Unajua kwanini zaidi ya simu za mkononi bilioni tano kutupwa mwaka huu?

E-waste

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Mwaka huu, simu za rununu au mkononi bilioni 5.3 zinatarajiwa kutupwa,kwa mujibu wa Mamlaka ya kimataifa inayosimamia vifaa vya umeme na kielektroniki (WEEE).

Inaelezwa, kwa mujibu wa takiwmu kimataifa, inaonyesha kuongezeka kwa tatizo la mazingira la "e-waste".

Watu wengi huhifadhi simu za zamani, badala ya kuzichakata ili kutumika, utafiti unasema.

Madini ya thamani ambayo hayajatolewa kutoka kwa taka za kielektroniki, kama vile shaba iliyo kwenye waya au kwenye betri zinazoweza kuchajiwa, lazima zichimbiwe.

"Watu huwa hawatambui kuwa vitu hivi vyote vinavyoonekana kuwa duni vina thamani kubwa na kwa pamoja katika kiwango cha kimataifa vinawakilisha idadi kubwa," mkurugenzi mkuu wa WEEE Pascal Leroy alisema.

Kuna wastani wa simu za mkononi bilioni 16 kote ulimwenguni - na huko Ulaya, karibu theluthi moja hazitumiki tena. WEEE inasema utafiti wake unaonyesha "mlima" wa taka za umeme na elektroniki - kutoka kwenye mashine za kufuliwa, kupikia hadi kompyuta na vifaa vya mfumo wa (GPS) - utakua hadi tani milioni 74 kwa mwaka ifikapo 2030.

E waste

Chanzo cha picha, Science Photo Library

Mapema mwaka huu, Royal Society of Chemistry ilizindua kampeni ya kukuza uchimbaji wa taka za kielektroniki ili kutoa bidhaa mpya, ikionyesha mzozo wa kimataifa, ikiwemo vita vya Ukraine, unatishia minyororo ya usambazaji wa vifaa vyenye madini ya thamani.

Magdalena Charytanowicz, wa WEEE, anasema: "Vifaa hivi vinatoa rasilimali nyingi muhimu ambazo zinaweza kutumika katika utengenezaji wa vifaa vipya vya elektroniki au vifaa vingine, kama vile betri za gari za umeme au paneli za jua (sola) - zote ni muhimu."

Zaidi ya asilimia 17 tu ya takataka za kielektroniki duniani zinarejelewa ipasavyo au kuchakatwa upya- lakini Umoja wa Kimataifa umeweka lengo la kuongeza kiwango hicho hadi kufikia asilimia 30% ifikapo mwaka ujao.

Inaangazia kuwa ni mojawapo ya "mikondo ya taka inayokua kwa kasi na ngumu zaidi ambayo huathiri afya ya binadamu na mazingira, kwani inaweza kuwa na vitu vyenye madhara".

Nchini Uingereza, zaidi ya bidhaa milioni 20 za umeme ambazo hazijatumika lakini zinazofanya kazi, zenye thamani ya kama £5.63bn, kwa sasa zimehifadhiwa katika nyumba za Uingereza, tafiti za shirika la Material Focus zinasema.

Pia ikakisia kwamb kaya moja Uingereza inaweza kuuza vifaa hivyo vya teknolojia visivyotumika na kujiupatia mpaka £200.