Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 11.03.2024
Machester United itafanya kila iwezalo kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na Uingereza Harry Kane, 30, iwapo atapatikana msimu huu wa joto. (Give Me Sport)
Mmiliki mpya wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe anatazamiwa kuidhinisha dau la zaidi ya pauni milioni 100 kwa kiungo wa kati wa Benfica Mreno Joao Neves, 19. (Mirror, via Mail)
Liverpool wamemchagua meneja wa Brighton Roberto de Zerbi, kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann na Ruben Amorim wa Sporting Lisbon kugombea nafasi ya Jurgen Klopp. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United, Manchester City na Liverpool, bado hajafanya mazungumzo ya kandarasi na Bayern Munich ikiwa imesalia chini ya miezi 18 katika mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (90 min)
Arsenal wako tayari kumuuza beki wao Kieran Tierney msimu huu wa joto lakini The Gunners wanataka pauni milioni 20 kwa mlinzi huyo wa Scotland mwenye umri wa miaka 26. (Give Me Sport)
Chelsea bado hawajafanya maamuzi kuhusu mustakabali wa kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, licha ya Tottenham kumtaka. (Caught offside)
Chelsea huenda ikawauza wachezaji 15 katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Football.London)
Manchester United inanuia kuongeza mshahara wa kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 18, mara tatu chini ya mwaka mmoja baada ya kusaini mkataba mpya, ili kumbakisha klabuni hapo hadi 2030. (Sun).
AC Milan bado wanafanya mazungumzo na Arsenal kuhusu uhamisho wa beki wa Poland Jakub Kiwior, 24. (Fichajes, via Team Talk)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi