Kombe la Dunia 2022: Uingereza itamenyana na Senegal katika hatua ya 16 bora - kila kitu unachohitaji kujua

Iliyochapishwa

England ilikata tiketi ya kukutana na mabingwa wa Afrika Senegal katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa 3-0 Jumanne dhidi ya Wales.

Haya ndiyo unayohitaji kujua kuhusu wapinzani wao - na ni njia gani kikosi cha Gareth Southgate kinaweza kuhitaji kushinda ili kubeba Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1966.

Je, England inacheza na nani baadaye?

Uingereza itamenyana na Senegal baada ya kufuzu kwa raundi ya mtoano wakiwa washindi wa Kundi B.

Senegal ilifuzu kutoka hatua ya makundi kwa mara ya pili pekee baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Ecuador mapema Jumanne, na kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Uholanzi katika Kundi A.

England itacheza lini tena?

 Mechi hiyo itafanyika Jumapili, Disemba 4 kwenye Uwanja wa Al Bayt nchini Qatar.

Uingereza itacheza saa ngapi Jumapili?

Mchezo wa timu ya England wa hatua ya 16 bora utaanza saa 19:00 GMT - 22:00 kwa saa za hapa Doha.

  Je, timu ya soka ya Senegal ni nzuri kiasi gani?

Senegal wameorodheshwa katika nafasi ya 18 duniani - wakiwa juu zaidi kuliko taifa lolote la Afrika - na walishinda Kombe lao la kwanza la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2021 baada ya kushindwa na washindi wa fainali 2019 na 2002.

Walifika robo-fainali ya Kombe la Dunia mwaka wa 2002 lakini hawakufuzu tena hadi 2018, walipotolewa katika hatua ya makundi kwa kushinda moja katika mechi tatu.

Watakosa wachezaji kadhaa muhimu dhidi ya England Jumapili, ingawa, kiungo wa Everton Idrissa Gueye akitumikia adhabu ya kutocheza mechi moja na fowadi wa Bayern Munich Sadio Mane aliondolewa kwenye dimba kwa sababu ya jeraha.

Je, Uingereza na Senegal zilikutana hapo awali?

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa pande hizo mbili kucheza.

Senegal iko wapi?

Senegal iko Afrika Magharibi, karibu na Bahari ya Atlantiki.

Je, England itacheza na nani ikiwa itaifunga Senegal?

England inakabiliwa na njia inayoweza kuwa ngumu kuelekea fainali huku mechi ya robo fainali ikiwa na washindi wa Kundi D - Ufaransa - au washindi wa pili wa Kundi C - Poland - wakisubiri.

Mechi hiyo itafanyika Jumamosi, Disemba 10 na nusu fainali itachezwa siku nne baadaye, Jumatano, 14 Desemba.

Croatia, washindi wa pili 2018, ni miongoni mwa wale ambao England inaweza kukutana nao, pamoja na Ureno ya Cristiano Ronaldo.

Fainali itafanyika kwenye Uwanja wa Lusail nchini Qatar tarehe 18 Desemba. Wapinzani wanaowezekana wanaweza kuwa Uholanzi, Poland, Uhispania au Brazil, ambazo zote ziko upande tofauti wa droo.