Ndege ya Urusi yagongana na ndege isiyo na rubani ya Marekani juu ya bahari nyeusi

Iliyochapishwa

Ndege ya kivita ya Urusi imegongana na ndege isiyo na rubani ya Marekani, na kusababisha ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani kuanguka kwenye Bahari Nyeusi, jeshi la Marekani limesema.

Inasemekana kuwa ndege hiyo isiyo na rubani ilikuwa katika ziara ya kawaida kupiga doria katika anga ya kimataifa wakati ndege mbili za Urusi zilipojaribu kuizuia.

Kamandi ya Umoja wa Ulaya ilisema ajali hiyo ya Jumanne ilitokana na "kitendo kisicho cha kitaalamu cha Warusi".

Vikosi vya Marekani na washirika vitaendelea kufanya kazi katika eneo hilo, iliongeza. Hakuna tamko juu ya tukio hilo kutoka kwa Urusi.

"Ndege yetu ya MQ-9 ilikuwa ikifanya operesheni za kawaida katika anga ya kimataifa iliponaswa na kugongwa na ndege ya Urusi, na kusababisha ajali na hasara kwa MQ-9," taarifa ya Marekani ilisema.

Mara kadhaa kabla ya mgongano huo ndege za kivita aina ya Su-27 zilimwaga mafuta kwenye ndege hiyo isiyo na rubani kwa njia "ya kutojali, isiyojali mazingira na isiyo ya kitaalamu".

Ndege zisizo na rubani za MQ-9 Reaper ni ndege kubwa zisizo na rubani zenye mabawa ya mita 20 (futi 66) zilizoundwa kwa ajili ya ufuatiliaji

Shashank Joshi, mhariri wa jarida la Economist, alisema huenda Warusi walikuwa wakijaribu kuitishia ndege hiyo isiyo na rubani kwa kuwa ilikuwa ikitandaza mawasiliano yao.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, John Kirby, alisema hatua za Urusi kukamata ndege za Marekani si jambo la kawaida katika Bahari Nyeusi, lakini ni mara ya kwanza kwa ndege kama hiyo kuanguka.

Mvutano umeongezeka katika eneo hilo tangu Urusi kunyakua eneo la Crimea mnamo 2014.

Tangu uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine Marekani na Uingereza zimeongeza upelelezi na uchunguzi wa ndege, ingawa hufanya operesheni zaokatika anga ya kimataifa.