Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Filamu 12 bora zaidi za kutazama Desemba hii
Kutoka kwenye wasifu wa kuigiza filamu za kutisha Nicole Kidman hadi taswira Bob Dylan iliyomshirikisha Timothée Chalamet, hizi ndizo orodha ya filamu za kutazama mwezi huu.
'Beatles '64'
Ilikuwa Februari 1964 ambapo Marekani ilishindwa na Beatlemania. Kikosi cha ‘The Fab Four’ walitumia wiki tatu katika nchi hiyo ambayo walifanikiwa kuwa na ushawishi mkubwa,ambapo ziara yao ilijumuisha kuonekana kwenye kipindi cha ‘The Ed Sullivan Show’, ambacho kilitazamwa na watu milioni 73, pamoja na tamasha lao la kwanza kufanyia huko Washington DC Marekani.
"Ndugu wa Maysles walikuwa waongoza filamu ya moja kwa moja, kama walivyoiita," Tedeschi alisema katika jarida la Rolling Stone.
"Katika picha hiyo, unaweza kuona kwamba nyota hao ‘Beatles’wakiwa na utulivu sana. Wana mvuto hasa kwenye kamera. Lakini hata mashabiki, wasichana waliojitokeza mbele ya jengo la Plaza Hotel,au kile tunachokiita Ukumbi wa Sullivan sasa - pia wana mvuto sana.
Kuna kitu kuhusu nguvu za Al na David ambacho kiliwatuliza watu, na kuwaruhusu kutayarisha filamu."
Iliachiliwa rasmi 29 November katika jukwaa la Disney+
'The Return'
Ralph Fiennes na Juliette Binoche waliigiza katika The English Patient pamoja mwaka wa 1996, na wamekutanishwa tena katika The Return, filamu nyingine ya aina yake kuhusu makovu ya kiakili na kimwili yaliyosababishwa na vita.
Iliandikwa na kuongozwa na Uberto Pasolini, filamu ya mfululizo swords-and-sandals inatokana na sehemu ya mwisho ya The Odyssey ya Homer, ambamo Odysseus (Fiennes) anarejea Ithaca baada ya muongo mmoja wa kupambana na Trojans na muongo mwingine wa kupambana na viumbe vikubwa vya kutisha.
Mkewe mvumilivu Penelope (Binoche) amekuwa akihangaika na wanaume wengi ambao walijaribu bahati zao kwake, lakini Odysseus huenda pia anajeruhiwa akiingilia jambo hilo kabla ya kuchelewa.
"Ni mbaya yenye umwagaji damu, lakini imezingatia na kupima kila neno," anaeleza Steve Pond katika The Wrap.
Uso wake unaonyesha matatizo na mapambano ambayo mhusika amepitia, na sauti yake ni ya ustadi sana, na kuongeza kina na hisia katika matendo yake.
Imezinduliwa tarehe 6 Disemba nchini Marekani
'Better Man'
Better Man ni filamu ya 2024 kuhusu wasifu wa mwimbaji wa pop Muingereza Robbie Williams. Iliandikwa, kutayarishwa kwa pamoja na kuongozwa na Michael Gracey. Williams anaonyeshwa kama sokwe akiwa na CGI, akiigiza na Jonno Davies kwa kutumia mwendo.
Better Man ilionyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye Tamasha la Filamu la 51 la Telluride mnamo tarehe 30 Agosti 2024.
Tamasha hilo limeratibiwa tena nchini Marekani tarehe 25 Desemba na Paramount Pictures na nchini Australia tarehe 26 Desemba na Roadshow Films.
Nightbitch ni filamu ya ucheshi na kutisha kwa wakati mmoja kutoka Marekani iliyotoka mwaka 2024,iliandikwa na kuongozwa na Marielle Heller,kutoka kwenye riwaya ya 2021 ya Rachel Yoder iliyoitwa (Can You Ever Forgive Me?
Nyota Amy Adams ameigiza kama mama aliyechoshwa na shughuli za nyumbani huku akimlea mtoto mchanga wa kiume.
Anahisi kuwa amepoteza utambulisho wake kama msanii, haendani na akina mama wenzake wa mijini na mumewe (Scoot McNairy) hapendi anachopitia.
Nightbitch ni kuhusu hitaji la mama kuwa huru
Nyota waliong’aa katika filamu hiyo Ammy Adams,Scoot McNairy, Arleigh Snowden, Emmett Snowden, Mary Holland, Ella Thomas, Archana Rajan, na Jessica Harper.
Nightbitch ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la Toronto la 2024, mnamo Septemba 7, 2024,na limeratibiwa kuonyeshwa katika onyesho nchini Marekani na kampuni ya Searchlight Pictures mnamo Desemba 6, 2024,kadhalika Canada, Uingereza na Ireland.
'The Count of Monte-Cristo'
Mwaka jana, kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Kifaransa ya Dimitri Rassam, Chapter 2, ilitoa filamu mbili za kifahari kutoka kwa Alexandre Dumas' The Three Musketeers.
Kana kwamba hiyo haitoshi, kampuni hiyo sasa imekamilisha maboresho mengine ya Dumas, mkasa wa saa tatu kupitia riwaya yake ya kawaida ya kisasi, kujificha na mchezo wa mapanga.
The Count of Monte-Cristo. Pierre Niney anaigiza kama Edmond Dantès, baharia ambaye anatuhumiwa kwa uhaini mwanzoni mwa Karne ya 19. Amefungwa katika gereza la kisiwani kwa miaka mingi, lakini mfungwa mwenzake anamweleza juu ya siri iliyofichwa, na hatimaye alipiza kisasi.
"Maboresho ya hali ya juu yanasimama kama mojawapo ya matoleo bora zaidi ya kazi ya Dumas hadi sasa, anasema Linda Marric katika jukwaa la HeyUGuys.
Kuzinduliwa tarehe 20 Disemba nchini Marekani.
'Kraven the Hunter'
Umekuwa mwaka tulivu kwa filamu za mashujaa, lakini tayari kumekuwa na seti mbili katika Spider-Man Universe ya Sony, yaani, zinahusu wahusika wasaidizi kutoka Jumuia za Marvel's Spider-Man, lakini hazimuhusishi Spidey mwenyewe.
Aaron Taylor-Johnson anaigiza kama mwindaji wa wanyama wakubwa nchini Urusi na mwenye nguvu na hisia kali.
Huenda Sony haitaki mimi kuongoza kwa hili’’Chandor alieleza lakini filamu hiyo ni mkasa wa janga.Lakini ukifuatilia kwa umakini hutaweza kutaraji filamu hii kuwa na mwisho wa kusisimua.
Imeongozwa na J. C. Chandor kutoka filamu ya Richard Wenk na timu ya uandishi ya Art Marcum na Matt Holloway, filamu hiyo nyota Aaron Taylor-Johnson, pamoja na Ariana DeBose, Fred Hechinger, Alessandro Nivola, Christopher Abbott, na Russell Crowe.
Itaachiliwa 12 December katika sinema kimataifa
'The Lord of the Rings: The War of the Rohirrim'
The Lord of the Rings: The War of the Rohirrim ni filamu inayotoka hivi karibuni chini ya muongozaji Kenji Kamiyama kutoka filamu ya Jeffrey Addiss & Will Matthews na Phoebe Gittins & Arty Papageorgiou, kwa mujibu wa mtengenezaji J. R. R. Tolkien.
Imetolewa na New Line Cinema, Warner Bros Animation, na Sola Entertainment kwa ushirikiano na WingNut Films, kukiwa na waigizaji nyota Brian Cox, Gaia Wise, Luke Pasqualino, na Miranda Otto.
The War of the Rohirrim inasimulia hadithi ya Helm Hammerhand (Cox), mfalme mashuhuri wa Rohan, na familia yake wanapotetea ufalme wao dhidi ya jeshi la Dunlendings.
Jackson ni mtayarishaji mkuu na mwandishi mwenza Phillipa Boyens,mtayarishaji. Lakini The War of the Rohirrim ni tofauti na kazi za awali.
Miongo miwili mfululizo kabla ya filamu ya Jackson,inaichukua simulizi hii kutoka katika riwaya ya Tolkien,ambapo wahusika wake wakuu hawajawahi kuonekana hapo kabla.
Pia imeongozwa na rai awa Japani Kenji Kamiyama,ambaye ametengeneza filamu ya vibonzo katika mtindo wa kijapani.
Kuachiliwa katika jukwaa la kimataifa 11 December
'Mufasa: The Lion King'
The Lion King imekuwa filamu bora iliyo katika mtindo wa vibonzo,Inasimulia kisa cha jinsi baba yake Simba yatima, Mufasa, alivyofunga safari yake ya hatari hadi nchi ya Pride, iliyosikika kwenye nyimbo mpya za Lin-Manuel Miranda. Sehemu ya kushangaza zaidi ya filamu hiyo ni mwongozaji wake, Barry Jenkins, ambaye anafahamika zaidi kwa tamthilia yake iliyoshinda tuzo ya Oscar, Moonlight.
"Niliona hadithi hiyo ikivutia sana," Jenkins alisema katika The New York Times. "Kuna mhusika huyu ambaye tunamjua kama mkuu wa asili au wa kifalme, na tunaingia ndani na kuchunguza jinsi mtu huyu alikotokea.
Pia tunaangalia ni nini kinachowafanya watu wengine kuwa wazuri na wengine wabaya, na kwa namna gani watu hutofautiana kwa namna moja au nyingine."
Ilizinduliwa tarehe 18 Disemba katika kumbi za sinema za kimataifa
'Nosferatu'
Nosferatu ni filamu ya kutisha ya Marekani ya 2024 iliyoandikwa na kuongozwa na Robert Eggers. Ni marudio ya filamu ya Kijerumani ya 1922, ambayo kwa upande wake ilitokana na riwaya ya Bram Stoker ya 1897 iliyoitwa Dracula.
Nyota wa filamu hiyo Bill Skarsgård, Nicholas Hoult, Lily-Rose Depp, Aaron Taylor-Johnson, Emma Corrin, Ralph Ineson, Simon McBurney, na Willem Dafoe.
Utengenezaji wa filamu hiyo ulianza mwaka wa 2015 wakati Eggers alipopanga kuifanya filamu yake ya pili, akiielezea kama kazi aliyoipenda, lakini hatimaye akabadili uamuzi na kuchelewesha mchakato huo.
Skarsgård na Depp waliigiza kama viongozi mnamo Septemba 2022. Hoult alijiunga na waigizaji wengine mwezi uliofuata, huku waigizaji waliosalia wakithibitishwa mwanzoni mwa utayarishaji.
Filamu ilifanyika hasa katika Studio za Barrandov huko Prague kati ya Februari na Mei 2023.
Uzinduzi wake ni tarehe 25 Disemba nchini Marekani, Canada, Mexico na Uhispania
'That Christmas'
Simulizi kadhaa zilizoingiliana kwa picha za kuvutia zilifaa Zaidi kwa msimu wa sikukuu nchini Uingereza?
Mvulana mwenye haya ambaye anapata kigugumizi mbele ya mbele ya msichana anayempenda?
That Chrismas inaweza kuwa filamu katika mtindo wa vibonzo lakini ni rahisi kukisia kwamba iliandikwa na Richard Curtis, mtunzi mahiri wa mahaba ambaye aliandika na kutayarisha filamu ya Love Actually.
Kuzinduliwa tarehe 6 Desemba kwenye jukwaa la kimataifa Netflix.
'A Complete Unknown'
Ni filamu yenye simulizi ya hisia kuhusu historia ya Maisha iliyoongozwa na James Mangold, ambaye aliandika filamu hiyo pamoja na Jay Cocks.
Filamu hiyo imetokana na kitabu cha 2015 Dylan Goes Electric! Newport, Seeger, Dylan, and the Night That Split the Sixties na Elijah Wald, filamu inahusu utata unaozunguka kubadili kwa ala zilizoimarishwa kwa umeme na Bob Dylan.
Timothée Chalamet (ambaye ameshiriki kuitayarisha) amecheza kama Dylan, na Edward Norton, Elle Fanning, Monica Barbaro, Boyd Holbrook, na Scoot McNairy wakiwa miongoni mwa washiriki.
Jina la filamu limetokana na maneno ya wimbo wa Dylan wa 1965 "Like a Rolling Stone".
'Baby girl'
Babygirl ni filamu ya kusisimua ya Kimarekani ya 2024 iliyoandikwa, kuongozwa na kutayarishwa na Halina Reijn. Imechezwa na nyota Nicole Kidman, Harris Dickinson, Sophie Wilde, na Antonio Banderas.
Filamu hii inachunguza ugumu wa mabadiliko ya mamlaka na jinsia katika mazingira ya kazi wakati Mkurugenzi Mtendaji wa cheo cha juu (Nicole Kidman) anapoanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi aliyekwenda kujifunza kwa vitendo (Harris Dickinson), ambaye ni mdogo kwa umri.
Kuzinduliwa tarehe 25 Disemba nchini Marekani
Imetafsiriwa na Martha Saranga