AU yakaribisha wito wa Tigray wa mazungumzo ya amani ya Ethiopia

Chanzo cha picha, AFP
Umoja wa Afrika umekaribisha tangazo la waasi wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia kwamba wako tayari kushiriki katika mazungumzo ya amani.
Mkuu wa Kamisheni ya AU, Moussa Faki Mahamat, alisema ni fursa ya kipekee kumaliza mzozo huo na kuwataka waasi na serikali ya Addis Ababa kutekeleza usitishaji vita mara moja.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mapigano yalianza tena mwezi Agosti baada ya miezi kadhaa ya utulivu, lakini siku ya Jumapili uongozi wa Tigray ulisema uko tayari kushiriki katika mchakato wa amani chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika.
Viongozi wa Tigray hapo awali wamekuwa wakikosoa upatanishi unaoongozwa na AU, badala yake walimpendelea Rais wa Kenya anayeondoka Uhuru Kenyatta kuongoza mazungumzo hayo.
Hakujawa na majibu ya moja kwa moja kutoka kwa serikali ya Ethiopia lakini hapo awali imesema ingezungumza wakati wowote, mahali popote.











