Kijana mwenye umri wa miaka 20 anayemiliki kampuni yenye thamani ya karibu dola bilioni 1

ZEPTO

Chanzo cha picha, COURTESY ZEPTO

Iliyochapishwa

Alifanikiwa kutumia formula ya kawaida katika ulimwengu wa biashara: kutafuta suluhisho la shida.

Lakini kwa upande wa Aadit Palicha, kinachoshangaza zaidi ni ujana wake - ana umri wa miaka 20 tu - na kasi ambayo ameweza kwenda nayo kutoka alipoanza biashara ambayo kwa sasa ina thamani ya dola za Marekani milioni 900.

Palicha ni mwanzilishi mwenza wa Zepto, kampuni ambayo imejiegemeza kuwafikishia wateja kila aina ya bidhaa za vyakula majumbani kwa kutumia muda mfupi zaidi, ndani ya dakika 10 na ambayo kwa sasa inachukuliwa kuwa moja ya kampuni zinazokua kwa kasi zaidi nchini India.

"Imekuwa safari ya kichaa sana. Tulizindua Zepto mnamo Julai 2021 na tangu wakati huo, katika takriban miezi 16-17, tumetoka kwenye mauzo ya sifuri hadi kama dola $ 200 milioni kwa mwaka. Tunatarajia mwelekeo huu wa ukuaji kusababisha ongezeko la mauzo ya $ 1. bilioni kwa mwaka katika robo ya tatu au ya nne ya mwaka huu wa 2023," Palicha alisema wakati wa mahojiano na kipindi cha Radio Business Daily cha BBC.

Lakini wamefanyaje na wamewezaje?

Ilianza tu kama utani wakati wa janga la virusi vya Corona. Palicha na mwanzilishi mwenza, Kaivalya Vohra, walikuwa wakiishi Mumbai na kutafuta wazo la biashara.

"Wakati wa kufungiwa kwa mara ya kwanza (kutokana na Corona), kupata chakula ilikuwa (ngumu). Sehemu nyingi za vyakula zilifungwa na chaguzi za mtandaoni zilichukua siku 6-7 bora, kutokana na hali ilivyokuwa," anasema.

"Kwa sisi wawili ilikuwa ni juhudi kubwa sana kurekebisha hilo na tulipozungumza na majirani zetu - ambao wengi wao walikuwa wakubwa kuliko sisi - tuliona kwamba lilikuwa tatizo kubwa kwao. Kwa hiyo wazo likatujia: kwa nini hatuwapelekei chakula? huo ukawa mwanzo wa Zepto: njia ya haraka, rahisi zaidi, ya kuaminika na safi ya kupata chakula," anaongeza.

Kuwasilishiwa chakula ndani ya dakika 10

Kitu kimoja kinachoitofautisha Zepto na washindani wake ni ahadi yake ya kukufikishia oda yako kwa muda mfupi wa ndani ya dakika 10.

ZEPTO

Chanzo cha picha, COURTESY ZEPTO

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Nini Siri yenu? Kinachojulikana kama maduka yasiyoonekana ama ghost Stores (au maduka makubwa).

"Tunakufikishia ulichotuagiza kwa dakika 10 kimsingi kutokana na mtandao wa maduka madogo madogo au ghost store ambayo tumeshirikiana nayo kote nchini," anasema Palicha.

Anafafanua kuwa mtumiaji anapofungua programu ya Zepto, anakuta orodha ya bidhaa zaidi ya 5,000 zilizopangwa vizuri, lakini nyuma ya hapo, kinachofanywa na mfumo huo ni kumuunganisha mnunuzi na duka ndogo la ghost lililo karibu na mahali ambapo oda hiyo inapaswa kufikishwa. .

Maduka haya yana umaalumu kwenye mtandao na yameratibiwa na kupangwa ili kuboresha mchakato mzima wa kupata na kufunga bidhaa zilizoombwa ili ziandaliwe chini ya sekunde 90.

Kisha, utaratibu umewekwa kwa wale wanaopeleka mzigo -walio karibu na eneo yalipo maduka- anapaswa kufanya hivyo kwa wastani wa umbali usiozidi kilomita 1.7.

"Hiyo haihitaji waende kwa kasi sana. Tunaweza kufikisha kwa haraka kwa sababu ya umbali mfupi badala ya mwendo wa kasi [wa madereva]," anasema Palicha.

Uamuzi wa kuweka muda wa kuwasilisha mzigo kuwa dakika 10 haukuwa matokeo ya kubahatisha, bali ni matokeo ya majaribio waliyofanya kwa uwezekano tofauti na ambayo yalionyesha kuwa wanaweza kupata mapato zaidi kwa chaguo hilo.

"Tuligundua kwamba mara kwa mara wateja wanakuwa wengi ikiwa unawasilisha mzigo ndani ya dakika 10. Kuna wakati ambapo uwasilishaji wa mzigo kwa dakika 30 au 40 unaonekana sawa, lakini kuna matukio ya haraka sana ambapo muda huo haufai - wakati mtu anahitaji wali au cream ya kunyoa lakini mara moja - basi unapata oda zaidi kutoka kwa mteja huyo kwa kuwasilisha kwa muda mfupi wa ndani ya dakika 10," anasema Palicha.

kuhitimisha mafanikio

Hivi sasa, Zepto inafanya kazi katika miji mikuu ya India na ina zaidi ya watu 1,000 wanaofanya kazi katika ofisi zake na makumi ya maelfu ya wasafirishaji.

Walakini, Palicha ni mwangalifu linapokuja suala la kutangaza mafanikio yake.

"Hatujisikii kama tayari tumefanikiwa. Mara tu tutakapokuwa kampuni yenye faida kubwa, inayouzwa hadharani ndipo nitaweka bendera kwenye sakafu na kusema tumefanikiwa. Nadhani tumekuwa tu sasa. . Kwa kweli, kujiamini kuwa tumefanikiwa ni hatari kidogo kwa sababu kuna mengi zaidi tunaweza kufanya, "anasema.

"Unaweza kujisikia vizuri kuhusu hilo. Kampuni yangu ina thamani ya dola za Marekani milioni 900 - ambayo ni pesa nyingi - na nina umri wa miaka 20. Lakini ukweli ni kwamba - kampuni iliyoanzishwa kwa uwekezaji wa dola milioni 1,000$ inaweza kufa wakati wowote kwa makosa madogo matatu, kwa hiyo hadi umalize safari yako [kuifanya kampuni iwe na faida na kwenda kwa umma] ndo useme umefanikiwa vinginevyo inaweza kufa wakati wowote," anaongeza.

"Ikiwa hatutatetereka sasa na kuendelea kufanya kazi kama tulivyofanya, hii ni fursa inayoweza kubadilisha mchezo katika moja ya soko kubwa zaidi nchini," anahitimisha.