Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Man Utd kumsajili Calvert-Lewin

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United iko katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 28, ambaye ni mchezaji huru baada ya kandarasi yake na klabu ya Everton kukamilika wiki hii. (Sun)
Juventus imeongeza juhudi za kumsajili winga wa Uingereza Jadon Sancho, 25, kutoka Manchester United na huenda ikamjumuisha na kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 27, katika dili hilo. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Juventus pia ina nia ya kumsajili kiungo wwa Mali Yves Bissouma mwenye umri wa miaka 28 kutoka Tottenham Hotspur msimu huu wa kiangazi. (La Gazzetta dello Sport - Kiitaliano)
Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 27, na Muingereza mwenzake, mshambuliaji wa Manchester City Jack Grealish, 29, huenda wakahama vilabu vyao kwa kima cha pauni milioni 40 tu kila mmoja msimu huu wa kiangazi. (Manchester Evening News)
Barcelona, hata hivyo, inatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester United siku zijazo kuhusu mpango wa kumsajili Rashford kwa mkopo na chaguo la hatimaye kumsajili kwa mkataba wa kudumu. (Footmercato - kwa Kifaransa)
Kocha wa Paris St-Germain Luis Enrique anasema "hana shaka" winga wa Ufaransa Bradley Barcola atasalia katika klabu hiyo, licha ya Bayern Munich kuonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images
Al-Nassr ya Saudia imefanya mazungumzo ya awali na mshambuliaji wa Real Madrid Rodrygo, 24, ambaye amekuwa akinyatiwa na vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia. (Sacha Tavolieri - kwa Kifaransa)
Mshambulizi wa zamani wa Italia Mario Balotelli, 34, anawaniwa na Ligi Kuu ya Soka ya Marekani na Liga MX baada ya kuondoka Genoa. (Sportsport)
Chelsea imeiambia Manchester United kuwa italazimika kulipa pauni milioni 35 iwapo inataka kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27. (Mirror).
Mshambulizi wa Korea Kusini Son Heung-min, 32, hana nia ya kuhamia Los Angeles FC licha ya kuwa tayari kuhama Tottenham msimu huu wa kiangazi. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Sunderland imepiga hatua katika mazungumzo yake na klabu ya Brugge kuhusu mpango wa kumsajili winga Chemsdine Talbi,20, ambaye ni mzaliwa wa Ubelgiji lakini ameamua kuiwakilisha Morocco. (Sky Sports)
Burnley na Leeds zinavutiwa na mshambuliaji wa Marekani na Norwich Josh Sargent, 25, huku ofa iliyowasilishwa na klabu ya Ujerumani Wolfsburg ikiwa chini ya thamani yake ya £16m. (Pink Un)
Klabu ya Brazil Flamengo imewasilisha dau la pauni milioni 5 kumsajili winga wa West Brom na Jamhuri ya Ireland Mikey Johnston, 26. (Express and Star).
Mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 27, yuko tayari kuhamia Arsenal badala ya klabu ya Saudi Pro. (Record- kwa Kireno)
Klabu ya Sporting iko tayari kwa mpango wa malipo wa Gyokeres baada ya kutaka euro 80m (£69m) hapo awali. (A Bola - kwa Kireno)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












