Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi msako wa silaha za siri za Iraq ulivyosambaratika
Miaka 20 baada ya uvamizi wa Iraq, bado kuna utata kuhusu uwepo wa "silaha za maangamizi" (WMDs) ambazo zilipatia Uingereza sababu ya kushiriki vita vya Iraq.
Taarifa mpya kuhusu msako wa silaha za maangamizi zimejitokeza kama sehemu ya msururu wa habari za BBC -Shock and War: Iraq miaka 20 baadaye, kwa misingi ya mazungumzo na makumi ya watu waliohusika moja kwa moja na msako huo.
"Mshituko." Hilo lilikuwa ni neno moja kutoka kwa afisa wa ngazi ya juu wa shirika la ujasusi la Uingereza alilomueleza mwenzangu mwishoni mwa mwaka 2001 alipokuwa akijibu kuhusiana na mtizamo wake kuhusu iwapo Wamarekani wanasema kweli wanaingia katika vita vya Iraq.
Maafisa wa shirika la ujasusi la Mareknani CIA pia wanakumbuka kushitushwa na wenzao wa Uingereza . "nilifikiri watakuwa na mshituko wa moyo pale pale mezani ," anakumbuka Luis Rueda, mkuu wa kikundi cha operesheni cha CIA nchini Iraq. "Kama wasingekuwa wanaume wenye haiba, wangevuka upande mwingine wa meza na kunipiga kofi ."
Habari ilifika haraka katika ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza Downing Street. Ujumbe huo ulifikishwa na wapelelezi badala ya wanadiplomasia.
"Nilikuwa labda mtu wa kwanza kumwambia waziri mkuu, ‘’Iwe unataka au usitake, unajumuika nao kwa sababu inaonekana ni kama wanajiandaa kwa ajili ya uvamizi," wakaTi ule aliyekuwa mkuu wa MI6, Sir Richard Dearlove, na ambaye alikuwa akifanya ziara za mara kwa mara mjini Washington, ameiambia BBC katika mahojiano ya nadra.
MI6 – ambayo ni taasisi ya huduma za ujasusi za uingereza katika nchi za kigeni – ilikuwa karibia inaingia katika mojawapo ya matukio ya kihistoria yenye utata na yenye athari kuwahi kushuhudia katika historia yake.
Kwa Marekani , suala la silaha za maangamizi (WMDs), lilikuwa ni suala la pili lililoifanya impindue kiongozi wa Iraq, Saddam Hussein. "Tungeivamia Iraq kama Saddam Hussein angekuwa na kipande cha karatasi au bangili ," anasema Bw Rueda. "Tungesema, 'Oh, atang’oa macho yako.'"
Kwa Uingereza, inapokuja katika kuiuza Iraq kwa umma , kama tisho ambalo linasababishwa na silaha za Iraq za maangamizi WMDs – silaha za kikemikali, za kibaiolojia - ilikuwa muhimu.
Kuna wakati ilidaiwa kuwa serikali ya Uingereza ilibuni madai kuhusu silaha za maangamizi - WMDs.Lakini mawaziri wakati ule walisema walikuwa wamehakikishiwa na majusi wao wenyewe kuwa silaha hizo zipo.
"Ni muhimu kusema kweli kuelewa ujasusi niliokuwa nikiupata ndio ambao niliokuwa nikiutegemea, na ninafikiri nilikuwa na wajibu wa kuutegemea ," waziri mkuu wa zamani Sir Tony Blair ananiambia. Siku moja kabla ya uvamizi alisema aliomba – na alipewa- hakikisho kutoka kwa Kamati ya pamoja ya ujasusi. Alikataa kukosoa huduma za ujasusi kwa kutokuwa sahihi.
Mawaziri wengine walisema kuwa walikuwa na mashaka wakati huo
"Mara tatu nilimhoji Richard Dearlove kuhusu usahihi wa ujasusi huu," anasema aliyekuwa wazir wa mambo ya nje wakati huo, Jack Straw. "Nilikuwa tu na hisia ambazo hazijatulia kuhusu uvamizi.
Lakini Dearlove alinihakikishia kila mara kwamaba hawa mawakala wa ujasusi walikuwa ni watu wa kutegemewa ." Hatahivyo, Bwana Straw anasema kwamba ni wajibu wa wanasiasa kuchukua jukumu , kwasababu wanachukua maamuzi ya mwisho.
Alipoulizwa iwapo anaona uvamizi wa Iraq kama kushindwa kwa ujasusi, jibu la Sir Richardh lilikuwa rahisi: "Hapana." Bado anaamini Iraq ilikuwa na aina fulani ya mpango wa silaha na mpangu huo huenda ulihamia kwenye mpaka wa Syria.
Wengine hawakubaliani na maoni ya Sr Richard "Ilikuwa ni kushindwa vibaya ," anasema Sir David Omand, ambaye wakati huo alikuwa mratibu wa usalama na ujasusi wa Uingereza . Anasema upendeleo wa serikali uliipelekea kuwasikiliza taarifa za wataalamu wachache ambao waliunga mkono fikra kwamba Saddam Hussein alikuwa na silaha za maangamizi-WMDs, na kupinga ushahidi ambao ulisema kuwa hana.
Baadhi ya viongozi wa ndani ya MI6 wanasema pia walikuwa na mashaka. "Wakati ule nilihisi kile tulichokuwa tunakifanya kilikuwa ni kosa," anasema afisa mmoja ambaye alifanya kazi katika uvamizi wa Iraq ambaye hajawahi kuzungumza kabla na aliomba asitajwe.
"Hapakuwa na taarifa mpya wala za kuaminika au tathmini ambavyo vilionyesha kwamba Iraq ilikuwa imeanza mipango ya silaha za maangamizi na kwamba walikuwa ni tisho kwa ulimwengNadhani kwa mtizamo wa serikali ni kitu pekee ambacho walipata cha kutumia …. Silaha za maangamizi-WMD lilikuwa ndio jambo pekee walilotumia kuhalalisha uvamizi wao kisheria ."
Mwandani mwingine katika shirika la ujasusi la Uingereza anakumbuka akipokea ujumbe unaosema "hapakuwa na kazi muhimu " kwa huduma za ujasusi zaidi ya kushawishui umma wa Waingereza juu ya hatua iliyochukuliwa. Walisema kwamba maswali yaliibuka kuhusu iwapo hili lilikuwa linafaa, na ujumbe ulifutwa.
Tarehe 12 Septemba, Sir Richard aliingia Downing Street na taarifa za chanzo kipya cha habari muhimu. Mtu huyu alidai mipango ya Saddam Hussein T ilikuwa imeanzishwa tena na kwamba angetoa taarifa mpya zaidi karibuni. Ingawa chanzo hiki hakikuchunguzwa kikamilifu , na taarifa zake hazikuwashirikisha wataalamu, taarifa zake ziliwasilishwa kwa waziri mkuu.
Kulikuwa na uwezekano wa baadhi ya vyanzo vipya vya habari vilikuwa vinabuni taarifa kwa ajili ya kupata pesa au kwasababu walitaka kuona Saddam amepinduliwa. Januari 2003, nilikutana na mtoro kutoka katika huduma za ujasusi za Saddam nchini Jordan. Alidai kuwa alihusika katika kutengeneza maabara zinazohamishwa za kufanya kazi katika silaha za kibaiolojia, mahala ambapo wakaguzi wa umoja wa mataifa hawawezi kufika.
Madai yake yaliweza kufika kwa waziri wa mambo ya kigeni wa Februari 2003, ingawa baadhi ndani ya serikali ya Marekani walikuwa tayari wamewasilisha "taarifa ya pingamizi", iliyosema kuwa taarifa ile ilikuwa sio ya kuaminika.
Chanzo kingine kilichokuwa na jina bandia "Curveball", ambaye Marekani na Uingereza walimtegemea , pia alikuwa anatbuni maelezo kuhusu maabara.
Ni muhimu kukumbuka kwamba Saddamwakati mmoja alikuwa na silaha za maangamizi. Wiki chache kabla ya vita vya mwaka 2003, nilitembelea kijiji cha Halabja kilichopo kaskazini mwa Northern Iraq, na kusikia wenyeji wakielezea siku amoja katika mwaka 1988 wakati jeshi la Saddam lilipowaangushia silaha ya kikemikali . Ukweli kuhusu kile kilichotokea kwa silaha hizo ulijulikana tu baada ya vita.
Saddam alikua ameagiza kuangamizwa kwa kiasi kikubwa cha mpango wake wa silaha za maangamizi WMD katika miaka ya mwanzoni mwa 1990 baada ya Vita vya kwanza vya Ghuba kwa matumaini ya kupata idhini ya wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa , mmoja wa wanasayansi wa ngazi ya juu wa Iraq aliniambia. Kiongozi wa Iraq huenda alitumai kuanza upya mipango ya silaha baadaye.
Lakini alikuwa ameharibu kila kitu kisiri , kwa upande mmoja alitaka kuendelea fikra kwamba huenda bado ana kitu fulani ambacho anaweza kukitumia dhidi ya Jirani yake Iran , ambaye alikuwa ndio amemaliza kupigana naye. Kwahiyo wakati Iraq baadaye ilipoulizwa na wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kuthibitisha iwapo ilikuwa imeangamiza kila kitu, haikufanya hivyo.
Kufikia mwaka 2002, wakaguzi wa Umpja wa mataifa walirejea Iraq kusaka silaha za maangamizi. Baadhi ya wakaguzi hao, wakizungumza na BBC kwa mara ya kwanza wanaweza kukumbuka wakitazama katika maeneo ambayo majasusi walionyesha kutoka Magharibi wakisema huenda kulikuwa na maabara zinazoweza kuhamishwa za za silaha za maangamizi. Walipata kile ambacho mmoja wao anakiita "Lori la matamgazo ya kuuza ice cream " lililokuwa lime funikwa na utando wa buibui.
"IIisikitisha wakati ule," Sir Richard sasa anakumbuka. Anawashutumu wakaguzi kwa "kutokuwa na uwezo wa kikazi" kwa kushindwa kupata chochote. Hans Blix ambaye aliongoza ukaguzi wa Umoja wa Mataifa wa mipango ya siulaha za kikemikali na kibaiolojia, anaiambia BBC kwamba hadi mwanzoni mwa mwaka 2003 , alikuwa naamini kulikuwa na silaha za maangamizi, lakini alianza kushuku uwepo wa silaha hizo baada ya kufika mahala walipoambiwa zipo hawakupata kitu.
Alitaka muda zaidi wa kupata majibu lakini hakupewa.
Kushindwa kupatikana kwa ‘’silaha’’ hakungezuia vita Machi 2003.
"Nilijaribu kuzuia vita hadi muda wa mwisho," Tony Blair aliiambia BBC. Rais George Bush, kwa kuogopa mshirika wake atapoteza kura katika bunge siku moja kabla ya vita, alimpigia simu ya video ambayo ilikuwa ni fursa ya kuzuia uvamizi na kuhusika baada uvamizi, lakini waziri mkuu alikataa.
Alitetea uamuzi wake kama suala la kimsingi katika kutekeleza haja ya kumshughulikia Saddam Hussein, lakini pia kwasababu ya haja ya kuendelea uhusiano wa Uingereza na Marekani . "Ingekuwa na athari muhimuj kwa uhusiano," anasema na kuongeza kuwa: "Nilipokuwa waziri mkuu, hapakuwa na shaka iwe chini ya utawala wa Rais Clinton au Rais Bush, rais yeyote wa Marekani aliyechukua simu kwanza.
Alikuwa ni waziri mkuu wa Uingereza. Leo tuko nje ya Ulaya na Joe Biden anaweza kuchukua simu ya Rishi Sunak fkwanza? Sina uhakika."
Lakini hakuna silaha za maamngamizi zilizopatikana baadaye pia" Yote yalisambaratika ," afisa mmoja wa MI6 anasema, anakumbuka vyanzo tathmini ya ndani. Na hii itaacha athari kubwa na za kudumu kwa majasusi na wanasiasa.