mimi si mtaalam wa makipa lakini nilikuwa nimekaa karibu na Peter Schmeichel, ambaye ni mmoja wa wachezaji bora zaidi, na akasema De Gea angepaswa kuizuia.
Kiwango cha De Gea hakikuwa cha kuridhisha sana msimu wote na ni mchezaji huru msimu wa joto lakini inaweza kuwa kwamba anapata mkataba mpya kwa sababu Ten Hag anaamua kuwa na nafasi nyingine ambazo zinahitaji kuimarishwa kwanza.
City wamebakiza mechi moja kushinda mataji matatu
Kwanza taji la Ligi Kuu, sasa Kombe la FA - linalofuata ni fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Wamesalia na mchezo mmoja kabla ya kushinda mataji matatu na klabu hiyo haitawahi kupata nafasi nzuri zaidi ya Jumamosi ijayo huko Istanbul kushinda Treble.
'Ilikuwa kipaji cha meneja' - Guardiola anatania na Lineker kuhusu nyota Gundogan
Hiyo ingeipa timu hii hadhi ya hadithi na kuwaweka kwenye orodha sawa na wavulana wa Manchester United mnamo 1999.
Nadhani watafanya hivyo pia - natarajia watakuwa wazuri sana kuwazidi Inter Milan.
City ina wachezaji wengi maalum lakini kiini cha yote, bila shaka, ni Guardiola. Akiwa huko, itakuwa vigumu kuwazuia.
Nimekuwa nikizungumza kuhusu jinsi United inaweza kujiimarisha lakini kuna uvumi kwamba City inaweza kupoteza nyota wake wawili msimu huu wa joto, huku mustakabali wa Gundogan na Bernardo Silva wote ukiwa shakani.
Ni wachezaji mahiri lakini hata wakienda wote wawili, sioni itawaumiza sana City msimu ujao.
Tayari wamekabiliana na kupoteza wachezaji kama David Silva, Sergio Aguero na Yaya Toure, na shida kwa United na kila mtu mwingine ni kwamba hatujaona tu timu hii ikibadilika chini ya Guardiola, wanaonekana kuendelea kuwa bora na bora.