Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 11.03.2024

Harry Kane akishangilia kuifungia Bayern Munich dhidi ya Lazio kwenye Ligi ya Mabingwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Machester United itafanya kila iwezalo kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na Uingereza Harry Kane, 30, iwapo atapatikana msimu huu wa joto. (Give Me Sport)

Mmiliki mpya wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe anatazamiwa kuidhinisha dau la zaidi ya pauni milioni 100 kwa kiungo wa kati wa Benfica Mreno Joao Neves, 19. (Mirror, via Mail)

Liverpool wamemchagua meneja wa Brighton Roberto de Zerbi, kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann na Ruben Amorim wa Sporting Lisbon kugombea nafasi ya Jurgen Klopp. (Football Insider)

Kieran Tierney

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal wako tayari kumuuza beki wao Kieran Tierney msimu huu wa joto

Kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United, Manchester City na Liverpool, bado hajafanya mazungumzo ya kandarasi na Bayern Munich ikiwa imesalia chini ya miezi 18 katika mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (90 min)

Arsenal wako tayari kumuuza beki wao Kieran Tierney msimu huu wa joto lakini The Gunners wanataka pauni milioni 20 kwa mlinzi huyo wa Scotland mwenye umri wa miaka 26. (Give Me Sport)

Chelsea bado hawajafanya maamuzi kuhusu mustakabali wa kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, licha ya Tottenham kumtaka. (Caught offside)

Conor Gallagher

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher

Chelsea huenda ikawauza wachezaji 15 katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Football.London)

Manchester United inanuia kuongeza mshahara wa kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 18, mara tatu chini ya mwaka mmoja baada ya kusaini mkataba mpya, ili kumbakisha klabuni hapo hadi 2030. (Sun).

AC Milan bado wanafanya mazungumzo na Arsenal kuhusu uhamisho wa beki wa Poland Jakub Kiwior, 24. (Fichajes, via Team Talk)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi