Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 25.07.2024

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Atletico Madrid "wana imani kubwa" kupata dili la kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Conor Gallagher, 24. (Team Talk)

Crystal Palace wanalenga kumnunua winga wa Marseille na Senegal Ismaila Sarr, 26. (Standard),

Inter Milan wanatumai kuwa harakati za Arsenal kumnunua mlinzi wa Bologna na Italia Riccardo Calafiori, 22, zitawalazimisha kumuuza mlinzi wa Poland Jakub Kiwior, 24. (Standard)

Manchester United wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Denmark mwenye umri wa miaka 25 Morten Hjulmand kutoka Sporting Lisbon. (FootballTransfers)

Chelsea wanakaribia kukamilisha dili la kumnunua mlinda mlango wa Villarreal na Denmark chini ya umri wa miaka 21, Filip Jorgensen, ambaye pia amevutiwa na Marseille. (Athletic – Subscription Required)

Chelsea wametoa ofa ya pauni milioni 17 pamoja na nyongeza kwa Jorgensen mwenye umri wa miaka 22 katika jitihada za kuimarisha chaguo lao la golikipa. (Mail)

Trent Alexander-Arnold, 25, anataka kusalia na Liverpool licha ya beki huyo wa pembeni wa Uingereza kuvutia Real Madrid. (Mail )

Rais wa Real Sociedad Jokin Aperribay amekanusha kuwa kuna mazungumzo yoyote yanayoendelea na Liverpool kuhusu uwezekano wa kumnunua winga wa Japan Takefusa Kubo, 23. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Newcastle wana hamu ya kutaka kumnunua beki wa AC Milan na Ujerumani Malick Thiaw, 22, kwa takriban pauni milioni 35. (Times – Subscription Required)

Fulham watatoa ofa iliyoboreshwa kwa mchezaji wa Arsenal Emile Smith Rowe. The Cottagers na Crystal Palace zote zimewasilisha ombi la kutaka kumnunua kiungo huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 23 lililokataliwa na The Gunners mwezi huu. (Sky Sports)

Leicester City wanashindana na West Ham kumnunua winga wa Arsenal mwenye umri wa miaka 24 Reiss Nelson. (Times – Subscription Required)

Arsenal wako tayari kusikiliza ofa za kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Eddie Nketiah, huku Marseille wakiibuka kama mahali pazuri pa kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Mirror)

Manchester United wanatazamiwa kuzidisha utafutaji wao wa beki wa pembeni huku mchezaji wa kimataifa wa Morocco na Bayern Munich Noussair Mazraoui, 26, akifikiriwa kuwa chaguo linalowezekana. (Telegraph)

Manchester United lazima isubiri kumuuza Aaron Wan-Bissaka kabla ya kumsajili beki wa pembeni badala yake, huku West Ham wakimtaka beki huyo wa Uingereza, 26. (Manchester Evening News)

Everton wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Napoli Jesper Lindstrom kwa mkopo. Mchezaji huyo wa Denmark mwenye umri wa miaka 24 atakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa katika klabu hiyo ya Premier League. (Liverpool Echo)

Nottingham Forest wamefanya mazungumzo na klabu ya Argentina ya Talleres kuhusu uwezekano wa kumsajili winga wa Paraguay mwenye umri wa miaka 24 Ramon Sosa. (Nottingham Post)

Beki wa Liverpool Mholanzi Sepp van den Berg anatarajiwa kuondoka Anfield msimu huu huku kukiwa na hamu kutoka kwa Hoffenheim na Mainz. (Florian Plettenberg)

Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla